Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 5/1 kur. 195-199
  • Ujihadhari na Kinaya!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ujihadhari na Kinaya!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • JE! KRISTENDOMU YU KARIBU KUANGUKA?
  • HATARI YA KINAYA YAONYESHWA MFANO
  • YEHOVA SI MKINAIFU JUU YA WAVUNJA AGANO
  • MAULIZO YANAYOSTAHILI KUJIBIWA
  • Yehova Achomoa Upanga Wake Kutoka Ala!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Kitabu Cha Biblia Namba 28—Ezekieli
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Kutii Onyo la Kimungu Ni Hekima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Kimbilio Lao—Ni Uwongo!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 5/1 kur. 195-199

Ujihadhari na Kinaya!

Makala hii ni ya kutumia kwa mafunzo ya kitabu ya kundi

1, 2. Ni maneno gani ya Yesu wanaosema hawataki kuzungumza juu ya dini wanapaswa kufikiria?

JE! WEWE umepata kusema, unaposemeshwa na mwanafunzi wa Biblia: ‘Mimi naona kwamba dini ni jambo la kipekee, si la kuzungumza. Mimi sitaki akili zangu ziamshwe, zichafuliwe’? Je! wewe unapendelea kuwa mkinaifu? Hata hivyo Yesu Kristo mwenyewe alisema juu ya nyakati zetu:

2 “Jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”​—Luka 21:34-36.

3-5. Biblia na uhakika mwingine vinaonyesha nini kwa habari ya kinaya yenye msingi wa maoni yasiyohakikishwa?

3 Bila shaka, kinaya na uradhi, pamoja na amani ya akili, chaweza kuwa chema. Lakini kinaya chenye kutegemea juu ya matumaini au mawazo yasiyo na msingi chaweza kuwa chenye hatari zaidi.

4 Kwa mfano, si jambo la hekima mtu kukaa nyumbani mwake katika hali ya kukinai wakati maonyo ya dhoruba na ya kuondoka yanapotolewa kwa radio. Kwa hakika mithali ya Biblia imeonekana kuwa ya kweli juu ya watu wengi kama hao, wasiosikia maonyo: “Mjinga hasikii na hupata huzuni, na wapumbavu wanaharibiwa na kinaya chao wenyewe.”​— Mit. 1:32, The New English Bible.

5 Huenda wengine wakabisha juu ya maonyo kama walivyofanya wenyeji katika maeneo fulani yaliyopatwa na mafuriko ya maji hivi karibuni. Taarifa ilisema hivi: “Watu wakinaifu, wakifikiri wamelindwa kwa sababu ya kingo na kazi nyingine za kuzuia mafuriko ya maji zilizojengwa baada ya ‘mafuriko yenye miaka mia moja’ yenye kujulikana sana ya mwaka wa 1946, walikataa kutii maonyo kwamba mafuriko mabaya zaidi huenda bado yakaja.”

6. Ni jambo gani la upumbavu zaidi kuliko kinaya wakati wa onyo kama la mafuriko, dhoruba, na mambo kama hayo?

6 Lakini namna gani juu ya onyo la kimungu, zaidi ikiwa onyo hilo lilikuwa limetolewa kwa miaka mingi, na ikiwa uchunguzi usio wa upande mmoja wa mambo ya hakika ulionyesha kwamba onyo hilo lilihesabiwa haki? Je! hapo kinaya kisingekuwa upumbavu hata zaidi?

JE! KRISTENDOMU YU KARIBU KUANGUKA?

7-10. Maandishi ya makanisa ya Kristendomu yanaonyesha nini juu ya lazima ya kuiacha nia ya ukinaifu, mtu kuona yuko salama ndani yake?

7 Kuna onyo hilo, na onyo hilo ni juu ya kuanguka kwa dini za Kristendomu, pamoja na mjengo wa jamii ya watu ambao katika huo dini hizi zinaunganishwa. Lakini je! mambo ya hakika yanahesabu onyo hilo kuwa haki na lazima ya kuacha nia yenye kinaya, ikiwa mtu ni mshiriki wa mojawapo za taratibu hizi za makanisa?

8 ‘Basi, fikiria maandishi ya makanisa. Je! kweli wameinua kanuni za adili za watu, hata za washiriki wao wenyewe? Kuliko hivyo, je! hawakuufuata ulimwengu, wakiziacha kanuni na kujishusha wenyewe kwa kadiri ambavyo kuwafuata kusingekuwa na tofauti ya kufuata tengenezo lo lote la kilimwengu? Je! makanisa yameonekana yenye kuwafanya washiriki wao wawe tofauti, au kuwatayarisha vizuri zaidi waishi maisha safi, zenye adili?

9 Namna gani siasa, kugawanyika kwa mataifa, na vita? Dini za Kristendomu hazikuwaonya watu juu ya hatari, zaidi, ubatili wa kutegemea wanadamu. Pahali pake, wameunga mkono utawala wa wanadamu na kuendeleza utukuzo wa mataifa. Mara nyingi wamefika hata kwa kadiri ya kuwaagiza washiriki wao watu wa kupigia kura katika uchaguzi wa kisiasa. Wamefanyiza na kutia moyo mauaji makubwa ya watu, kutia na watu wasio askari, katika vita vyenye umwagaji mwingi wa damu.

10 Kwa hiyo, je! imempasa mtu anayeshirikiana na dini katika sehemu ya ulimwengu inayoitwa ya Kikristo ajione kwamba yuko salama? Je! asadiki ya kwamba, bila kujali linalotukia, Kristendomu hawezi kuanguka, kwa hasara yake mwenyewe?

HATARI YA KINAYA YAONYESHWA MFANO

11-13. Mwenendo na hali ya viongozi wa Yerusalemu vilikuwa nini katika mwaka wa 612 B.C.E., miaka mitano tu mbele ya uharibifu wa Yerusalemu?

11 Mtu ye yote akielekea kuwa mkinaifu na asiyesikia ujumbe wa kuonya kwamba msiba u karibu kuja juu ya Kristendomu, na aufikirie mfano wa Biblia ambao bila shaka utamwamsha katika kukinai kwake.

12 Mfano huo ni ule ambao haungetumiwa leo, zaidi katika nchi za Magharibi. Hata hivyo, ni wenye nguvu sana na wa kweli kwa kadiri mfano unavyoweza kuwa.

13 Mfano huu ulipewa kwa nabii Ezekieli yapata miaka mitano tu mbele ya uharibifu wa Yerusalemu. Ezekieli, katika njozi, aliona wanaume wenye kinaya 25. Walikuwa wakuu wa Yerusalemu. Kama watu wa mji wenye cheo, washauri wa mfalme, walikuwa wakitoa shauri baya kwa Yerusalemu. Hawakuwa wakitenda tofauti na maonyo yaliyotolewa na manabii Ezekieli na Yeremia tu, bali inaelekea sana walikuwa wakimtia moyo Mfalme Sedekia aasi juu ya Babeli na kuvunja agano ambalo alikuwa amelifanya kwa kuapa mbele za Mungu. (2 Nya. (Sik.) 36:11-13; 2 Fal. 24:18 mpaka 25:1) Walikuwa wakitegemea uwezo wa kijeshi wa Misri, ‘mkono wenye nyama,’ ili kuwaokoa. Kwa maana haikuwa imemalizika miaka mitatu kufuata njozi ya Ezekieli (612 B.C.E.) kwamba Mfalme Sedekia akaasi, kwa ukubali wao.

14, 15. Ni mfano gani ambao Mungu alimpa Ezekieli katika njozi?

14 Kwa hakika Mungu alisema hivi kwa Ezekieli katika njozi na mfano ambao alimpa nabii. Ezekieli anatoa taarifa hivi:

15 “Tena roho ikaniinua, ikanileta hata lango la upande wa mashariki wa nyumba ya [Yehova], lililoelekea upande wa mashariki; na tazama, mahali pa kuingilia pa lango walikuwako watu ishirini na watano; na katikati yao nikamwona Yaazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, nao ni wakuu wa watu. [Yehova] akaniambia, Mwanadamu, hawa ndio watu wale watungao uovu, na kutoa mashauri mabaya ndani ya mji huu; wasemao, Wakati wa kujenga nyumba si karibu; mji huu ni sufuria na sisi tu nyama.”​—Eze. 11:1-3.

16. Eleza maana ya mfano huo.

16 Wakuu hawa wa kiserikali na washauri wa Mfalme Sedekia walijiona kukinai ndani ya Yerusalemu mji wenye kukazwa sana kwa ngome. Kuta za mji zilikuwa kama kingo za sufuria, zisizovunjika, kama walivyofikiri. Kama nyama inayopikwa ndani ya sufuria, wasingetolewa nje, kuondolewa. Washauri walijiona kwamba wangeweza kuendelea kukaa humo kwa kuomba msaada kutoka kwa mfalme wa Misri juu ya Babeli. Basi wakawaza kwamba ulikuwa wakati wa kujenga nyumba, wakitumaini kukaa ndani yake kwa muda mrefu.

17, 18. Maneno ya Ezekieli yalitoaje onyo kwa wakuu wa watu katika Yerusalemu?

17 Wakinaifu, wenye kiburi na wanaobaki wa watu katika Yerusalemu walihitaji kuonywa. Kwa hiyo Mungu alimwamuru Ezekieli atoe unabii ulioonekana kuwa mkali na wenye nguvu sana. Yehova alisema hivi:

18 “Mmesema maneno hayo, Enyi nyumba ya Israeli; maana mimi nayajua yaingiayo katika mioyo yenu. Mmewaongeza watu wenu waliouawa ndani ya mji wenu, nanyi mmezijaza njia kuu zake waliouawa. Basi Bwana [Yehova] asema hivi; Watu wenu waliouawa, ambao mmewalaza katikati yake, hao ndio nyama hiyo, na mji huu ndio sufuria; lakini ninyi mtatolewa nje kutoka katikati yake.”​—Eze. 11:5-7.

19. Pahali pa wakuu kubaki wakiwa salama katika Yerusalemu kama ‘nyama katika sufuria,’ ni akina nani wangebaki, na jambo gani lingetokea kwa wakuu?

19 Watu hawa walikuwa wamezidi mno hata kuwaua wale waliokuwa katika mji waliopendelea kuendelea kunyenyekea Babeli. Lakini Mungu alionyesha kwamba, pahali pa wakuu hawa kuendelea kukaa ndani ya Yerusalemu, kama walivyodhania, ni wale ambao walikuwa wameua ndio wangeendelea kukaa humo. Wangekuwa wakuu wenye kiburi ndio wangevutwa kutoka katika nyumba zao na Wababeli. Wangeziona nyumba zao zikichomwa mbele ya kuanguka kwao kwa upanga wa mfalme wa Babeli. Ezekieli aliwaambia wakuu hao hivi:

20-22. (a) “Upanga” ambao Yehova angeleta ulikuwa nini, na “wageni” ambao wangeutumia walikuwa akina nani? (b) Mungu aliwahukumuje wakuu “katika mpaka wa Israeli”?

20 “Ninyi mmeuogopa upanga; nami nitauleta upanga juu yenu, asema Bwana [Yehova]. Nami nitawatoa ninyi nje kutoka katikati yake, na kuwatia katika mikono ya wageni, nami nitafanya hukumu kati yenu. Mtaanguka kwa upanga; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi [Yehova]. Mji huu hautakuwa sufuria lenu, wala ninyi hamtakuwa nyama ndani yake; nitawahukumu katika mpaka wa Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni [Yehova]; kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.”​—Eze. 11:8-12.

21 Bila shaka, maneno haya yanaonyesha kwamba kweli Yehova angekuwa ndiye mwenye kutekeleza hukumu juu ya hawa watunga mashauri wenye ukinaifu. Lakini katika kufanya hivyo yeye angeutumia “upanga” mikononi mwa “wageni,” Wababeli, ndio wafanye kazi yenyewe ya kuua. Wale ambao wangeokoka kuuawa kwa “upanga” wasingekuwa salama ndani ya kuta za “sufuria” hilo la mfano, Yerusalemu. Wakivutwa nje, wangehukumiwa “katika mpaka wa Israeli.” Na ilitukia hivyo. Ilikuwa upande wa kaskazini wa eneo hilo lililokuwa limeshindwa na Mfalme Daudi, yaani, katika Ribla kuelekea Hamathi, ndiko yafuatayo yalikotukia:

22 “Naye amiri wa askari walinzi akamtwaa Seraya, kuhani mkuu, na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinzi watatu wa mlango; na katika mji akatwaa towashi mmoja aliyewasimamia watu wa vita; na watu saba katika wale waliouona uso wa mfalme, walioonekana katika mji; na karani wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana ndani ya mji. Na Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawatwaa, akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla. Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Ndivyo Yuda alivyochukuliwa utumwani, akatolewa katika nchi yake.”​—Yer. 52:24-27.

YEHOVA SI MKINAIFU JUU YA WAVUNJA AGANO

23. Yehova alionyeshaje kwamba si mkinaifu kwa wale wanaovunja agano lake?

23 Kwa njia hiyo Yehova alionyesha kwamba yeye ni Mwenye Kushika Agano asiyeshindwa. Yeye si mkinaifu juu ya mapatano ambayo anafanya. Yeye anatimiza ahadi, naye hatawaachilia wale wasioaminika kwa mapatano yao na wanaoziasi sheria za Mungu na kwa ukinaifu wanajiona kwamba haileti tofauti, na ya kwamba wako salama. Alisema waziwazi kwa wale wakinaifu katika Yerusalemu hivi: “Nitawahukumu.” Kwa sababu gani? “Kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.”​—Eze. 11:11, 12.

24. (a) Kristendomu ameonyeshaje kwamba yeye anajifikiri mwenyewe kuwa katika ujamaa wa agano na Mungu? (b) Viongozi wa Kristendomu wametenda kama wale wakuu namna gani, washauri wa uongo wa Yerusalemu?

24 Kama Israeli wa kale, je! Kristendomu wa kisasa amejidai kuwa katika uhusiano wa agano pamoja na Mungu? Ndiyo. Yeye amegawa mamilioni ya nakala za Biblia katika zaidi ya lugha elfu moja. Biblia hizi zimehakikisha jina lake la kimungu kama likiwa Yehova au Yahweh. Yeye anajidai kwamba mpatanishi wake kati ya Mungu huyu na wanadamu ni Yesu Kristo Mwana wa Mungu, na ya kwamba yeye yu katika “agano jipya” pamoja na Mungu. (Yer. 31:31-34; Luka 22:20; 1 Tim. 2:5, 6) Walakini, yeye amevunja sheria zake, amevunja agano lake pamoja na Mungu. Kuongeza kwa hatia yake ya damu ameachilia ufisadi kati ya washiriki wake wa kanisa, na akatangaza kwamba Mungu amefariki, kwamba yeye hapendezwi na wanadamu na hashiriki katika habari ya historia. Kweli, mapadre wake wanasema kwamba yeye amelisahau agano lake jipya. Wakati onyo linapotolewa kwao wanalipuza, hata kulidhihaki. (2 Pet. 3:3, 4) Kama washauri wa Mfalme Sedekia wa Yuda, wanatabiri mambo mema juu ya mipango ya Kristendomu ya kidini, ya kisiasa na ya kibiashara, wakiwaambia watu waweke tumaini lao katika ‘mkono wenye nyama,’ na kwa hakika wakiwafanya washiriki wao wa kanisa wakikaa kwa ukinaifu.​—Yer. 6:14.

25. Viongozl wa Kristendomu wanaonaje, sawasawa na wakuu wa Yerusalemu?

25 Kristendomu hana ukuta wa mawe kumzunguka kama ulivyokuwa mji wa kale wa Yerusalemu. Hata hivyo, mapadre na viongozi wake huenda wakajiona kama walivyojiona wakuu wa Yerusalemu, kwamba Kristendomu yuko mahali pa salama, kama vile nyama ndani ya chombo cha chuma. “Ukuta” wake ni kile ambacho anatumaini, nguvu za kivita za mataifa. Yeye anaunga mkono utawala wa wanadamu, zaidi kupitia kwa tengenezo la ulimwengu kama Umoja wa Mataifa. Kwa kweli, Federal Council of Churches of Christ in America iliuita ule uliotangulia, yaani, Ushirika wa Mataifa “wonyesho wa kisiasa wa ufalme wa Mungu duniani.”

26, 27. Ezekieli alipokuwa akitazama njozi, ni jambo gani la ajabu lilifuata?

26 Je! Yehova atafanya lo lote juu ya matendo ya Kristendomu ambayo yameshutumu jina lake? Je! yeye atawaamsha viongozi wa uongo wa kidini na vile vile wanasiasa hao wanaojidai kwamba mataifa ambayo wanaongoza ni mataifa ya Kikristo? Je! wataamshwa katika hali yao ya ukinaifu? Angalia yaliyotukia katika habari ya Ezekieli:

27 “Ikawa, nilipotoa unabii, Pelatia, mwana wa Benaya, akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, Ee Bwana [Yehova], je! utawakomesha kabisa mabaki ya Israeli?”​—Eze. 11:13.

28. Ezekieli alionaje juu ya kifo cha Pelatia katika njozi?

28 Katika njozi, kilikuwa kitu gani kilichomfanya Pelatia mkuu aanguke hali amekufa wakati Ezekieli alipokuwa amemaliza kutoa unabii na kutoa onyo juu ya “wakuu wa watu” 25? Kulingana na alivyolia kwa sauti kuu kwa kuogopa, nabii Ezekieli alikuona kuwa kufikilizwa kwa mara moja kwa hukumu kutoka kwa Yehova. Alikuona kama ishara si ya kukaribia kwa kifo kwa wakuu wengine 24 tu, bali, ole! vile vile ya kukomeshwa kabisa kwa wote “mabaki ya Israeli.” Walakini, yeye hakutilia shaka haki ya Mungu kuwakomesha wote kabisa.

29. Kwa sababu ya ambayo Mungu alifanya juu ya Yerusalemu, ni maulizo gani tunaweza kuuliza juu ya Kristendomu?

29 Kwa namna Mungu alivyowatazama watu hawa katika Yerusalemu waliovunja agano lake na kwa kinaya wakajiona wenyewe kuwa salama katika kutumaini kwao kwa kimwili uwezo wa kilimwengu, Mungu anamtazamaje Kristendomu na viongozi wake? Je! atawaacha waendelee kusema “Mungu amefariki,” wazipuze sheria za agano lake jipya ambalo katika hilo wanajidai kuungana na yeye, na kulidhihaki onyo kutoka katika Neno lake Biblia, linalotangazwa waziwazi sasa?

30. Watu wakinaifu wanapaswa kufanya nini, ama sivyo msiba wao utakuwa nini?

30 Ikiwa ye yote ameelekea kuwa mkinaifu, asiyemtumikia Mungu sana na kuliangalia Neno lake au onyo la kukaribia kwa ‘dhiki kubwa,’ imempasa ajihadhari! Imempasa aamke kutoka katika hali yo yote ya usingizi, ya ulegevu, awe macho na kusikia atakachosema Mungu. Kama sivyo, Mungu atakuwa akitenda kabisa kupatana na hukumu na haki katika kumwangamiza wakati wa hatari inayokuja juu ya ulimwengu huu.

MAULIZO YANAYOSTAHILI KUJIBIWA

31, 32. Kutokana na kuchunguza kwetu kwa unabii huu wa Ezekieli, ni woga gani huenda ukachochewa, na ni maulizo gani huenda watu wengine wakauliza?

31 Kama vile Ezekieli alivyoogopa kuharibiwa kwa watu wote wa Yehova wa agano wakati wa uharibifu wa Yerusalemu uliokuwa ukikaribia, huenda woga ule ule ukaipata mioyo ya watu wenye kuelekea dini wasiofahamu tofauti kati ya Kristendomu na Ukristo wa kweli. Je! nia ya Kristendomu kwa Mungu na kushindwa kwake maana yake ni kwamba Ukristo umeshindwa?

32 Kwa kufikiria mambo haya, huenda kwa kuogopa mtu akaongozwa kuuliza ulizo hivi, ‘Ikiwa katika “dhiki kubwa” inayokuja juu ya taratibu nzima ya mambo Yehova anamkomesha kabisa Kristendomu na rafiki zake za kilimwengu, je! hii itamaanisha uharibifu wa Ukristo wote wa kweli?’

33. Je! kuna watu ambao wangetaka kuharibu, si Ukristo wa kinafiki wa uongo tu, bali vile vile na ibada ya kweli?

33 Kuna wale ambao wangependa iwe hivyo. Ukomunisti na watu wengine wenye kutaka mageuzi wanaochukia Ukristo wa Biblia wangependa kushiriki katika kuufutilia mbali, si Ukristo wa unafiki tu wa Kristendomu, bali vile vile “dini iliyo safi,” ibada ya kweli ya Kikristo ya Mwenye Enzi Yote Bwana Yehova.​—Yak. 1:27.

34. Ni maulizo gani yanabaki kujibiwa, na watu wenye unyofu wa moyo watafanya nini?

34 Je! watu hawa wenye kutaka mageuzi wasio wa kidini wataridhika kuona Ukristo unafutwa katika dunia? Au kutakuwako upambanuzi kati ya dini ya uongo yenye unafiki na Ukristo wa kweli, ili Ukristo uokoke? Tukikumbuka kwamba, ijapokuwa serikali za kilimwengu zitatumiwa katika kumharibu Kristendomu, kwa kweli ni hukumu ya Mungu ndiyo inayofikilizwa, tutatazamia yale yaliyofuata kusikiwa na nabii Ezekieli kutoka kwa Mungu. Haya yatazungumzwa katika toleo litakalokuja la gazeti hili. Kwa sasa, watu wenye mioyo minyofu hawatakuwa wenye kinaya, bali watakuwa wakichunguza ili waone yaliyo mapenzi ya Mungu kwao, ili wapate kuamua ni njia gani, ikiwapo, Mungu ametoa kwa wokovu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki