Ushike Sana Uzima Ulio Kweli Kweli
“Waagize.. . . wafanye mema, wawe matajiri katika kazi nzuri, wawe wakarimu, tayari kushiriki, wakijiwekea wenyewe akiba kwa usalama msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate kuushika sana uzima ulio kweli kweli.”—1 Tim. 6:17-19, NW.
1-3. (a) Simulia yaliyotukia wakati makutano yenye hasira yalipodai kwamba “mtu huyu” Yesu auawe. (b) Inaelekea Yesu alikuwa akifikiria nini alipokuwa katika hali hizo? (c) Yote haya yanatokeza maulizo gani?
TAZAMA, mtu huyu!” Alisimama mbele ya makutano yenye kupiga makelele, na kati yao makuhani wakuu na wakuu wa Wayahudi waliopiga kelele wakisema, “Msulibishe! Msulibishe!” Uuaji ulikuwa katika mioyo yao yenyewe wakati walipopaza sauti wakisema, “Amestahili kufa.” Ni vyepesi kuona akilini makutano haya yenye uadui yakitafuta damu. Na walikuwa wakitaka damu ya nani? Si ya mwingine ila ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.—Yohana 19:4-7.
2 Bila shaka Yesu alikuwa akifikiria mambo mengi wakati alipokuwa akisimama nje ya jumba la Pilato. Alijua kwamba alikuwa ameshuka kutoka mbinguni ili ayafanye mapenzi ya Baba yake. Alifahamu kwamba mapenzi hayo yalitia kufa juu ya mti wa mateso, na hili ndilo jambo ambalo mara hiyo alikutana nalo. Lakini namna gani wakati ujao? Je! angefufuliwa? Alijua hili lilitegemea juu ya kama alikuwa amehukumiwa kuwa mwaminifu katika yote ambayo alikuwa amepewa kufanya; tena juu ya kama angeweza kuvumilia mkazo mkubwa wa saa hizi za mwisho mpaka kufa.
3 Lakini hapa tuko mwishoni mwa hadithi. Ilianzaje? Labda tutataka kujua, na Yesu wakati wa kufa aliwezaje kuushika sana uzima ulio kweli kweli?
4, 5. (a) Ilikuwaje Yesu akazaliwa katika Bethlehemu? (b) Ni tangazo gani la tukio hili lililofanywa, na lilitolewa kwa nani?
4 Ilikuwa katika mwaka wa 2 B.C.E. malaika Gabrieli alipomfikia Mariamu, aliyeposwa na Yusufu, wakati alipokuwa katika kijiji cha Nazareti akamwambia kwamba atazaa mwana wa kiume, na ya kwamba mtoto huyo kweli angekuwa Mwana wa Mungu. Kutoka hapo mwaka ule ule Mariamu na Yusufu walisafiri kwenye mji wa Bethlehemu, maili kama 60 kusini, ili wakaandikishwe kama ilivyoamriwa na Kaisari Augusto. Wakati wa amri hii ulipatana na mpango wa Mungu, kwa maana mara walipofika Mariamu akamzaa Yesu katika hori. Yote haya yalitukia kama yalivyokuwa yametangulia kusemwa katika unabii.—Luka 1:26-35; 2:1-7; Mik. 5:2.
5 Malaika wa Yehova alitangaza tukio hili la maana sana kwa wachungaji waliokuwa katika mashamba ya karibu usiku huo wenye kujulikana sana, akisema: “Mimi ninaweletea habari njema ya furaha kuu . . . leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.” Mara hiyo wakafanya haraka ‘wakalione hilo lililofanyika.’ Waliporudi kwenye makundi yao ya wanyama walimtukuza na wakamsifu Mungu “kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona.”—Luka 2:8-20.
MATUKIO YA UTOTO KATIKA MAISHA YA YESU
6. Jambo gani lilitukia wakati Yesu alipokuwa mwenye umri wa siku nane?
6 Kulingana na desturi ya Wayahudi, Yesu alitahiriwa siku ya nane naye alitolewa hekaluni katika Yerusalemu siku 40 tangu kuzaliwa kwake, ili Yusufu na Mariamu watoe dhabihu inayofaa kulingana na ‘sheria ya Yehova.’ Ilikuwa wakati wa ziara hii ya kwenda hekaluni kwamba wakakutana na mzee aitwaye Simeoni ambaye kwake ilikuwa imefunuliwa “kwa njia ya roho takatifu kwamba asingeona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Yehova.” Akikichukua kitoto mikononi mwake Simeoni alimbariki Yehova, akisema: “Macho yangu yameona njia yako ya kuokoa . . . na utukufu wa watu wako Israeli.” Tena, nabii mke mwenye umri wa miaka 84 aitwaye Ana “akaja karibu na akaanza kumshukuru Mungu na kusema juu ya mtoto kwa wale wote waliokuwa wakingojea ukombozi wa Yerusalemu.”—Luka 2:21-38, NW.
7, 8. Ni mifululizo gani ya matukio yaliyofanya jamaa ya Yesu kwenda kwanza Misri na kutoka hapo kurudi kwenye kijiji cha Nazareti?
7 Kwa kupendeza, wakati fulani kufuata matukio haya, wanajimu waliosemekana kuwa wamemfikia Yesu siku alipozaliwa (kulingana na mafundisho ya Kristendomu), sasa wakafika. Kwanza walikuwa wamekwenda Yerusalemu na huko wakaambiwa waende Bethlehemu, na huko “wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye.” Walipokwisha kuzifungua hazina zao na kumtolea mtoto zawadi zenye gharama wakarudi moja kwa moja kwenye nchi yao ya mashariki, walipokwisha kuonywa kwa kimungu katika ndoto wasirudi kwa Herode katika Yerusalemu. Ndipo malaika wa Yehova alipompasha Yusufu habari hivi: “Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.”—Mt. 2:1-15. walimtukuza na wakamsifu Mungu “kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona.”—Luka 2:8-20.
8 Hivyo kutoka mwanzo Mwana wa Mungu kama mtoto aliyezaliwa hivi karibuni alikuwa hatakiwi na mtu fulani, na mtu fulani huyo alikuwa Shetani Ibilisi, adui mkuu wa Yehova. Herode, kama mjumbe wa Shetani, alipoona kwamba alikuwa amedanganywa na wanajimu, alikasirika sana. Akaagiza kwamba watoto wote wa kiume waliomo katika Bethlehemu wenye umri wa miaka miwili na kwenda chini wauawe. Ibilisi na chombo chake cha kidunia walizidi mno katika kujitahidi kumwua Mwana wa Mungu. Ikawa Herode alipokwisha kufa ndipo Yusufu, Mariamu na Yesu wakarudi kutoka nchi ya Misri wakakaa Nazareti.—Mt. 2:19-23.
9, 10. (a) Jambo gani lilitukia wakati wa Sikukuu ya Kupitwa wakati Yesu alipokuwa mwenye umri wa miaka kumi na miwili? (b) Kufuata haya, tuna habari gani juu ya Yesu wakati wa miaka yake ya ujana?
9 Huko katika wilaya ya Galilaya mtoto Yesu alikua akiwa pamoja na baba yake mlezi na mama yake na ndugu na dada zake. Alifundishwa kazi ya useremala naye “akakua, akaongezeka nguvu.” Tunaposikia tena juu ya Yesu, habari ya kihistoria inatuambia kwamba alikuwa amesafiri pamoja na wazazi wake kwenda Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Kupitwa, wakati huo akiwa mwenye umri wa miaka kumi na miwili. Ikawa akajitenga na wazazi wake, na mwisho walipomwona zikiisha kupita siku tatu, kumbe! alikuwa katika hekalu “ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.” Hapana, kijana huyu Yesu hakuwa akipoteza wakati wake pamoja na genge la vijana watundu wakizurura mjini. “Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?” akawaambia wazazi wake wenye kushangaa.—Luka 2:39-50.
10 Yesu alirudi Nazareti akaendelea kuwatii wazazi wake, na kama habari isemavyo: “Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.” Wakati uliofuata katika maisha yake Yesu kwa hakika angehitaji hekima yote, nguvu za kimwili na baraka ya Mungu ambazo angeweza kujipatia katika utoto.—Luka 2:51, 52.
YESU ANAANZA HUDUMA YAKE YENYE NGUVU
11. Jambo gani la maana sana katika maisha ya Yesu lililotukia katika mwaka wa 29 C.E.?
11 Matukio ya mwaka wa 12 C.E. yalipokwisha kutukia hatuna habari juu ya Yesu mpaka mwishoni mwa mwaka wa 29 C.E., wakati, kwa umri wa miaka 30, anapomjia Yohana Mbatizaji, kwa wazi binamu yake, akimwomba abatizwe katika Mto Yordani. Mara hiyo akiisha kufanya ubatizo Yohana hakuona roho takatifu tu ikishuka katika umbo la njiwa juu ya Yesu bali vile -vile alisikia sauti kutoka mbinguni ikisema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Hivyo kutoka alipobatizwa, Yesu alipata msaada wa nguvu nyingi kutoka kwa Yehova.—Mt. 3:13-17.
12, 13. Shetani alijaribuje kumwangamiza Yesu mwanzoni mwa huduma yake, lakini mpango wa werevu ulishindwa namna gani?
12 Ili ajitayarishe kwa kazi yake kubwa Yesu aliongozwa na roho takatifu katika jangwa la Uyahudi, alikofunga kwa siku 40. Mwishoni mwa kipindi hiki, wakati Yesu alipokuwa katika hali ya udhaifu wa kimwili, Ibilisi, akiwa bado anataka kumharibu huyu Mwana wa Mungu, alimfikia kwa vishawishi vitatu, akitumaini kuvunja ukamilifu wake. Alishauri kwamba Yesu ageuze mawe yawe mkate ili atosheleze njaa yake. Hili halikuwa na matokeo. Ndipo alipojaribu kumshawishi Yesu aonyeshe kama alikuwa Mwana wa Mungu kwa kuruka kutoka kileleni cha hekalu. Hili vile vile halikuwa na matokeo. Kisha “mkuu wa ulimwengu huu,” Ibilisi, akatoa kwa Yesu falme zote za kibinadamu ikiwa angeanguka afanye tendo la kumwabudu Shetani. Tena hili halikuwa na matokeo. Mtu huyu Yesu, ambaye ni mkamilifu katika nguvu za kimwili na za moyoni, aliitikiaje matoleo haya? Je! aliyafikiria, akayakadiri katika akili zake, au alivutwa na kutamanika kwayo? Je! alimjibu Ibilisi kwa kuwaza kwa kibinadamu au kulingana na ufasaha wa waalimu wa Kiyahudi? Hapana, katika kila shawishi alitumia mara hiyo Neno la Mungu kwa jibu lake na katika kujitetea, akisema: “Imeandikwa . . .”—Mt. 4:1-11; Yohana 12:31.
13 Hivyo tangu mwanzo wa huduma yake maalum ya kidunia Yesu alitembea katika ukamilifu wake, akiwa mwaminifu kwa Baba yake wa kimbinguni, Yehova. Na aliendelea kufanya hivi mpaka alipopigiliwa misumari kwa aibu sana. Kwa hakika Yesu alionyesha kwamba alikuwa akifikia, mwisho, kuushika sana uzima ulio kweli kweli, uzima wa milele!
14. (a) Je! tunajua sura ya Yesu ilivyokuwa? (b) Basi, tutajuaje alikuwa mtu wa namna gani?
14 Je! wewe umetaka kujua kama Yesu alikuwa na sura gani, au huyu Mwana wa Mungu alikuwa mtu wa namna gani? Juu ya sura yake, Biblia haisemi kabisa. Haituambii lo lote juu ya namna rangi ya nywele au macho yake ilivyokuwa, wala haitoi urefu wake, ratli au alama nyingine zo zote katika mwili wake. Mambo kama hayo hayana maana sana. Walakini, jambo ambalo ni la maana kuliko yote ni namna ya mtu alivyokuwa, na juu ya hili tunajifunza sana kutokana na mambo ambayo alifanya, ambayo alisema, na namna alivyoyasema na yale ambayo wengine walisema juu yake.
15. Kulingana na historia, Yesu kama mfanya kazi analinganaje na wengine wa wakati wa zamani au wa sasa?
15 Ni uhakika uliokubaliwa usioweza kupingwa, Yesu Kristo alikuwa mtu mkubwa na mwenye cheo kuliko wote katika dunia hii. Historia yote ya kibinadamu iliyotangulia wakati wake ilivuta fikira juu ya kuja kwake na historia yote tangu wakati huo iko juu ya kufika kwake. Na jambo ambalo tena ni lenye kustaajabisha ni wakati mfupi sana ambao katika huo alitimiza mengi sana. Si kupiga chuku kusema kwamba kwa muda wa miaka mitatu na nusu Yesu alitimiza mengi mara mia kuliko ambavyo watu wengine wanavyotimiza katika muda wa maisha. Ikiwa unatilia shaka usemi huu, basi linganisha mambo ambayo kiumbe kingine cho chote kimetimiza na usemi ulioongozwa kwa roho ya Mungu wa mtume Yohana: “Kuna na mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.” Hakuna shaka kwamba Yesu alikuwa mfanya kazi mwenye bidii!—Yohana 21:25.
16. Je! washiriki wa Yesu walikuwa tayari kufanya kazi ya kuhubiri na kufanya wanafunzi akiisha kuuawa?
16 Upesi Yesu alipokwisha kubatizwa aliwachagua wanafunzi fulani ambao wakati uliofuata walisafiri pamoja naye na walishirikiana sana na yeye wakati wa huduma yake. (Yohana 1:35-51) Unakumbuka namna, mwishoni mwa huduma yake ya kidunia, Yesu aliyefufuka alivyowaambia washiriki hawa, ‘Nendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote.’ Katika kufanya hivyo yeye hakuwa akiwatuma katika kazi ambayo hawakuijua. Sivyo; ila, walikuwa wamemtazama sana kwa karibu miaka mitatu akifanya wanafunzi, na hivyo walizoezwa kwa kufaa na kutayarishwa kufanya kazi ambayo Yesu mwenyewe alikuwa ameanzisha.—Mt. 28:19, NW.
17. Ni matukio gani machache kati ya yale yaliyotukia wakati wa miezi ya kwanza sita ya huduma ya Yesu, na ni kwa kadiri gani alieneza eneo katika kipindi hiki?
17 Ilikuwa katika Kana ya Galilaya ambako Yesu alikofanya mwujiza wake wa kwanza kama ishara ya kutia nguvu imani ya wanafunzi wake katika Umasihi wake. Kutoka hapo alitembelea Kapernaumu na akahubiri huko kwa wakati fulani mbele ya kukwea kwenda Yerusalemu kwa Sikukuu ya Kupitwa katika mwaka wa 30 C.E. Hivyo katika miezi ya kwanza sita ya kuhubiri kwake na kufanya wanafunzi Yesu alikuwa amezunguka sana—kutoka bonde la chini la Yordani mahali ambapo Yohana alipokuwa akibatiza kwenda karibu na Bahari ya Galilaya katika kaskazini na vilima upande wake wa magharibi, halafu kutelemka kusini kwenda Yerusalemu.—Yohana 2:1-13.
“MTU” KATIKA TENDO
18. Ni sifa gani za maana sana zilizoonyeshwa na Yesu alipotembelea Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Kupitwa katika mwaka wa 30 C.E.?
18 Kama Pilato angalitazama eneo la hekalu wakati Yesu alipokuwa akitembea katika hilo wakati huo wa Sikukuu ya Kupitwa akiwa na mjeledi mkononi mwake, inaelekea angalipaza sauti hivi, “Tazama! Mtu huyu katika tendo!” Ah, ndiyo! mtu hodari sana, asiyeogopa mwenye kujaa ghadhabu ya haki kwa kuona nyumba ya ibada ya Baba yake inageuzwa kuwa nyumba ya biashara. Basi akaingia katika tendo, akafukuza kondoo na ng’ombe, akamwaga fedha na kuzipindua meza—yeye peke yake. Huyu hakuwa mwoga, kama vile mara nyingi picha za Kristendomu zinavyomwonyesha Yesu kuwa. Wanafunzi wake, wakimtazama mtu huyu hodari kwa kutenda, walisema kwamba unabii wa Zaburi 69:9, NW ulikuwa ukitimizwa huko mbele ya macho yao yenyewe: “Bidii ya nyumba yako imenila kabisa.”—Yohana 2:14-17, NW.
19, 20. (a) Ni nani aliyekuwa Nikodemo, na kulitukia mazungumzo gani kati yake na Yesu? (b) Ni jaribu gani ambalo Yesu alisema lingeonyesha kama mtu ni mbaya au mzuri?
19 Sifa nyingine yenye maana sana iliyoonyeshwa na Yesu ilikuwa uwezo wake wa kusema kweli kwa uhodari, pasipo woga alipokuwa mbele ya watawala. Hii ilionyeshwa wakati Farisayo Nikodemo alipokwenda kumwona wakati wa usiku. Nikodemo, “mkuu wa Wayahudi,” alimtaja Yesu sawasawa, akisema: “Twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu.” Katika kujibu, Yesu alisema: “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Wakati Farisayo huyu alipoonyesha uzito wake wa kufahamu, Yesu alimkemea, akisema: “Je! wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? . . . Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?” Hata hivyo, Yesu hakuonyesha upendeleo, maana aliendelea kumpa mtu huyu nafasi ile ile kama mtu mwingine ajue kweli, kweli ya kwamba wale wanaojizoeza imani peke yao katika Mwana mzaliwa wa pekee wa Mungu ndio watakaoushika sana uzima ulio kweli kweli. “Amwaminiye yeye [Mwana],” Yesu akamwambia, “hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.” Hivyo, iliachwa juu ya Nikodemo aamue mwenyewe kama angepokea hukumu kali ya kimungu au sivyo.—Yohana 3:1-12, 16-18.
20 Labda mshiriki huyu wa Baraza Kuu alichagua wakati wa giza ili amfikie Yesu kwa sababu aliwaogopa Wayahudi, na akaona huenda akaharibu sifa yake ikiwa angeonwa na wao akiwa mbele ya Yesu. Labda hii ndiyo iliyokuwa sababu Yesu alimalizia mazungumzo yake pamoja na Nikodemo kwa kusema: “Hapa pana jaribu: nuru imekuja katika ulimwengu, lakini wanadamu wakapendelea giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu. Watu wabaya wote wanachukia nuru na kuiepuka, wakiogopa mazoea yao yasije yakaonyeshwa wazi. Mtu mnyofu anakwenda kwenye nuru ili ipate kuonekana waziwazi kwamba Mungu yuko katika yote anayofanya.”—Yohana 3:19-21, New English Bible.
21. Ni ushuhuda gani ulioonyesha kwamba kazi ya Yohana Mbatizaji ilikuwa ikipungua?
21 Mambo haya yalipokwisha kutukia Yesu na wanafunzi wake wakaingia katika upande wa mashambani wa Uyahudi, ambako waamini wengi walikobatizwa, si na Yesu bali na wanafunzi wake. Kwa kweli, wengi sana walikuwa wakibatizwa hata wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wakamwuliza iliyokuwa maana ya hili. Katika kujibu, katika mambo mengine, Yohana alieleza hivi: “Yeye [Yesu] hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.”—Yohana 3:22–4:2.
22. Jambo gani lilitukia katika mji wa Sikari lililofungua njia kwa Wasamaria wengi, ili wakati ujao, waushike sana uzima ulio kweli kweli?
22 Upesi Yohana Mbatizaji alipokwisha kufungwa, Yesu aliondoka katika Uyahudi akaenda katika Galilaya. (Mt. 4:12) Njiani yeye na wenzi wake walipita katika eneo la Wasamaria, ambako Yesu alitoa kidogo “ushuhuda wa bahati” kwa mwanamke kisimani nje ya mji wa Sikari. Yeye alikuwa “amechoka kwa safari yake”; hata hivyo, yeye aliitumia nafasi ili ajijulishe mwenyewe, maana Wasamaria vile vile walikuwa wakimtazamia Masihi. Matokeo ya maongezi hayo pamoja na mwanamke Msamaria karibu na kisima yakawa kwamba watu wengine walitoka mjini kuja kumlaki Yesu. Nao, vile vile, walimwomba sana akae pamoja nao hata akakaa huko siku mbili, na “watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake.”—Yohana 4:3-43.
YESU AANZA HUDUMA KUU YA GALILAYA
23. Kurudi kwenye wilaya ya Galilaya, ni kichwa gani ambacho sasa Yesu alitia katika ujumbe wake, na kwa sababu gani?
23 Wakati fulani Sikukuu ya Kupitwa ya mwaka wa 30 C.E. ilipokwisha kufanywa, mhudumu huyu mwenye nguvu sana alirudi katika wilaya ya Galilaya na akatumia sehemu iliyo kubwa zaidi ya miaka miwili iliyofuata katika eneo hilo. Kwa sababu hii habari inasema hivi, “Yesu akarudi kwa nguvu za [roho], akaenda Galilaya,” inayoeleza vizuri sababu gani Wagalilaya walikuwa na pendeleo la kushuhudia sehemu ya kazi zake zenye nguvu zaidi. Ujumbe wake wenye kutiwa nguvu na roho kwa wakati wa kwanza ulitia kichwa kilichotumiwa na Yohana Mbatizaji, ambaye kwa sasa alinyamazishwa kwa kufungwa, yaani, “Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”—Luka 4:14, 15; Mt. 4:17; Marko 1:14, 15; Yohana 4:43.
24. (a) Ni tukio gani la ajabu sana lililotukia katika sinagogi la Nazareti? (b) Lakini watu wa mji waliitikiaje, na kwa sababu gani hivyo?
24 “Kwa nguvu za [roho]” Yesu akaingia katika sinagogi la mji wa nyumbani kwake wa Nazareti siku ya sabato na akawasomea kutoka katika kitabu cha Isaya, sura ya 61, mistari ya 1 na 2: “Roho [ya Yehova i] juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa [Yehova] uliokubaliwa.” Ndipo Yesu alipotangaza hivi: “Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” Basi, walistaajabia maneno yake yenye kupendeza, lakini alipokataa kufanya miujiza ili awafurahishe na, pahali pake, akawalinganisha wasikiaji wake na Waisraeli wasio na imani katika siku za manabii Eliya na Elisha, “wakajaa ghadhabu” na wakamtoa nje kwa haraka kwenye ukingo wa kilima kwa kutaka wamtupe chini. Walakini, huyu Yesu mwenye nguvu, mwenye kuongozwa na roho alipita tu katikati yao akaondoka akaenda Kapernaumu, maana huu haukuwa wakati wala haikuwa ndiyo namna ya kufa kwake.—Luka 4:16-31.
25, 26. (a) Je! Yesu aliacha kuhubiri katika eneo la Galilaya kwa sababu ya kutendewa vibaya katika mji wa kwake wa Nazareti? (b) Ni miujiza gani ambayo alifanya, na kwa matokeo gani?
25 Alipokuwa akitembea kando ya pwani ya Bahari ya Galilaya, Yesu aliwakaribisha wanafunzi wanne wafuatane naye katika huduma yake—Petro na ndugu yake Andrea, Yakobo na ndugu yake Yohana. Ndipo habari inapotuambia namna huyu mfanya wanafunzi mwenye bidii alivyokuwa “akizunguka katika Galilaya yote . . . kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna.” Upesi ripoti zilienea mahali pote katika Shamu yote na makutano ya watu wakaja wakiwa na namna zote za magonjwa—kati yao watu wenye ugonjwa wa kifafa, ugonjwa wa kupooza, wenye kupagawa na mashetani—naye akawaponya wote.—Mt. 4:18-24.
26 Alikuwako vile vile mwenye ugonjwa wa ukoma ambaye, katika kupiga magoti, alimsihi Yesu hivi: “Ukitaka, waweza kunitakasa.” Akivutwa na huruma, Yesu alimgusa akasema: “Nataka, takasika.” Ndipo yule mtu alipoambiwa asitangaze jambo hili, bali aende akajionyeshe mwenyewe kwa kuhani na toleo lililotakiwa na Torati. Lakini kwa sababu watu wanasema juu ya miujiza hiyo, upesi habari zilienea mpaka ilipokuwa haiwezekani kwa Yesu hata kuingia mjini waziwazi. Basi alitafuta amani na utulivu kidogo katika mahali pa upweke nje ya mji, hata hivyo makutano “wakamwendea kutoka kila mahali.”—Marko 1:40-45; Luka 5:12-16.
27. Jambo gani lilionyesha namna Yesu alivyokuwa mwenye kuvumilia mno wengine?
27 Unaweza kuwazia namna hii ilivyomaliza wakati na nguvu za Yesu. Hata mtu mkamilifu anahitaji wakati fulani aburudike na kupumzika, lakini inaonekana kwamba watu hao, kwa shauku yao ya kutaka kuponywa magonjwa yao (na ujue bila malipo), hawakutaka kumhurumia Yesu hata kidogo. Lakini jambo ambalo ni lenye kupendeza zaidi ni kwamba Yesu hakunung’unika hata kidogo au kuonyesha kuudhika kwa sababu ya ukosefu huu wa huruma, na hii ilionyesha nyingine ya sifa zake kubwa sana, yaani, kuwavumilia kwake mno watu.
28. (a) Jambo gani lilionekana wazi sana wakati Yesu alipomponya mtu mwenye kupooza katika Kapernaumu? (b) Je! wote waliokuwapo walifurahia kuona mwujiza ukifanywa?
28 Kufuata muda wa kutokuwapo katika Kapemaumu kwa siku fulani ikaripotiwa kwamba Yesu alikuwa amerudi na upesi watu wengi sana wakasongamana ndani na nje ya nyumba alimokuwa akikaa hata ikawa haiwezekani kuingia. Kwa hiyo, rafiki wanne wenye nguvu wa mtu aliyepooza walitoboa tundu katika dari wakamtelemsha pamoja na kitanda kidogo mpaka mahali Yesu alipokuwa. Sehemu hii ya tukio lenye kuchekesha sana ndiyo watu wengine wanayokumbuka tu. Walakini, kuliko kuwa jambo la kuwavuta watu macho, lilionyesha imani ambayo watu hao walikuwa nayo, naye ‘aliiona imani yao.’ Basi akasema: “Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.” Lakini si kila mtu aliyekuwapo alifurahia kusikia hivyo. Waandishi fulani walimlaumu Yesu katika mioyo yao. Kwa vile alikuwa na uwezo wa kufahamu yaliyokuwa katika mioyo yao, Yesu alijaribu kuzungumza nao hivi: “Vyepesi ni vipi,” akauliza, kusema, “Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende”? Halafu akaeleza sababu gani alitumia usemi wa kwanza—“mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi.” Sasa je! hiyo haikuwa njia ya upole ya kuwakemea waandishi hao? Kwa njia hiyo ushuhuda mkubwa ulitolewa na wale waliokuwapo walipaza sauti wakisema: “Namna hii hatujapata kuiona kamwe.”—Marko 2:1-12; Mt. 9:2-8.
29. Wapinzani walipopinga kula kwa Yesu pamoja na watoza kodi na wenye dhambi, aliwajibu namna gani kwa kufaa?
29 Mojawapo la mambo yanayomstaajabisha msomaji wa habari hizi za historia zilizoongozwa na roho ya Mungu ni namna mara nyingi Yesu alivyokuwa na jibu lililo sawasawa na lenye kufaa kuwapa wapinzani. Kwa mfano, alipokwisha kumchagua Lawi mtoza kodi awe mmoja wa wafuasi wake, mtu huyu alifanya karamu kubwa akamkaribisha Yesu na wanafunzi wake na vile vile watoza kodi na wenye dhambi wengi. Basi, Mafarisayo na waandishi wao walimlaumu Yesu kwa kula pamoja na watu hawa ambao, machoni pao, walidharauliwa kama wanadamu wenye dhambi na waovu, watu wanaostahili kuepukwa. Basi jibu kamilifu la Yesu lilikuwa nini ili kunyamazisha hawa wenye dhihaka ya Kifarisayo? Hili: “Wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”—Luka 5:27-32.
“MTU” ALIFANYA MEMA SIKU YA SABATO
30, 31. (a) Kulitukia nini wakati Yesu alipotembelea birika ya Bethzatha siku ya sabato? (b) Yesu alionyesha namna gani haki ya kufanya mema siku ya sabato?
30 Wakati wa mwaka wa 31 C.E. tena Yesu alisafiri kwenda Yerusalemu kwa Sikukuu ya Kupitwa. Karibu na mlango wa kondoo wa mji katika birika inayoitwa Bethzatha aliona mambo ya kusikitisha. Watu wengi wenye magonjwa, wengine vipofu, wengine viwete au wenye viungo vilivyopooza, walikuwa wakitaka waponywe. Akimchagua mtu aliyekuwa amekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka 38, Yesu alimwambia: “Simama, jitwike godoro lako, uende.” Mtu huyu alifanya hivyo, akiwa amepona kabisa!—Yohana 5:1-9.
31 Lakini pahali pa kumtukuza Mungu kwa sababu ya jambo lililokuwa limetukia, Wayahudi waliotazama hili walimlaumu Yesu kwa sababu alifanya kazi nzuri hii ya kuponya siku ya sabato. Yesu aliwajibuje? Alisema hivi: “Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.” Ah, ndiyo, katika kumwiga Mfanya kazi Mkuu kuliko wote, asiyeacha kutushughulikia sisi wakati wo wote, anayeangazia jua na kunyesha mvua hata siku ya sabato, vivyo hivyo huyu Bwana wa Kazi Yesu hakuacha hata kidogo kufanya kazi ya kilichokuwa chema kwa faida ya wengine hata siku ya sabato.—Yohana 5:10-17.
32, 33. Zaidi ya kupinga kuponya kwa mwujiza siku ya sabato, ni shtaka gani jingine ambalo wapinzani walimfanyia Yesu, lakini yeye alijibuje?
32 Je! makutano yalikubali maelezo ya Yesu? Hapana, bali walikasirika hata zaidi, “walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu”—bila shaka, ndivyo walivyoona. Ni vigumu kuwazia kwamba watu hao walipofushwa sana na mapokeo ya kidini kwamba, hata ijapokuwa ushuhuda huo usioweza kupingwa wa kwamba yeye alikuwa Masihi, walikataa kukubali kwamba alikuwa Mungu aliyemponya mtu huyu kupitia kwa Yesu. Hata hivyo, Yesu aliendelea kuzungumza nao, akiwaonyesha kwamba yeye hakuwa “akijifanya sawa na Mungu,” bali yeye alikuwa akimpa Yehova sifa yote kwa mambo ambayo alikuwa amefanya, akisema, “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda.” Maana, wangemwona akifanya mambo yaliyo makubwa hata zaidi, kwa kuwa wakati ulikuwa unakuja “wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu,” ndiyo, “saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka.”—Yohana 5:18-30.
33 Katika kuambia makutano hayo kweli hizi kubwa je! Yesu alifikiri angewasadikisha kwamba yeye alikuwa Masihi? Hapana. Yeye hakuwa mpumbavu hivyo. Kwa hiyo, alimalizia maongezi yake, akisema: “Kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?”—Yohana 5:46, 47.
34. Pindi nyingine, kwa sababu gani shtaka la kuvunja sabato lilifanywa juu ya wanafunzi wa Yesu?
34 Sikukuu ya Kupitwa ilipomalizika katika Yerusalemu, wakati wa kurudi kwenye wilaya ya Galilaya wanafunzi wa Yesu walivunja masuke machache ya ngano wakala wakati wa kupita shambani. Tena Mafarisayo waliwalaumu juu ya kuvunja sabato. Katika kujibu, Yesu alisema kwamba sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato, na zaidi ya hayo, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.”—Marko 2:23-28.
35. Tena siku nyingine ya sabato, Yesu tena alizungumza kwa kutoa sababu namna gani pamoja na wapinzani wake kwamba ilikuwa vema kufanya miujiza siku ya sabato, na kwa matokeo gani?
35 Wakati wa sabato nyingine, Yesu alikuwa katika sinagogi nao Mafarisayo walikuwa wakitazama kama ‘angevunja’ sabato kwa kuponya mkono wa mtu uliopooza. Ili wapate kumshtaki, waliuliza hivi: “Ni halali kuponya watu siku ya sabato?” Katika kujibu, Yesu aliwauliza hivi: “Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa?” Kisha akamwambia yule mtu anyoshe mkono wake uliopooza, na mara hiyo ukawa mzima kama mkono mwingine. Tena, je! viongozi hao wa kidini wa Kifarisayo walimsifu Mungu kwa onyesho hili la kimungu la Umasihi wa Yesu? Hapana; ila, walikasirika sana na “wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.” Hivyo tunaona tena kwamba huyu “Bwana wa sabato” hakuwaogopa wanadamu hao waovu. Yeye aliendelea kufanya mema na kufanya kazi siku saba kila juma katika kazi ambayo Yehova alikuwa amempa aifanye.—Mt. 12:9-14; Luka 6:5-11.
MWALIMU MKUU ALISONGA MBELE BILA KUKOMA
36. Kwa sababu gani kulikuwako haraka iliyo kubwa hata zaidi sasa kuliko wakati Yesu alipoanza huduma yake?
36 Miezi mitatu kufuata Sikukuu ya Kupitwa ya mwaka wa 31C.E. Yesu alifika katikati ya kazi yake ya kufanya wanafunzi. Alibakia na mwaka mwingine mmoja na miezi tisa tu ya kumaliza mgawo na kuushika sana uzima ulio kweli kweli. Kulikuwa hakuna wakati wa kupoteza. Kazi nyingi ilikuwa bado inatakiwa kufanywa.
37. Ni hotuba gani yenye kujulikana sana ambayo Yesu alitoa karibu na Kapernaumu, tukiisoma itakuwa na faida gani ya pekee kwetu?
37 Yapata wakati huu Yesu alitoa hotuba yake yenye kujulikana sana inayoitwa Mahubiri juu ya Mlima. Mahali ulipokuwa mlima huo hapajulikani kwa uhakika, lakini palikuwa karibu na Kapernaumu upande wa Bahari ya Galilaya. Jambo ambalo ni la maana ni yale ambayo Yesu alisema wakati huo. Utaona mahubiri haya yameandikwa katika Mathayo, sura ya tano, mstari wa tatu, mpaka sura ya saba, mstari wa 27. Katika hotuba hiyo bila shaka Yesu aliwapa wasikilizaji wake mengi ya kufikiria, kwa kweli, zaidi kuliko inavyowezekana kurudia kuyasema katika maneno machache. Litakuwa jambo la faida kwetu sote kukaa kitako na kusoma mahubiri hayo na kufikiria aliyosema. Huko Yesu alikuwa akisema mawazo ya Mungu chini ya uongozi wa roho kama Baba yake wa mbinguni alivyoagiza. Hivyo ikiwa tunataka kufikiri mawazo ya Mungu itafaa tutumie wakati tusome na kutafakari juu ya mambo yaliyosemwa huko.
38. Jambo gani lilifanya njia za kufundisha za Yesu kuwa zenye matokeo sana?
38 Wasikilizaji wa Yesu walionaje juu ya hotuba hiyo ya hadharani? “Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.” Kwa hakika yeye alionyesha kwamba alikuwa Mwalimu Mkuu, asiyelingana na mtu ye yote duniani. Kati ya mambo yaliyofanya njia za Yesu za kufundisha ziwe zenye matokeo sana yalikuwa ni kutumia mifano iliyo myepesi, mifupi, yenye kufahamika waziwazi, yenye kufikiri kwa akili na maulizo yenye kupenya yaliyofanya wasikilizaji wake waichunguze mioyo yao wenyewe kuamua, ama kuikubali kweli ama kuipinga.—Mt. 7:28, 29.
39. Zaidi ya mafundisho yake ya ajabu, jambo gani jingine ambalo Yesu aliendelea kufanya ili kuwasadikisha watu kwamba yeye alikuwa Masihi?
39 Kuongeza kwa kutumia kwake njia zenye matokeo za kufundisha, huyu Mwalimu Mkuu aliendelea kukazia sehemu ya mwisho ya huduma yake kwa kutumia miujiza wakati alipokuwa akizunguka huku na huku. Katika Kapernaumu alimponya mtumishi aliyepooza wa askari jeshi asiye Mwisraeli, kwa sababu, kama Yesu alivyosema: “Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.” Wakati jeneza lenye kuchukua maiti ya mwana mmoja peke yake wa mjane lilipopita karibu likielekea sehemu ya makaburi ya Naini, Yesu aliligusa na kwa amri yake yule kijana mwanamume alifufuliwa. Lo! namna kulivyokuwako ushuhuda wa Umasihi wa Yesu!—Mt. 8:5-13; Luka 7:11-17.
40. Yohana Mbatizaji aliyefungwa angejuaje kwamba kweli Yesu alikuwa ndiye Masihi?
40 Habari za mambo haya ya ajabu zikamfikia Yohana Mbatizaji mfungwa, na hivyo akatuma wajumbe kwenda kuuliza juu ya Yesu, “Wewe ndiwe yule ajaye . . . ?” Katika kujibu, Yesu aliwaambia wakaripoti mambo ambayo walikuwa wakiyaona kwa macho yao wenyewe—vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema. Kwa hakika hilo lingemsadikisha Yohana kwamba “yule ajaye” alikuwa amekuja kweli.—Luka 7:18-23.
41, 42. (a) Jambo gani lilitukia pindi moja wakati Yesu alipokuwa akila chakula pamoja na Farisayo? (b) Mwalimu Mkuu alionyeshaje kwa busara kwamba wenye kujitakia haki watapokea msamaha kidogo kwa dhambi zao?
41 Hata wakati Yesu alipochukua wakati ili apate kula sikuzote alikuwa macho na tayari kufundisha watu kweli. Chukua, kwa mfano, wakati alipokuwa akiegemea chakulani katika nyumba ya Farisayo na mwanamke mwenye dhambi mbaya sana akaja akilia, kwa kutumaini Yesu asamehe dhambi zake. Aliosha miguu ya Yesu kwa machozi yake, akaipangusa kwa nywele zake, akiibusu polepole na kuipaka kwa mafuta mazuri yenye gharama sana. Katika kuona hivi Farisayo alimwonea Yesu mashaka katika moyo wake, kwa kweli, alidharau tendo lote. Lakini angalia namna Mwalimu Mkuu, kwa mfano ufuatao, alivyomfundisha Farisayo huyu mwenye kujitakia haki somo ambalo asingelisahau upesi. Watu wawili walikuwa na deni kwa mkopeshaji fulani, mmoja alimkopa dinari 500, mwingine 50 tu. Kwa kuwa wadeni hawa hawakuweza kulipa deni yao, yule mkopeshaji alifuta deni zote mbili. Bila shaka, yule mdeni aliyekopa zaidi alikuwa na sababu ya kumpenda zaidi yule mkopeshaji. Sasa Yesu aliutumia mfano huu kwa hali iliyokuwa ikitukia pale pale, akisema:
42 “Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.”—Luka 7:36-50.
43. Jambo gani lilitukia wakati Yesu alipotembelea tena miji ya Galilaya kwa mara ya pili?
43 Mara matukio haya yalipokwisha Yesu alianza kutembelea miji na vijiji vyote katika Galilaya kwa mara ya pili, akiwachukua mitume wake kumi na wawili, pamoja na wanawake fulani ambao ni wanafunzi wenye kumwabudu Mungu. Katika utalii huu alifukuza mashetani zaidi, akapata upinzani zaidi kutoka kwa Mafarisayo, alisema mifano zaidi, alifungua macho zaidi ya vipofu, akafufua wafu zaidi, na akawafariji watu zaidi walioonewa kwa kuwahubiria habari njema za ufalme wake wenye utukufu.—Mt. 12:22-45; 13:1-52; Luka 8:1-3.
44. Lilikuwa itikio gani kwa kuhubiriwa kwa habari njema juu ya ufalme wa Mungu katika nchi ya Wagerasi?
44 Utalii wa kuzunguka ulimfikisha Yesu ng’ambo ya Bahari ya Galilaya kwenye nchi ya Wagerasi. Eneo hili jipya lingempokeaje Mwalimu Mkuu? Basi, wakati alipofukuza jeshi (“Legioni”) la mashetani katika wanaume wawili, nao mashetani wakafanya kundi la nguruwe kutelemka kwa mbio sana gengeni, wenyeji wa mji walimwomba Yesu aondoke katika wilaya yao. Je! Yesu alitaka kugombana na kukataa kuondoka? Hapana, hapakuwa na wakati wa kufanya hivyo. Yeye alikuwa ametoa ushuhuda. Bila shaka mmoja wa wale wanaume wenye mashetani alimwamini Yesu, naye alithawabishwa na agizo kutoka kwa Yesu kwenda na kueneza habari njema kati ya jamaa zake na kwenye miji iliyoungana pamoja inayojulikana kama Dekapoli. Basi kulikuwa hakuna haja kwa Yesu kukaa. Watu wenye kustahili zaidi walikuwa wakingojea kwa hamu sana avuke tena Galilaya ili wapate kupokea baraka ya, kuwapo kwake, kama Yairo mwenye binti aliyekuwa akifa na mwanamke mmoja asiyetajwa jina ambaye waganga hawakuweza kumponya ugonjwa wake wa kutoka damu kwa miaka kumi na miwili. Ndiyo, wakati ulikuwa mfupi mno kuupoteza kwa wapinzani wasiothamini.—Mt. 8:28-34; Marko 5:1-43.
45. Watu wa mji wa Nazareti waliitikiaje wakati Yesu tena aliporudi kufundisha katika sinagogi lao, ikimkumbusha nini?
45 Ikiwa Yesu alitembelea tena mji wa nyumbani kwake wa Nazareti, je! angekuta wamegeuza moyo? Je! wangekubali kosa lao la zamani na kwa furaha kumkaribisha mwenyeji wao mwenye cheo? Basi, aliporudi na kuanza kufundisha katika sinagogi lao, walistaajabia hekima yake, hata hivyo walijikwaza na wazo la kwamba yeye alikuwa “mwana wa seremala” tu. Katika kusema, “Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe,” labda Yesu alikuwa akimfikiria nabii Yeremia na namna watu wa mji wake walivyokuwa wamemkataa.—Mt. 13:54-58; Yer. 1:1; 11:21.
KUTIMIZA UHITAJI WA USHUHUDA ULIO MKUBWA ZAIDI
46, 47. (a) Ikiisha kupita miaka miwili ya ushuhuda wenye nguvu, je! twamwona Yesu akipunguza utendaji wa huduma yake? (b) Alionaje hali ya kiroho ya watu akiisha kulitembelea eneo kwa mara ya tatu, na alisema jambo gani limepaswa lifanywe juu yake?
46 Labda mmoja atakata shauri kwamba ikiisha kupita kama miaka miwili ya kuhubiri sana, akiisha kutembelea tena maeneo fulani, akiisha kufanya miujiza mingi mikubwa iliyoshuhudiwa na maelfu ya watu, sasa Yesu angefikiria kupunguza shughuli yake. Lakini kuliko kufanya hivyo, tunamwona akichukua hatua za kuongeza mwendo na kupanua kazi ya kuhubiri.
47 Kwanza, Yesu mwenyewe alianza utalii mwingine wa tatu, wa Galilaya, akitembelea “miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” Aliloona katika utalii huu wa mzunguko lilimsadikisha zaidi kuliko wakati wo wote juu ya uhitaji wa kuongeza na kupanua kazi ya kuhubiri. Po pote alipokwenda, akiwaona makutano “aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.” “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache,” akasema. Jambo gani lingeweza kufanywa juu yake? “Mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake,” lilikuwa ndilo shauri la Yesu.—Mt. 9:35-38.
48. Ni maagizo gani ambayo Yesu aliwapa wale kumi na wawili mbele ya kuwatuma katika kazi ya kuhubiri?
48 Kupatana na sala yake yenye bidii mtu huyu mwenye bidii na tendo alichukua hatua za kupeleka wahubiri zaidi wa habari njema katika shamba. Aliwaagiza mitume kumi na wawili akawapeleka wawili wawili, akifanya jamii sita za wahubiri wa Ufalme waende katika eneo katika pande mbalimbali sita. Katika kuwatuma wahudumu hawa wa wakati wote aliwapa maagizo juu ya mahali ambapo iliwapasa waende, na iliwapasa wamhubiri nani na iliwapasa wamwepuke nani. Tena waliambiwa jambo la kusema na wafanye sawasawa kama walivyokuwa wamemtazama Yesu akisema na kufanya. “Katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.” Kwa nguvu ya roho takatifu wangeweza ‘kuponya wagonjwa, kufufua wafu, kutakasa wenye ukoma, kutoa pepo.’ Haikuwapasa watoze fedha kwa kuponya huko kwa kimungu. “Mmepata bure, toeni bure,” ilikuwa ndiyo kanuni ambayo wangefuata.—Mt. 10:1-42; Marko 6:7-13.
49. Kwa sababu gani Yesu na mitume wake waliamua waende mahali pa upweke, lakini kukatukia nini?
49 Wakati kumi na wawili waliporudi ili wasimulie mambo mazuri ambayo waliona, Yesu alishauri waende mahali fulani pa upweke nje ya mji, kwa maana mahali walikokuwa “walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula.” Lakini watu wakapata habari juu ya mahali walikokuwa wakienda na hata wakatangulia kufika huko mbele ya Yesu na wanafunzi wake. Basi ilimpasa huyu Mwalimu Mkuu, mfano huu mkamilifu wa ukarimu usio wa choyo afanye nini? Alipowaona “akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.” Wakati ulikwisha. Ukawa ni wakati wa usiku. Wote waliona njaa. Basi mtu huyu wa Mungu mwenye kufanya miujiza aliwalisha wanaume 5,000 kwa mikate mitano na samaki wawili tu, na hata hivyo, kulikuwako vikapu kumi na viwili vya vipande vilivyosalia!—Marko 6:30-44.
50. Kwa muda mfupi Yesu alisemekana kuwa yu katika mahali gani palipotawanyika?
50 Tukio hili lilitukia karibu wakati wa Sikukuu ya Kupitwa katika mwaka wa 32, iliyomaanisha kwamba kulikuwa kumebakia kama mwaka mmoja tu ambao katika huo Yesu yampasa aimalize kazi yake na kuonekana mwenye kustahili uzima ulio kweli kweli ambao aliwekewa akiba kama thawabu kwa uaminifu wake. Basi, si ajabu kwamba sasa tunamkuta Yesu akihubiri katika mahali palipotawanyika na pote hapa kwa muda mfupi, kwa kuwa alijaribu kutoa ushuhuda mkubwa zaidi katika eneo kubwa zaidi kwa watu wengi zaidi. Kwanza, twamkuta yuko katika ujirani wa Kapernaumu katika pwani ya kaskazini ya Bahari ya Galilaya. Pili, amesemekana kuwa akifanya miujiza katika pwani ya Bahari ya Kati karibu na miji ya Tiro na Sidoni. Upesi kufuata hayo anaondoka huko, anakwenda Mashariki ya Bahari ya Galilaya na upande wa juu wa Yordani, akihubiri katika miji kumi inayoitwa Dekapoli na kufanya miujiza mingi katika eneo hilo.—Marko 7:24-37.
51. Ni taabu na masumbufu gani ambayo bila shaka Yesu alipatwa nayo, hata hivyo, kwa sababu gani mambo haya hayakutajwa?
51 Ebu fikiri juu yake, hakika Yesu alitembea sana ili afikie mahali hapa palipotawanyika. Na hata hivyo, yeye hakunung’unika hata juu ya kuchoka au juu ya taabu iliyofanyizwa na joto au mvua, mavumbi au matope, kama ambavyo huenda ikawa. Kwa kweli, mambo haya yalionwa kama yasiyo ya maana sana hata hayatajwi hata kidogo. Jambo kubwa, jambo la maana, kazi ya kuokoa uhai ya kuhubiri ambayo Yesu alifanya—hili ndilo jambo ambalo waandikaji wa Biblia walioongozwa na roho ya Mungu wanakazia katika masimulizi yao.
52. Nani waliokuwa wapinzani wakubwa kuliko wote wa Yesu, na jambo gani laonyesha wasingetubu na kumkubali Masihi?
52 Huko siyo kusema kwamba Biblia haisemi kabisa juu ya mambo ambayo Yesu alipatwa nayo katika huduma yake. Inatuambia mengi juu ya mateso na kupinga alikopata, hasa kutoka kwa viongozi wa kidini. Tangu mwanzo mpaka mwisho wa huduma yake ya kidunia ilimpasa apambane na upinzani wao wa sikuzote. Sasa ilikuwa zaidi ya miaka miwili, wakati ambao katika huo alikuwa amewaonyesha watu mifululizo ya ushuhuda wa kuonyesha kwamba kweli yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Na sasa, akiisha kulisha maelfu fulani ya watu (wanaume 4,000, kuondoa wanawake na watoto) kwa mikate saba na samaki wachache—tendo gumu lipaswalo kumsadikisha mtu mwenye mashaka asiyesadiki—tazama Mafarisayo na Masadukayo wanakuja wakitafuta ishara ya kutoka mbinguni kwamba Yesu alikuwa Masihi. Yesu alijibuje? Alirudia kusema yale ambayo alikuwa amewaambia wakati uliotangulia, yaani, “Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona.” Na kama matukio yaliyofuata yalivyoonyesha, wakati hiyo “ishara ya Yona” ilipotukia, wakati Yesu alipokuwa katika moyo wa nchi kwa siku tatu kama Yona alivyokuwa katika tumbo la samaki, hata hivyo hao watu ‘wabaya na wenye zinaa’ walikataa kusadiki!—Mt. 15:32—16:4; 12:38-40.
53. Karibu na mwisho wa huduma ya Yesu ya Galilaya ya miaka miwili, jambo gani la maana sana lilitukia, na wapi?
53 Mbele ya kumaliza huduma yake kubwa ya Galilaya iliyokuwa imechukua sehemu kubwa zaidi ya miaka miwili, Yesu akamchukua Petro, Yakobo na Yohana juu ya mlima mrefu. Huko, katika ule ambao labda ulikuwa Mlima Hermoni wenye futi 9,000 waliona tamasha ya kugeuka.—Mt. 17:1-13.
YESU AELEKEZA UANGALIFU WAKE KUSINI
54. Utendaji wa Yesu ulielekezwa wapi wakati wa miezi sita ya mwisho?
54 Ilikuwa mwishoni mwa mwaka wa 32, katika sikukuu ya vibanda, wakati Yesu alipoelekeza utendaji wake kusini, Yerusalemu na kando yake na katika wilaya za Uyahudi na Perea. Huko ndiko alikoelekeza kazi yake ya kuhubiri wakati wa miezi sita ya mwisho ya huduma yake ya kidunia. Walakini, kama mahali penginepo, Yesu alifundisha watu mafundisho yenye hekima na kanuni za haki, mara nyingi akitumia mifano inayofaa. Sehemu ya maneno yake ya maana sana na unabii ilitolewa wakati wa shughuli hii kusini.
55. Twamwona Yesu akihubiri wapi, usoni mwa upinzani, na ana nini la kuwaambia wenye kuamini na wasioamini?
55 Kwa kadiri mwisho ulivyokaribia zaidi, na adui walivyoendelea kuwa wabaya zaidi, ilimpasa Yesu awe mwerevu hata zaidi wasije wakamwua mbele ya wakati uliowekwa na Mungu. (Yohana 7:1-19, 25) Na hata hivyo, je! tunamwona mhubiri huyu mwenye bidii akificha vilimani, au akipunguza nguvu ya ujumbe wake ili usiumize maoni ya kidini ya viongozi wa dini? Hata kidogo. Yeye aliingia pasipo kuogopa katika hekalu na akaanza kufundisha watu, kama ilivyokuwa desturi yake. Kwa wale waliomwamini alisema hivi, “Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” Lakini kwa wapinzani alisema hivi, “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda.”—Yohana 8:31, 32, 44.
56. Jambo gani lilifanywa ili kuongeza mwendo wa kugawa watu katika wakati mfupi uliobaki wa huduma ya Yesu?
56 Yesu alijua kwamba humu katika eneo hili vile vile ‘mavuno yalikuwa ni mengi, lakini watenda kazi wachache.’ Basi ikiwa, katika wakati mchache aliokuwa nao, ushuhuda wenye matokeo ulipaswa utolewe katika eneo hili, kama alivyokuwa amefanya wakati wa miaka miwili kaskazini, basi kazi fulani ya kuanzisha ingepaswa kufanywa. Kwa hiyo yeye “aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.” Hii ilikuwa na maana ya kwamba, pahali pa wale kumi na wawili waliotumiwa katika Galilaya mwaka uliotangulia, sasa walikuwako mashahidi 70 wakipaza sauti katika nchi wakisema, “Ufalme wa Mungu umewakaribia.” Kwa hakika hii ingewatayarisha watu ili waweze kuamua upesi kama wangekubali au wangempinga Masihi wakati angetembelea mji wao.—Luka 10:1-16.
57. Wakati wahubiri wa injili 70 waliporudi, wakifurahi kwa sababu mashetani walitii sauti yao, Yesu alisema nini, akimaanisha nini?
57 Wakati wale 70 waliporudi walitoa ripoti kwa furaha kwa Yesu wakisema, “Hata pepo wanatutii kwa jina lako.” Walakini, waliambiwa hivi, “Msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Kwa hakika, uwezo juu ya mashetani ulionyesha uwezo wa Yehova uliokuwa juu yao tu, lakini kuandikishwa kwa jina la mtu mbinguni kulitegemea uaminifu wake. Hivyo imempasa mtu ajitahidi kuwa mwaminifu, kwamba anafukuza mashetani ama anafanya jambo fulani lisilo la tamasha sana.—Luka 10:17-24.
58. Ni baadhi ya kweli gani za maana sana ambazo Mwalimu Mkuu alifundisha wakati wa huduma yake kusini?
58 Ebu flkiria kweli fulani kuu ambazo Mwalimu huyu asiyechoka wakati wo wote alizowafundisha watu wakati alipokuwa akifanya huduma yake kutoka kwa hali hizi kwenda kwa hali nyingine. Kila siku alionekana kuwa anatokeza kweli mpya kutoka katika ghala ya hekima na maarifa ya Baba yake. Hadithi yake juu ya Msamaria jirani lilikuwa somo la upendo wa jirani na rehema. Martha alikemewa kwa sababu alikuwa mwenye kusumbuka mno juu ya mambo ya kimwili; Mariamu alisifiwa juu ya maoni yake. Mashetani walifukuzwa kwa “kidole cha Mungu,” si kwa “mkuu wa pepo.” (Luka 10:24-42; 11:14-22) Usisumbukie utakachokula au kuvaa, bali, zaidi, utafute ufalme wa Mungu sikuzote na mahitaji yote yatatolewa. “Kundi dogo” lisiogope, kwa sababu Baba yao atawapa sehemu katika Ufalme. “Wakili mwaminifu” ni yeye ambaye Bwana anamweka juu ya mali zake zote.—Luka 12:22-32, 41-44.
59. Yesu aliwajibuje wapinzani wakati alipolaumiwa tena kwa kuwaponya wagonjwa siku ya sabato?
59 Alipolaumiwa kwa sababu ya kumponya mwanamke aliyekuwa amekunjika kwa muda wa miaka kumi na minane katika siku ya sabato, Yesu alisema: “Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! hamfungui ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?” Tena, siku ya sabato alimponya mtu aliyekuwa ana ugonjwa wa safura, akisema: “Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato?”—Luka 13:10-17; 14:1-6.
60. Simulia baadhi ya mifano yenye kupendeza iliyotumiwa na Mwalimu Mkuu.
60 Na, lo! inapendeza na kufaa kama nini mifano ambayo Mwalimu Mkuu huyu alitumia! Mara nyingi alisimulia mfano unaofaa ili kufumba vinywa vya wenye kulaumu katika wasikilizaji wake. Ebu kwa kifupi angalia mifano michache kati ya hii. Alikuwako tajiri, lakini si tajiri kwa Mungu, aliyekusudia kubomoa ghala zake ili ajenge zilizo kubwa zaidi, ila akafa wakati wa usiku. (Luka 12:13-21) Ufalme wa Mungu unafanana na punje ndogo sana ya haradali inayokua mpaka kuwa mti mkubwa, au, tena, unafanana na chachu kidogo katika unga. (Luka 13:18-21) Imewapasa wageni wanaoalikwa kwenye karamu wakalie viti vya chini ikiwa nyuma wanatumaini kukuzwa. Mjenzi wa mnara anahesabu gharama kwanza; mfalme asiyeweza kushinda vita anafanya mapatano ya amani upesi. Mchungaji anafurahia zaidi kumwona kondoo mmoja aliyepotea kuliko kondoo wake 99 walio salama; mwanamke anafurahia zaidi kuona shilingi moja iliyopotea kuliko zile tisa zisizopotea. (Luka 14:7-11, 28-33; 15:4-10) Halafu tena kuna ule mfano wenye kujulikana sana wa mwana mpotevu, na vile vile ule juu ya tajiri na Lazaro. (Luka 15:11-32; 16:19-31) Mjane mwenye kuendelea kuomba mpaka hakimu mbaya sana akakubali ombi lake kwa sababu aliendelea kumsumbua tu akitaka haki. Watu wawili walikuwa wakiomba katika hekalu; sala za mtoza kodi mwenye dhambi zilijibiwa, lakini si zile za Farisayo mwenye kujitakia haki. (Luka 18:1-14) Hii ni michache kati ya mifano iliyotumiwa na Mwalimu Mkuu.
SIKU TUKUFU ZA MWISHO ZA HUDUMA YA YESU
61. Mbele ya kumaliza huduma yake ya kidunia, Yesu alisema inampasa apatwe na nini?
61 Yesu alijua juu ya mateso na mauti ambayo angepata upesi. Hivyo kwa mara ya tatu aliwaonya mitume wake juu ya matukio haya yaliyokuwa yakija, akisema: “Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.” Yesu hakuogopa kupatwa na mambo haya, ili apate kuonekana mwaminifu mpaka mauti na kuushika sana uzima wa milele mbinguni juu.—Luka 18:31-33.
62, 63. (a) Kwa sababu gani kulikuwako shaka fulani juu ya kama Yesu angekuwapo kwenye Sikukuu ya Kupitwa katika Yerusalemu katika mwaka wa 33? (b) Lakini shaka hilo liliondolewaje Jumapili, siku tano mbele ya Nisani 14?
62 Wakati matayarisho yalipokuwa yakifanywa kwa Sikukuu ya Kupitwa mazungumzo katika Yerusalemu yote yalikuwa juu ya kama Yesu angetokea au sivyo. Hii ilikuwa kwa sababu “wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua [Yesu] alipo, alete habari, ili wapate kumkamata.”—Yohana 11:55-57.
63 Ilikuwa katika hali yenye kuchacha-chacha kama hii kwamba Yesu akatokea, na lo! namna alivyotokea! Alikuja hali amepanda kuingia mjini katika kuandamana kwa ushindi, akiwa na watu wakitandika mavazi yao na matawi ya mitende mbele yake, wakipaza sauti wakisema: “Mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la [Yehova].” Matokeo yakawa kwamba “mji wote ukataharuki,” na kwa habari ya Mafarisayo, walisemezana hivi, “Mwaona kwamba hamfai neno lo lote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.” Basi, lilipokuja giza Jumapili hiyo, Yesu aliondoka akalala nje ya mji kwa ajili ya usalama. Zilikuwako bado siku tano zaidi alizobaki nazo kufanya kazi kubwa katika hizo.—Luka 19:36-38; Mt. 21:1-11; Yohana 12:12-19.
64. Yesu alifanya nini Jumatatu ya juma hii ya kumalizia, na kwa sababu gani?
64 Siku iliyofuata, Jumatatu, Yesu alitakasa hekalu kwa kuwafukuza wafanya biashara na kuzipindua meza za wabadili fedha. Huyu hakuwa mchochezi wa machafuko ya utawala au mapinduzi. Huyu alikuwa Mwana mwenye haki wa Mungu na alitumia Andiko ili kuthibitisha tendo lake, akisema: “Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.” Itakumbukwa kwamba miaka mitatu iliyotangulia, Yesu alikuwa ameonyesha bidii yake nyingi kwa ibada safi ya Yehova kwa utakaso kama huo wa hekalu kwa kuwaondoa wafanya biashara wen ye pupa. Basi kutakasa huku kwa pili kuliitikiwaje? “Wakuu wa makuhani, na waandishi, na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza.” Ndivyo walivyoonekana kuwa watu wabaya sana na wasiotaka kuacha mabaya.—Mt. 21:12, 13; Luka 19:45-48.
65, 66. (a) Yalikuwa mambo gani mengine ambayo Yesu aliwaambia makutano ya hekaluni Jumanne? (b) Halafu, masikioni mwa mitume wake, ni habari gani zaidi kwa namna ya unabii na mifano ambayo Yesu alifunua?
65 Jumanne ilikuwa siku nyingine yenye shughuli sana kwa Yesu huyu asiyechoka. Tunamkuta yumo katika hekalu akifundisha watu hata ijapokuwa mamlaka yake ilitiliwa mashaka na makuhani wakuu na wanaume wazee. Aliwalenga hawa viongozi wa kidini wasioaminika alipokuwa akisema mifano yake ya wana wawili, wakulima wabaya sana na karamu ya arusi. (Mt. 21:23–22:14) Wakati alipoulizwa maulizo ya werevu juu ya kulipa kodi, juu ya ufufuo na juu ya amri iliyo kubwa kuliko zote katika Torati ni nini, Yesu alijionyesha kuwa mwenye uwezo wa kuyajibu yote kwa kutumia sababu zisizoweza kupingwa. Halafu yeye alitunga ulizo lake mwenyewe juu ya ukoo wa Masihi, ulizo lililowanyamazisha kabisa: “Hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.” (Mt. 22:15-46) Wakati wa pindi hii Yesu tena aliwalaumu vikali sana waandishi na Mafarisayo wanafiki.—Mt. 23:1-39.
66 Wakati Yesu alipoondoka katika eneo la hekalu alisema hivi kwa unabii: “Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.” Ndipo yeye na mitume wake walitoka wakaenda kwenye Mlima wa Mizeituni, alikotoa kwao unabii wake wenye kuonyesha mambo yatakayotukia wakati ujao juu ya mwisho wa hii taratibu ya mambo, na vile vile mifano ya mabikira kumi, talanta na ule mfano unaosimulia juu ya kutengwa kwa kondoo na mbuzi.—Mt. 24:1–25:46.
67. Jumatano inakumbukwa kwa sababu ya matukio gani maovu?
67 Jumatano, wakati Yesu alipobaki katika Bethania, adui katika Yerusalemu walifanya shauri lenye kuongozwa na Ibilisi ili wamkamate Yesu kwa siri. “Wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa; wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua.” Mwenye kutokea, chombo kinachofaa wakati na kilicho tayari kwa mabaya, alikuwa Yuda Iskariote, aliyeuliza hivi: “Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu?” Mapatano yalifanywa kumpa vipande 30 vya fedha.—Mt. 26:3-16.
68. Alhamisi, jioni, ilikuwa siku ya tukio gani?
68 Alhamisi ilijaa shughuli za matayarisho ya Sikukuu ya Kupitwa ya kila mwaka. Jioni hiyo, Yesu na mitume wake kumi na wawili walikusanyika katika chumba kikubwa cha juu katika Yerusalemu ili waadhimishe Sikukuu ya Kupitwa ya halali ya mwisho chini ya mpango wa agano la Torati. Lo! huu ulikuwa wakati wenye maana sana! Mbele ya kuchwa tena Yesu angeutoa uhai wake wa kidunia ili aushike sana uzima ulio kweli kweli, uzima wa milele na hali ya kutoweza kufa!—Marko 14:12-16.
69. Akiisha kuadhimisha Sikukuu ya Kupitwa ya mwisho, ni mifululizo gani ya matukio iliyofuatana wakati wa saa zilizobakia za maisha ya Yesu?
69 Humo katika faragha ya chumba cha juu cha wageni, ndimo walimokuwamo Yesu na mitume wake kumi na wawili tu. Ungekuwa usiku mrefu na usio wa kulala usingizi kwa huyu Mwana mwaminifu wa Mungu. Katika saa chache zilizofuata matukio fulani yenye maana sana yalipaswa yatukie kwa haraka kwa kufuatana. Kumi na watatu wanakula Sikukuu ya Kupitwa. Yesu anasafisha miguu ya mitume wake. Yuda anajulishwa kama ndiye msaliti; anaondoka upesi. Ndipo chakula cha jioni cha Ukumbusho kinaanzishwa na kumi na mmoja wanakaribishwa washiriki pamoja na Yesu katika agano la ufalme. Yesu anasali. Kisha kumi na mmoja na Yesu wanaondoka kwenda kwenye Bustani ya Gethsemane. Huko Yesu anasali kwa bidii mbele ya kusalitiwa na kukamatwa. Hukumu yake inakuwa yenye mfululizo wa mambo yenye kuchekesha wakati Yesu anapopelekwa kutoka kwa Anasi kwenda kwa Kayafa, na kutoka kwa Kayafa kwenda kwenye Baraza Kuu, kutoka huko kwa Pilato, kutoka kwa Pilato kwa Herode halafu kurudi tena kwa Pilato.—Mt. 26:20–27:2; Luka 23:1-16.
70. Simulia yaliyotukia wakati kuwa mfalme kulipogeuka kuwa ulizo lenye mabishano kule nje ya jumba la gavana.
70 Ebu wazia mambo hayo yanayotukia—makutano yenye ghasia kushindana na mtu mkamilifu, asiyeogopa ambaye amesimama kwa utulivu katikati yao wote. Pilato anauliza juu ya Yesu, “Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Yesu anajibu, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu.” Bila kupata kosa ndani yake, tena Pilato anamtoa mbele ya makutano yenye ghasia, akisema, “Tazama, mtu huyu!” Makutano yenye ghasia yanapiga makelele wakisema, “Msulibishe! Msulibishe!” Pilato anauliza, “Je! nimsulibishe mfalme wenu!” Makuhani wakuu wanajibu, “Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.”—Yohana 18:28–19:16.
71. Simulia kuuawa kwa Mwana wa Mungu asiye na hatia mikononi mwa askari za Kirumi.
71 Akiisha kupigwa mijeledi, kuteswa kwa miiba, kupigwa makofi usoni na kutemewa mate, Mwenye Haki huyu alipigiliwa misumari kwenye mti wa mateso ili apate kifo chenye maumivu mengi cha polepole. Kwa kumaliza, yapata saa 9 za alasiri Ijumaa, Nisani 14 katika mwaka wa 33 C.E., akalia kwa sauti kuu, akisema: “Imekwisha.”—Marko 15:16-20; Yohana 19:1-3, 30.
72, 73. Kwa kurudia mambo makuu, ni baadhi ya mambo gani ambayo Yesu alitimiza katika huduma yake ya muda mfupi hapa duniani?
72 Ndiyo, yote ambayo Yehova alikuwa amekusudia katika kumtuma Mwana wake mzaliwa wa pekee kwenye dunia yalikuwa yametimizwa kabisa. Yesu alikuwa amejifunza utii kwa mambo yaliyompata; akawa amemshuhudia Ibilisi kuwa mwongo na kujistahilisha mwenyewe kuwa Mshuhudiaji wa Yehova katika ulizo la maana sana la enzi yote ya ulimwengu wote. Yeye alikuwa amekuja ili ‘aishuhudie kweli,’ na kwa hakika akafanya jambo hili. Yeye alitangaza habari njema kwa maskini, akawafariji wanaoomboleza na akaitangaza siku ya kisasi cha Yehova kwa wenye cheo na watu wa kawaida vile vile. Yesu alifanya yaliyokuwa mema, alikuwa tajiri katika kazi nzuri, alikuwa mwenye ukarimu sana kwa kutumia wakati na nguvu zake kwa ajili ya wengine, alikuwa tayari kushiriki ujuzi wake na hekima kuu pamoja na wengine, na mwisho akaushika sana uzima ulio kweli kweli, uzima wa milele katika mbingu pamoja na Baba yake.—Yohana 18:37; 1 Tim. 6:12, 18, 19; Ebr. 5:8.
73 Tena katika yote haya Yesu alituachia sisi mfano tupate kuzifuata nyayo zake.
[Ramani katika ukurasa wa 302]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Yesu alipanua huduma yake, akitalii Galilaya mara ya tatu, akitembelea “miji yote na vijiji” ili auhubiri ufaIme wa Mungu
GALILEE
Chorazin
Capernaum
Bethsaida
Magadan
SEA OF GALILEE
Cana
Tiberias
Plain of Esdraelon
Nazareth
Mt. Tabor
Gadara
Nain
Jordan River
Bethany across the Jordan
[Ramani katika ukurasa wa 303]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Yesu alifikia eneo kutoka Foinike mpaka Dekapoli kwa muda mfupi karibu lote kwa miguu
MEDITERRANEAN SEA
PHOENICIA
Sidon
Tyre
ABILENE
MOUNT HERMON
ITURAEA
Caesarea Philippi
TRACHONITIS
GALILEE
Chorazin
Capernaum
Bethsaida
Cana
Magadan
Sea of Galilee
Tiberias
Nazareth
Nain
Bethany across the Jordan(?)
SAMARIA
Salim(?)
Aenon(?)
Samaria
MOUNT GERIZIM
Jacob’s Fountain
DECAPOLIS
Damascus
Raphana(?)
Hippos
Dion
Canatha
Gadara
Abila(?)
Scythopolis
Pella
Gerasa
SCALE OF MILES 0——10——20
Picture katika ukurasa wa 293]
Kwa umri wa miaka kumi na miwili Yesu alikuwa katika hekalu la Yehova, akisikiliza na kuuliza maulizo
Kufuata ubatizo wake katika mwaka wa 29 C.E., Yesu alianza huduma yake yenye nguvu sana
[Picha katika ukurasa wa 295]
Kwa bidii Yesu alitakasa hekalu la Yehova kwa kuwafukuza wale waliolifanya kuwa nyumba ya biashara
[Picha katika ukurasa wa 297]
Yesu aliwakaribisha wavuvi wa samaki Yakobo na Yohana wamfuate katika huduma yake
[Picha katika ukurasa wa 299]
Siku ya sabato Yesu aliponya mkono wa mtu uliopooza
[Picha katika ukurasa wa 300]
Katika Mahubiri yake juu ya Mlima, Yesu aliwapa wasikilizaji wake msingi ya kufikiria
[Picha katika ukurasa wa 301]
Katika wakati wa kula, kama hapa nyumbani pa Farisayo, Yesu alikuwa tayari kufundisha kweli
[Picha katika ukurasa wa 305]
Katika miezi ya kumalizia ya huduma yake Yesu alipanua utendaji wake, akituma mashahidi 70 wakatayarishe nija mbele yake
[Picha katika ukurasa wa 305]
Upesi mbele ya kufa kwake, Yesu alipanda kuingia katika Yerusalemu kwa maandamano ya ushindi; mji wote ulitiwa msukosuko
[Picha katika ukurasa wa 306]
Pilato hakuweza kuona kosa kwa Yesu, lakini makutano yenye ghasia walipiga makele, “Msulibishe!”