Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 9/1 kur. 399-402
  • Kutii Onyo la Kimungu Ni Hekima

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutii Onyo la Kimungu Ni Hekima
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • ONYO LA KUFIKIRIWA
  • Wakati wa Kuwapo kwa Mlinzi kama Ezekieli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Kitabu Cha Biblia Namba 28—Ezekieli
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Sikiliza—Mlinzi wa Yehova Anena!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 9/1 kur. 399-402

Kutii Onyo la Kimungu Ni Hekima

Makala hii ni ya kutumia kwa mafunzo ya kitabu ya kundi

1. Matendo ya Yehova kwa wanadamu yametoaje ushuhuda wa kuona kwake ubora mwingi wa uhai wa kibinadamu?

MATENDO ya Yehova kwa wanadamu yameonyesha kuona kwake ubora mwingi wa uhai wa kibinadamu sikuzote. Yeye hakutenda kwa haraka kutoa hukumu mbaya bali kwa rehema ametoa nafasi kwa watu na mataifa kusudi wageuze njia zao. (Yer. 18:6-10) Zaidi hili laweza kuonekana kwa alivyolitendea taifa la Israeli. Mara kwa mara Yehova aliwatokeza manabii walitie taifa hili lisilo aminifu moyo kusudi liuache mwendo wake mbaya.​—Isa. 55:6, 7; Eze. 33:10, 11.

2, 3. Ezekieli kama mlinzi angalijifanyaje mwenye hatia ya damu, na kwa sababu gani kifo cha watu wasioonywa kingekuwa cha haki hata hivyo?

2 Mmojawapo wa manabii hawa alikuwa Ezekieli, aliyeanza kazi yake ya unabii mwaka wa 613 B.C.E. kama mhamishwa katika Babeli. Cheo cha Ezekieli kilikuwa kama kile cha mlinzi aliyekuwa na daraka la kuonya watu wakati wa hatari. Wale walioshindwa kutii onyo ingewalazimu kujilaumu wenyewe kwa kifo chao. Hata kama Ezekieli kama mlinzi angalishindwa kufanya kazi yake, uasi wa watu uliwastahilisha kifo na kwa hiyo kifo chao kisingalikuwa chenye udhalimu. Walakini, Ezekieli angalikuwa mwenye hatia ya kutojali kwa mhalifu. (Eze. 33:1-6) Akikazia hili katika akili ya Ezekieli, Yehova alitangaza:

3 “Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa [nafsi] yako.”​—Eze. 33:7-9.

4, 5. Kuhifadhiwa kwa mtu wakati wa hukumu ya kimungu kunategemea nini?

4 Wale wanaoitikia onyo la Mungu linalotolewa kupitia kwa watumishi wake hawana cha kuogopa kwamba watahesabiwa sifa zao za zamani. Yehova Mungu ‘hakufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi.’ (Eze. 33:11) Bila shaka, watu wenye haki wakiacha mwendo wa uaminifu, hawataepushwa na hukumu mbaya. Kama mtu atakufa au kuendelea kuishi inategemea hali yake wakati wa kutekelezwa kwa hukumu ya kimungu. Akasema Yehova kupitia kwa Ezekieli:

5 “Nimwambiapo mtu mwovu, Hakika utakufa; kama akighairi, na kuiacha dhambi yake, na kutenda yaliyo halali na haki; kama mtu mwovu akirudisha rehani, na kumrudishia mtu mali yake aliyomnyang’anya, akizifuata sheria za uzima, asitende uovu wo wote; hakika ataishi, hatakufa. Katika dhambi zake zote alizozitenda, hata mojawapo haitakumbukwa juu yake; ametenda yaliyo halali na haki; hakika ataishi. Mwenye haki ageukapo, na kuiacha haki yake, na kutenda maovu, atakufa katika maovu hayo. Na mtu mbaya ageukapo, na kuuacha ubaya wake, na kutenda yaliyo halali na haki, ataishi.”​—Eze. 33:14-16, 18, 19.

6. Ni ubishi gani walioufanya Waisraeli wakati wa Ezekieli juu ya matendo ya Yehova yenye rehema?

6 Lo! ni rehema kama nini kwa Yehova kuhakikisha kwamba onyo la kutosha linatolewa! Wakati wa Ezekieli, hata hivyo, walikuwako Waisraeli walioshindwa kushukuru kwa upendo wa Mungu usio na kifani na rehema. Wao walisema: “Njia ya [Yehova] si sawa.” Na hali, wao kwa kweli ndio waliopaswa kugeuza kuwaza kwao na njia zao.​—Eze. 33:17, 20.

7. Kwa sababu gani Ezekieli asingeweza kulaumiwa kwa kifo cha waliokataa kujipatanisha wenyewe na njia za Yehova?

7 Wale wasiolitii onyo la Mungu kupitia kwa Ezekieli lakini walioshikilia kauli ya kwamba njia ya Mungu haikuwa sawa walijiletea msiba mkubwa. Uharibifu wa mji wenye uasi wa Yerusalemu nyuma ya miezi kumi na minane ya mazingiwa yenye kupata nguvu uliwaua wengi. Yeye alikuwa amekwisha wapa onyo Waisraeli wenye kutishwa na msiba. Kwa hiyo damu yao ilikuwa juu yao wenyewe.

8. Kwa sababu ya uaminifu wake, ni mambo gani ambayo hayakumpata Ezekieli na alipata tegemezo gani?

8 Kwa sababu ya uaminifu wake kama mlinzi, Ezekieli hakupata hukumu mbaya mwenyewe. Aliendelea kuishi na kupata uhakika wa kutumainiwa kwa maonyo yake ya unabii juu ya Yerusalemu. Yeye anatoa habari:

9. na maelezo ya chini. Ni lini mshuhudiaji wa uharibifu wa Yerusalemu alipohakikisha ukweli wa aliyokuwa ametabiri Ezekieli?

9 “Ikawa, katika mwaka wa kumi na mbilia wa kuhamishwa kwetu, mwezi wa kumi, siku ya tano ya mwezi, mtu mmoja aliyekuwa ametoroka toka Yerusalemu akanijia, akisema, Mji umepigwa.”​—Eze. 33:21.

10. Yehova alimtayarishaje Ezekieli kwa habari ya mshuhudiaji?

10 Kwa Myahudi wa kawaida au Mwisraeli habari hii ingalikuwa yenye kuvunja moyo. Lakini Yehova Mungu alimweka Ezekieli tayari kwayo. Yehova alijua kwamba mtoro huyu alikaribia mwisho wa utoro wake na karibu kutoa habari. Kwa hiyo katika jioni ya siku ya kufika kwa huyo Yehova alisema kwa Ezekieli akimpa maoni ya kwamba Yerusalemu ulikuwa umeharibiwa na kungali kulikuwako waokokaji katika nchi ya Yuda. Ezekieli anatuambia:

11. na maelezo ya chini. (a) Ni katika maana gani Ezekieli alikuwa amekuwa bubu mbele ya kufika kwa mshuhudiaji? (b) Waokokaji katika nchi ya Yuda walikuwa wakisema nini, na walikuwa wakitendaje?

11 “Basi mkono wa [Yehova] umekuwa juu yangu wakati wa jioni [wakati ambapo siku ya Kiyahudi ilianza], kabla hajafika yeye aliyetoroka; naye alikuwa amenifumbua kinywa changu, hata aliponijia wakati wa asubuhi; na kinywa changu kilikuwa wazi, wala sikuwa bubu tena.b Neno la [Yehova] likanijia, kusema, Mwanadamu, watu wale wakaao mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli husema ya kwamba, Ibrahimu alikuwa mmoja, akairithi nchi hii; lakini sisi tu watu wengi; tumepewa nchi hii iwe urithi wetu. Basi, waambie, Bwana [Yehova] asema hivi; Mnakula nyama pamoja na damu yake, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii? Mnategemea upanga wenu, mnatenda machukizo, mnanajisi kila mtu mke wa jirani yake; je! mtaimiliki nchi hii?”​—Eze. 33:22-26.

12. Kwa sababu gani waokokaji katika nchi ya Yuda wasingeimiliki nchi kama walivyofikiri?

12 Kwa kweli hukumu iliyotekelezwa juu ya Yerusalemu ilistahiliwa. Si kwamba watu kwa jumla walikataa tu kutii onyo, lakini vile vile wale waliookoka katika nchi ya Yuda hawakugeuza njia zao wakiikubali adhabu kali waliyopata. Waliendelea kula nyama ya wanyama wasioondolewa damu kulingana na sheria ya Mungu; wao waliendeleza ibada ya uongo pamoja na sanamu za kuchukiza; waliendelea kufanya tendo lenye kuchukiza la uzinzi, kunajisi hata mke wa jirani yao. Yehova hakujali kwamba wao walikuwa wengi wakilinganishwa na babu yao, mzee wa ukoo Ibrahimu, ambaye kwake nchi ilikuwa imeahidiwa na Yehova. (Mwa. 12:1-7) Kwa sababu ya kutogeuka kwao kutoka kwa njia zao mbovu kwa kutubu, wao hawakustahili kuendelea kuimiliki nchi. (Yer. 42:1–44:25) Wingi peke yake haukuwa wa maana kwa Yehova; utii wa Sheria yake ndio ulikuwa na maana!

13, 14. Yehova alitangaza nini juu ya nchi ya Yuda na waliobaki humo?

13 Wasiotubu hao wasingeachwa wakikaa katika nchi iliyotolewa na Mungu. Nchi ingeachwa ukiwa bila ya mwanadamu wala mnyama wa kufugwa, bila ya mtu kupitia humo kwa sababu ya woga wa kukaliwa kwake na mashetani. Nchi ingeachwa ukiwa kwa njia hii kwa kipindi kizima cha miaka sabini, kusudi kwamba ifurahie kipindi cha sabato, kulipiza miaka yote ya sabato ambayo Wayahudi walikuwa wameshindwa kushika. (2 Nya. (Sik.) 36:17-23; linganisha Danieli 9:1, 2; Yeremia 9:11; 26:9; 32:43; 33:10-12; 34:22.) Yehova alimwambia Ezekieli:

14 “Kama mimi niishivyo, hakika watu wale wakaao mahali palipoharibika wataanguka kwa upanga, naye mtu aliye katika uwanda, nitamtoa na kuwapa wanyama wakali, ili aliwe; na hao walio ndani ya ngome na mapango watakufa kwa tauni. Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa na ajabu, na kiburi cha uwezo wake kitakoma; nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa, asipite mtu. Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ndimi [Yehova], nitakapoifanya nchi kuwa ukiwa na ajabu, kwa sababu ya machukizo yao yote waliyoyatenda.”​—Eze. 33:27-29.

15, 16. Wahamishwa wenzi wa Ezekieli waliitikiaje kutabiri kwake?

15 Si waokokaji hawa peke yao walioshindwa kushukuru kwa upendo mkuu wa Yehova na rehema kwa kufanya onyo litolewe. Wahamishwa wenzi wake Ezekieli hata hawakuchukua kutabiri kwake kwa uzito. Akielekeza kwa wahamishwa hawa, Yehova alisema:

16 “Wana wa watu wako husimulia habari zako karibu na kuta, na ndani ya milango ya nyumba zao, na kuambiana, kila mtu na ndugu yake, wakisema, Haya! twende tukasikie ni neno gani hilo litokalo kwa [Yehova]. Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao. Na tazama, wewe umekuwa kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga kinanda vizuri; maana, wasikia maneno yako, lakini hawayatendi. Na hayo yatakapokuwapo, tazama, yanakuja, ndipo watakapojua ya kuwa nabii amekuwapo kati yao.”​—Eze. 33:30-33.

17. Habari ya uharibifu wa Yerusalemu ilikuwa na matokeo gani kwa waliozidi kutoamini?

17 Kwa sababu ya kutokuwa wasikivu, wahamishwa hao wa Kiyahudi walishangaa ushahidi ulipokuja kwamba Yerusalemu ulikuwa umeharibiwa. Kwa maana walishikilia kauli ya kutoamini, hawakuwa tayari hata kidogo kwa kishindo hiki. Walilazimishwa vile vile kukubali kwamba Ezekieli alikuwa amekuwa nabii wa kweli wa Yehova.

ONYO LA KUFIKIRIWA

18, 19. Ni kwa njia gani wakati wetu unalingana na ule wa Ezekieli?

18 Sisi leo twaishi katika wakati unaofanana sana na ule wa Ezekieli. Ijapokuwa wanajidai kuwa katika ujamaa wa agano na Mungu kama alivyokuwa Israeli wa kale, washiriki wa makanisa ya Kristendomu wanajiongoza wenyewe kama Israeli asiye mwaminifu wa kale. Hali zile zile zilizosimuliwa na mtume Paulo katika 2 Timotheo 3:1-5 zinaonekana waziwazi kati ya wanaojidai kumtumikia Mungu. Twasoma:

19 “Ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake.”

20. Ni akina nani leo wanaofanya kazi kama ile ya Ezekieli?

20 Je! wewe wayaona mambo aya haya leo? Uhakika wa kwamba hali zilizotabiriwa ni alama ya “siku za mwisho” wa taratibu mbovu iliyopo ya mambo unaonyesha kwamba wanadamu wamo hatarini. Kipindi hiki cha wakati kimetabiriwa kufikia upeo katika “dhiki kubwa” itakayoileta taratibu iliyopo isiyomcha Mungu kwenye mwisho wake. (Mt. 24:20-22; Ufu. 7:1-3, 14) Kama vile Ezekieli wa kale alivyotokezwa kama mlinzi kusudi atoe onyo, ndivyo na leo mashahidi wa Yehova wa Kikristo wanavyotangaza onyo juu ya msiba mkubwa utakaompata Kristendomu na vile vile sehemu nyingine yote ya taratibu hii ya mambo yenye hatia ya damu. Je! wewe unaitikiaje onyo hilo? Je! umejitenga mwenyewe na mazoea ya kidini na matengenezo ya Kristendomu? Je! unajiongoza mwenyewe kwa njia ambayo itamfanya Yehova Mungu ahakikishe kwamba utahifadhiwa hai wakati wazoeao uovu watakapofikia mwisho wao?

21. Kwa sababu gani Kristendomu hataokoka uharibifu?

21 Mungu asiye kigeugeu Yehova hatamwachilia Kristendomu na wafuasi wake kama vile asivyomwachilia Yerusalemu asiye mwaminifu. Kama vile Yerusalemu na nchi ya Yuda, mahali ambapo Kristendomu amekalia katika hii taratibu ya mambo ya kilimwengu pataachwa ukiwa kabisa bila ya vyama vyo vyote vya kidini kusalia humo. Vyombo vya taratibu ya leo ya mambo ya ulimwenguni pote vitatazama utupu ulioachwa na Kristendomu na taratibu zile nyingine za kidini za uongo. Kulingana na ambavyo mashahidi wa Yehova wametangaza kwa muda mrefu ulimwenguni pote, vyombo hivyo vya kilimwengu vitalazimishwa kujua yale yaliyoamriwa kwavyo katika kanuni inayorudiwa-rudiwa: “Itawapasa kujua ya kwamba mimi ndimi Yehova.”

22. Leo wengi wanatendaje sawa na wahamishwa wasioamini wenzi wa Ezekieli?

22 Kwa kuwa ndivyo ilivyo, bila shaka wewe hutataka kupatikana kati ya wale wanaofanana na wahamishwa wenzi wake Ezekieli. Lakini, watu wengi leo wanafanya lile lile. Wakiwa kando ya kuta zenye kutoa kivuli chenye kuburudisha, milangoni pa nyumba zao au po pote pengine, watu wanazungumza juu ya mashahidi wa Yehova wa Kikristo na kazi yao ya kuwatembelea wengine nyumba kwa nyumba. Watu wengi, hata kati ya wale ambao wangali wakishirikiana na Kristendomu, wanaeneza heshima nzuri juu ya mashahidi hawa. Hata huenda wakafika kwenye mikutano mikubwa ya watu wote ya mashahidi wa Yehova au kupanga funzo la nyumbani la Biblia liendelezwe pamoja nao na kuwakaribisha majirani au watu wa jamaa waungane nao katika funzo hili. Wao wanaipenda sauti na unyofu wa ujumbe wa kimungu na kuusikiliza kwa heshima. Lakini wanasitasita; hawasimami waziwazi upande wa Yehova kama watumishi wake waliojitoa. Wao wanapenda kufurahishwa tu na ujumbe wenye tegemezo la Kibiblia. Hawataki kuonekana wasiofuata dini kabisa, wakishambuliwa kuwa Wakomunisti wasioamini kuwako kwa Mungu.

23. Kwa sababu gani watu wengi leo hawataki kukubali kwamba mashahidi wa Yehova wa Kikristo ni wanenaji wa kweli wa Mungu?

23 Huenda wakaudhiwa na kelele ya Kristendomu kwamba mashahidi wa Yehova wa Kikristo ni “manabii wa uongo”! Na hali huenda wakawa hawasadiki kabisa kwamba hawa ni wanenaji wa kweli wa Yehova Bwana Mwenye Enzi Yote. Ili wajiache wakubali hivyo ingewalazimu wafanye jambo fulani. Hii ingemaanisha waache kushikilia tamaa mbaya na kufuatia kwa moyo wote faida yenye udhalimu.

24, 25. Kwa sababu ya uharibifu wa Kristendomu unaokuja, kwa sababu gani ni jambo lisilo la hekima kusitasita?

24 Hapana ye yote kati yetu anayetaka kuwa kama wenye kusitasita hawa, wasioitikia. Ni afadhali kujua sasa, kuliko kuchelewa mno, kwamba kuna jamii ya kweli ya kinabii ya Wakristo kati yetu, na kuukubali na kutenda juu ya ujumbe wa Biblia, “si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli.” (1 The. 2:13) Wale wanaongoja bila ya kufanya uamuzi mpaka yale ambayo mashahidi wa Yehova wa Kikristo wamekuwa wakitangaza ‘yatukie’ “ndipo watakapojua ya kuwa nabii amekuwapo kati yao.” (Eze. 33:33) Lakini kujua hivyo wamechelewa hakutamaanisha wokovu kwao, kwa maana mioyo yao na njia zao zitapatikana hazijageuka.

25 Nini kitakachopatikana kwa kusitasita na kutia mashaka mpaka mwisho kwamba Yehova anaweza kutokeza na ametokeza “nabii” wa kweli mnamo kizazi chetu? Bila shaka kufanya hivyo hakutampa ye yote kibali cha kimungu wala ulinzi unaotakiwa wakati wa “dhiki kubwa” inayokuja kasi. Ikiwa njia yetu itakuwa ile ya hekima na imani, basi, Biblia ikiwa mkononi, tutalitii onyo la mlinzi wa kweli wa Yehova na tutakimbilia mahali ambapo Yehova anaonyesha katika Neno lake. Ndipo, mlinzi wa kinabii wa Yehova apatapo habari kwamba Kristendomu amepigwa, sisi, pamoja na yule mlinzi mwaminifu, tutakapoendelea kuishi.

​—Kutoka Kitabu “The Nations Shall Know that I Am Jehovah”​—How?

[Maelezo ya Chini]

a Ziko, hati nane za Kiebrania mbali na Tafsiri ya Syriac na hati fulani za Septuagint Version ya Kigiriki zinazosema “mwaka wa kumi na mmoja” mahali pa “mwaka wa kumi na mbili.” Hii ingemaanisha kwamba yule mtoro kutoka Yerusalemu alifika wakati wa nusu ya mwisho ya Desemba (Tebeth 5) katika mwaka wa 607 B.C.E., au miezi sita nyuma ya Yerusalemu kutekwa nyara na Wababeli. (2 Fal. 25:2-4) Kama miezi ikihesabiwa tangu masika hata masika na mwaka tangu vuli hata vuli, Tebeth 5 ya “mwaka wa kumi na mbili” ingefika wakati wa nusu ya mwisho vile vile ya Desemba katika mwaka wa 607 B.C.E.

b Ububu wa Ezekieli ulikuwa wa mfano. Ezekieli alikuwa bubu kwa habari ya kutoa kwake kwa unabii juu ya Yerusalemu aliyehukumiwa. Ububu wenyewe ulianza wakati ambapo Ezekieli alijulishwa na roho ya Mungu kwamba mazingiwa ya Yerusalemu yalikuwa yameanza, na ukamalizika uharibifu wa mji ulipohakikishwa kuwa kweli na mtu aliyeushuhudia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki