Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 5/15 kur. 227-237
  • Kumfuata Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kumfuata Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “KUONGOKA KWAO MATAIFA”
  • KUUNGAMA KWA KINYWA
  • ‘KUKIRI HATA KUPATA WOKOVU’
  • KUJIKANA MWENYEWE
  • Kubatiza Kunafuata Kufundisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Kumtokeza Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Kufaidika Kutokana na “Mpatanishi Mmoja kati ya Mungu na Wanadamu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Kujiweka Wakf—Kwa Nani? kwa Sababu Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 5/15 kur. 227-237

Kumfuata Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu

1. (a) Kwa sababu gani uamuzi uliofanywa na babu zao katika Mlima Sinai sasa haukuwa kitu kwa Wayahudi wa asili waliotahiriwa kwa habari ya agano jipya? (b) Iliwapasa Wayahudi hao wafuate mfano wa nani, na katika njia gani?

KWA WAYAHUDI wa asili waliotahiriwa mambo hayakuwa namna ile ile Yesu Kristo alipokwisha kupaa kwenda mbele za Yehova Mungu mbinguni na kutoa kwake wema ulio bora sana wa dhabihu yake ya kibinadamu. Kwa sababu hii agano hili la kale la Musa lilifutwa, na agano jipya lilifanywa imara kwa damu ya Mwana wa Mungu, Mpatanishi wa agano hili. Nafasi ya kuingizwa katika agano hili jipya ilitolewa kwanza kwa Wayahudi wa asili. Babu zao wa karne kumi na tano zilizotangulia walikuwa wametangaza kwa mpatanishi Musa hivi: “Hayo yote aliyoyasema [Yehova] tutayatenda.” Lakini hii haikuwa kitu kwa wazao wao kwa habari ya agano jipya. Kwa agano hili la pili kulikuwako Mpatanishi mpya aliye mkubwa zaidi kuliko Musa, yaani, Yesu Kristo. Ili waingizwe katika agano jipya iliwapasa wamjibu Mpatanishi huyu aliye bora na mkubwa zaidi: “Hayo yote aliyoyanena [Yehova] tutayatenda, nasi tutatii.” Kwa kumfuata Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu, Yesu Kristo Mpatanishi, Wayahudi hawa wa asili walipaswa wajitoe wenyewe kwa Yehova, wafanye mapenzi yake kama yalivyopelekwa kwao kupitia kwa Mpatanishi huyu mpya na aliye mkubwa zaidi.

2. Kulingana na ambayo Petro aliwaambia Wayahudi siku ya Pentekoste ya mwaka wa 33 C.E., Mungu alikuwa amemfanyia Yesu nini kilichogeuza hali kwa Wayahudi hao wa asili?

2 Kwa kweli hali mpya ilikuwa imetokea kwa Wayahudi wa asili na iliwapasa kila mtu ajipatanishe na hali hiyo. Mtume wa Kikristo Petro aliwaeleza jambo hili wakati wa sikukuu ya Pentekoste ya mwaka wa 33 C.E., wakati Yehova Mungu kupitia kwa Yesu Kristo alipokwisha kuimimina roho takatifu juu ya wafuasi wa Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu. Alipokwisha kueleza yaliyokuwa yametukia kwa mwujiza na sababu gani, Petro aliwaambia maelfu hayo ya Wayahudi waliokusanyika: “Kwa hakika Daudi hakupaa mbinguni, bali yeye mwenyewe anasema, ‘Yehova alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka niweke adui zako kama kiti cha miguu yako.” ‘ Kwa hiyo acheni nyumba yote ya Israeli ijue kwa hakika kwamba Mungu alimfanya yeye kuwa Bwana na pia Kristo, huyu Yesu ambaye ninyi mlipigilia misumari.”​—Matendo 2:34-36, NW.

3. (a) Kama ilivyoonyeshwa na babu zao katika Mlima Sinai, Wayahudi hao wangejionyeshaje kustahili kuingizwa katika agano jipya? (b) Wakiisha kufanya ambayo Petro na mitume wengine waliwaambia kufanya, jambo gani lingeonyesha kwamba Wayahudi hao walikuwa wameingizwa katika agano jipya?

3 Sasa, chini ya hali mpya Wayahudi hao wenye kusikiliza walitangaza namna gani, “Hayo yote aliyoyasema [Yehova] tutayatenda,” na kujionyesha wenyewe kustahili kuingizwa katika agano jipya? Ilikuwa kwa kumkubali Yesu aliyepigiliwa misumari kama Bwana wao na kama Kristo au Masihi wa Yehova na kama Mpatanishi wao aliyetabiriwa na kufananishwa na nabii Musa. Wokovu haungeweza kuja kwao kupitia kwa njia nyingine. Maelfu ya Wayahudi hao walichomwa moyo na yale ambayo walisikia Petro akisema: Hivyo, wakati walipomwuliza Petro na wanaobaki wa mitume, “Wanaume, ndugu, tutafanya nini?” Petro aliwaelekeza kwa Wakili Mkuu wa uzima wa Mungu kwa kusema: “Tubuni, na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo kwa msamaha wa dhambi zenu, nanyi mtapokea zawadi ya bure ya roho takatifu. Kwa maana ahadi ni kwenu ninyi na kwa watoto wenu na kwa wale wote walio mbali, kwa kadiri ya ambavyo Yehova Mungu wetu ataita waje kwake. . . . Jiokoeni na kizazi hiki kipotovu.” (Matendo 2:37-40, NW) Ikiwa walipokwisha kuzamishwa katika maji ndipo walipopokea zawadi ya bure ya roho takatifu ya Mungu kupitia kwa Kristo hii ilimaanisha kwamba waliingizwa katika agano jipya.

4. Basi, ubatizo wa maji wa Wayahudi hao ulikuwa mfano wa nini?

4 Vema, basi, kubatizwa kwao katika maji kulifananisha nini? Kwa vile ubatizo wao ulipaswa uwe “katika jina la Yesu Kristo” na kwa kuwa ulitanguliwa na toba lao kwa Yehova Mungu, ulifananisha kujitoa kwao wenyewe kwa Mungu wafanye mapenzi yake. Kufanya mapenzi yake kulitia kumkubali kwao Yesu Kristo kama “Bwana” wao aliyepewa na Mungu na kama “Kristo” au Masihi wao aliyepewa na Mungu.

5, 6. (a) Kupokea kwao msamaha wa dhambi kungetoka kupitia kwa nani, na zilikuwa dhambi gani zao zilizohitajiwa sasa kusamehewa? (b) Kulingana na Waebrania 9:14, kusamehewa kwa dhambi zao kungetokeza nini kwao?

5 Bila kumkubali Yesu Kristo kama “Bwana na pia Kristo” wasingeweza kupata “msamaha wa dhambi” zao. Dhambi hizi ambazo sasa Mungu alisamehe kupitia kwa Yesu Kristo hazikuwa dhambi ambazo walifanya juu ya agano la Torati la Musa. Agano hilo pamoja na Israeli wa asili lilikuwa sasa limepita, limefutwa, na agano jipya lililoahidiwa lilikuwa sasa limepatanishwa na Mpatanishi aliye bora, Yesu Kristo. Basi dhambi ambazo ilikuwa lazima kwao watubu juu yake kwa Mungu kwanza zilikuwa dhambi zao juu ya Mungu kwa kushiriki katika kumpigilia misumari Mwana wake Yesu Kristo pamoja na dhambi zao wote. Kupokea kwao msamaha wa dhambi kutoka kwa Mungu kupitia kwa Kristo kungetokeza kupata kwao dhamiri njema. Kwa habari hii tunasoma:

6 “Basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa [roho ya milele] alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?”​—Ebr. 9:14.

7. Kulingana na masharti ya agano jipya, jambo gani liliahidiwa kwa habari ya dhambi, na Wayahudi hao waliobatizwa waliingizwa katika agano gani?

7 Msamaha huu wa dhambi unaotokeza dhamiri nzuri kwa Mungu ndio Yeye alikuwa ameahidi katika masharti ya agano jipya. Wakati Yehova alipotabiri juu ya agano jipya kupitia kwa nabii Yeremia, Yehova alimalizia unabii huu kwa kusema: “Maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” (Yer. 31:31-34) Karne zilizofuata, wakati mtume Paulo alipowaandikia Waebrania wa Kikristo, waliokuwa wazao wa asili wa Ibrahimu, “rafiki ya Yehova,” alitumia maneno ya unabii wa Yeremia na akaendelea kusema hivi: “Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena. Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.” (Ebr. 8:12, 13) Kwa hiyo, Wayahudi elfu tatu waliotubu na wakabatizwa katika jina la Yesu Kristo na kupokea zawadi ya bure ya roho takatifu waliingizwa katika agano jipya kupitia kwa ‘mpatanishi aliye bora,’ Yesu Kristo.​—Matendo 2:41.

8, 9. Siku fulani zilizofuata katika hekalu, Petro aliwaelekeza Wayahudi kwa nani, na alitangaza kwamba ilikuwa lazima wafanye nini, kwa matokeo gani kwao?

8 Siku fulani kufuata tukio la Pentekoste, Petro na Yohana walijikuta wenyewe wako hekaluni katika Yerusalemu. Katika kusema na makutano ya watu waliokusanyika kuwazunguka, Petro tena aliwaelekeza Wayahudi kwa Wakili Mkuu wa utawala wa kimungu. Tena Petro aliwaambia lazima watubu na kuongoka, kutafuta burudisho linalotokana na msamaha wa dhambi zao kutoka kwa Mungu kupitia kwa Kristo. Petro aliendelea kusema hivi:

9 “Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, Mungu wa babu zetu, amefanya heshima hii kwa mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlisaliti na mkamkana mbele ya Pilato, wakati alipokuwa ameamua kumwachilia. Lakini ninyi mlimkana Mtakatifu, Mwenye Haki. Ninyi mkaomba mfunguliwe mwuaji, na mkaua chanzo chenyewe [Mkuu, UV; Wakili Mkuu, NW] cha uzima. Lakini Mungu alimwinua yeye kutoka kwa wafu, kama sisi tuwezavyo kushuhudia. . . . Basi tubuni na kugeukia kwa Mungu, mpate kufutisha dhambi zenu, na nyakati zenye furaha zaidi zitakuja kutoka kwa kuwapo kwa Bwana, naye atamtuma Yesu, Kristo wenu ambaye mliwekewa. . . . Ilikuwa kwenu ninyi kwamba Mungu kwanza akamtuma mtumishi wake alipokwisha kumwinua kutoka kwa wafu, kuwabariki ninyi kwa kumfanya kila mmoja wenu aache uovu wake.”​—Matendo 3:13-26, AT; UV; NW.

10. Sababu gani wakati huo kulikuwa hakuna ubatizo wa Wayahudi wenye kutubu, na Petro na Yohana waliiambia Korti ni jina gani peke yake ambalo kwa hilo wokovu unapatikana?

10 Wakati Petro na Yohana walipokuwa hawajaweza kufanya mpango kwa Wayahudi wo wote wenye kutubu mle hekaluni wapate kubatizwa, hali iligeuka, kwa maana tunasoma hivi: “Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.” (Matendo 4:1, 2) Basi Petro na Yohana walitiwa kifungoni usiku, na kesho yake walihukumiwa na wakafunguliwa. Mbele ya Korti walitangaza kwamba hakuna jina jingine chini ya mbingu ambalo limepewa kati ya wanadamu kwa kuokolewa kwalo isipokuwa jina la Wakili Mkuu wa utawala wa kimungu wa Yehova. (Matendo 4:3-23) Mitume walikataa kuacha kumfuata yule mwenye jina la maana sana.

11. (a) Filipo mhubiri wa injili alikuja kuhubiri katika Samaria namna gani? (b) Wasamaria wenye kuamini walibatizwa katika jina la nani, na hivyo wakawa wanafunzi wa nani?

11 Mwisho kukatokea mateso makali sana katika Yerusalemu na Mkristo Myahudi mwaminifu Stefano alipigwa kwa mawe mpaka akafa. Wanafunzi wa Kristo walitawanyika kutoka Yerusalemu, isipokuwa mitume kumi na wawili. Kati ya wale waliotawanyika alikuwako Filipo Mhubiri wa Injili. Yeye alikwenda kaskazini kwenye mji wa Samaria “akawahubiri Kristo.” Filipo alileta furaha kuu kwa mji kwa yale aliyohubiri na kwa ishara za miujiza ambazo alifanya. Wasamaria waliamini sana vile vitabu vitano vilivyoandikwa na Musa, na walikuwa wakitahiriwa. Kwa hiyo, wengi kati yao walimkubali Yesu Kristo kama ‘mpatanishi aliye bora’ aliyefananishwa na Musa. Kwa habari ya hao Wasamaria wenye kuamini, Filipo alitimiza ambalo Yesu alikuwa ameamuru kufanya, kwa maana tunasoma hivi: “Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.” (Matendo 8:1-13; Mt. 28:19, 20; Matendo 1:8) Wasamaria hao walibatizwa katika jina la Yesu; wakawa wanafunzi wake waaminio, waliobatizwa.

12. (a) Filipo alikuja namna gani kumhubiri towashi Mwethiopia katika gari lake, na Filipo alimbatiza katika jina la nani? (b) Ni mwendo gani ambao ubatizo huo ulionyesha kwamba Mwethiopia alikuwa amechukua?

12 Alipokwisha kufanya wanafunzi wengi kati ya Wasamaria waliotahiriwa, Filipo aliongozwa na malaika wa Mungu kwenda kwa mwongofu wa dini ya Kiyahudi aliyetahiriwa. Mtu huyu, towashi Mwethiopia, alikuwa akirudi kutoka kuabudu Yerusalemu. Wakati Filipo alipolaki gari na kumsalimu, yule Mwethiopia alikuwa akisoma katika unabii wa Isaya, katika sura ambayo sasa ni ya hamsini na tatu. Yule Mwethiopia alimwuliza Filipo juu ya nani ambaye Isaya alikuwa akisema katika sura hiyo. Ndipo, kama Matendo 8:35 linavyotuambia, “Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.” Tena Filipo alimwambia yule Mwethiopia juu ya ubatizo wa maji, na yule mtu akaomba abatizwe mara walipofika palipokuwa na maji mengi. Bila shaka, Filipo alimbatiza katika jina la Yesu. (Matendo 8:36-39) Kama Wasamaria wale wenye kuamini, Mwethiopia huyu aliyetahiriwa alijitoa mwenyewe kwa Yehova Mungu afanye mapenzi yake kama mwanafunzi wa Yesu Kristo.

“KUONGOKA KWAO MATAIFA”

13. (a) Mataifa wanatofautianaje na Wayahudi juu ya daraka kwa mauti ya Yesu na kwa habari ya laana ya Torati? (b) Yehova alianza kutoa toba kwa Mataifa wakati gani na pamoja na nani?

13 Bila kuwa kama Wayahudi waliotahiriwa walioshiriki katika lawama la kumwua Yesu Kristo nje ya Yerusalemu, watu wa Mataifa hawakupaswa watubu juu ya kuwa na sehemu yo yote katika kumpigilia misumari Mwana wa Mungu asiye na hatia. Wao hawakuwa chini ya laana ya agano la Torati ya Musa. (Gal. 3:13) Walakini, wao walikuwa wenye dhambi waliotokana na Adamu na Hawa wenye dhambi, na walikuwa na dhambi nyingi za kipagani ambazo walipaswa wazitubie na ambazo kwa hizo walilaaniwa na Mungu kufa. Walikuwa, kama mtume Paulo alivyowaambia, “mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.” (Efe. 2:12) Kwa desturi walikuwa watu wasiotahiriwa. Lakini katika mwaka wa 36 C.E. Yehova Mungu kwa rehema alianza kuwapa “mataifa nao toba liletalo uzima,” kupitia kwa Yesu Kristo. (Matendo 11:18) Mtu ambaye walianzia alikuwa Kornelio wa Kaisaria. Mji huu ulikuwa kiti cha jimbo cha Pontio Pilato, gavana wa Kirumi wa jimbo la Uyahudi.

14. Je! Komelio na wale waliokusanyika pamoja katika nyumba yake walikwisha kujua jambo fulani juu ya Yesu, na Petro aliwaambia nini juu ya kupata msamaha wa dhambi?

14 Kornelio akida wa Kiitalia na wale ambao alikuwa amekusanya katika nyumba yake walikuwa wamekwisha kujua habari fulani juu ya Yesu Kristo. Basi mtume Petro, aliyetumwa kuhubiri kwao, aliwaambia hivi: “Ninyi mnajua habari iliyokuwa ikizungumzwa katika sehemu yote ya Uyahudi, kuanzia Galilaya baada ya ubatizo ambao Yohana alihubiri, yaani, Yesu aliyekuwa mtoka Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa roho takatifu na nguvu, naye alipita katika nchi akifanya mema na kuponya wale wote walioonewa na Ibilisi; kwa sababu Mungu alikuwa pamoja na yeye. Na sisi ni mashahidi wa mambo yote ambayo alifanya.” Petro aliendelea kusema hivi kwa kumalizia: “Manabii wote wanamshuhudia yeye, kwamba kila mtu anayeweka imani katika yeye anapata msamaha wa dhambi kupitia kwa jina lake.”​—Matendo 10:37-43, NW.

15. Jambo gani linaonyesha kama Mataifa hao wenye kusikiliza walipokea msamaha wa dhambi, na, kwa amri ya Petro, waligeuka kuwa nini?

15 Kwa kimya, katika mioyo yao, Kornelio na Mataifa hao waliokusanyika pamoja naye wakawa waamini katika Yesu Kristo nao wakapokea msamaha huu wa dhambi kupitia kwa jina lake na kwa sababu hiyo dhamiri njema kwa Mungu. Ulikuwa ushuhuda gani wa hilo? Masimulizi yanatuambia, kusema: “Wakati Petro alipokuwa bado akisema juu ya mambo haya roho takatifu iliwaangukia wale wote waliokuwa wakisikia neno. Na waaminifu waliokuwa wamekuja pamoja na Petro. . . waliwasikia wakisema kwa lugha na [kumtukuza] Mungu. Ndipo Petro alipojibu: ‘Je! ye yote anaweza kukataza maji ili hawa wasibatizwe ambao wamepokea roho takatifu hata kama sisi tulivyopokea?’ Ndipo alipowaamuru wabatizwe katika jina la Yesu Kristo.” (Matendo 10:44-48, NW) Hawa wakawa wanafunzi wa Kristo waaminio.

16. Paulo na Sila walijikutaje wamo jela katika Filipi ya Makedonia, na usiku wa manane kulitukia nini?

16 Huu ulikuwa mwanzo, na kutoka hapo, kwa kadiri wakati ulivyosonga mbele, Mataifa wengine wasiotahiriwa waliongoka na wakabatizwa katika jina la Yesu. Chukua mfano wa yaliyotukia katika Filipi ya Makedonia, karibu na mwaka wa 50 C.E. Mtume Paulo alipokuwa amekwisha kumponya mwanamke kijana mwenye kupagawa na mashetani ya uaguzi, yeye na mwenzi wake Sila walifungwa kwa mashtaka ya uongo. Karibu usiku wa manane, wakati walipokuwa wakisali na kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kulitukia tetemeko kubwa la dunia na kwa mwujiza wafungwa wote wakajikuta wenyewe wamefunguliwa. Paulo alimpazia sauti mlinzi wa jela aliyeshikwa na woga akamwambia asijiue, maana wafungwa hawakuwa wametoroka. Sasa jambo gani lilitukia? Na tusome:

17. Paulo na Sila walimwambia mlinzi wa jela na nyumba yake waokoke namna gani, nao waliitikiaje habari hii?

17 “Akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Wakamwambia neno la [Yehova], yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.”​—Matendo 16:29-34.

18. (a) Mlinzi wa jela na nyumba yake waligeuka kuwa washiriki wa kikundi gani? (b) Kulingana na amri “Mwamini Bwana Yesu,” je! tendo kubwa la wokovu lilipaswa lielekezwe kwa Yesu, na jibu linatolewa namna gani na yaliyotukia muda uliofuata hapo katika habari hiyo?

18 Mlinzi huyu wa jela Mfilipi asiyetahiriwa na nyumba yake wakawa washiriki waliobatizwa wa kundi la Kikristo katika Filipi, na bila shaka wakapokea na roho takatifu kwa kuwekewa mikono na mtume Paulo. (Flp. 1:1) “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka,” ndivyo walivyoambiwa. Mengi yanapaswa yafahamike katika usemi huo, “Mwamini Bwana Yesu.” Huu, na vile vile ukweli wa kwamba Kornelio Mtaifa asiyetahiriwa na waamini wenzake katika nyumba yake ‘walibatizwa katika jina la Yesu Kristo,’ unatokeza ulizo, Tendo kubwa la wokovu lilielekezwa kwa nani​—kwa Yesu Kristo au kwa Yehova Mungu? Jibu linatolewa na ukweli wa kwamba, akiisha kumwambia yule mlinzi wa jela Mfilipi namna ya ‘kuokoka,’ Paulo na Sila “wakamwambia neno la [Yehova]” na nyumba yake yote na mlinzi wa jela walifurahi sana “maana amekwisha kumwamini Mungu.”

19. Kulingana na Paulo, ilikuwa hali gani ya kidini au ya kiroho ya wapagani hao wasiotahiriwa, na ilikuwa lazima wajiweke wenyewe wakf kwa nani ili wapate wokovu?

19 Yatupasa tukumbuke kwamba wapagani hawa wasiotahiriwa hawakuwa ‘hawana Kristo’ tu, bali vile vile ‘wamefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile’ na ‘hawana Mungu duniani.’ (Efe. 2:12) Wao walikuwa wa jamii ile ya wapagani ambao Paulo aliandikia, akisema: “Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.” Tena: “Jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli.” (1 Kor. 12:2; 1 The. 1:9) Walijiweka wakf kwa sanamu hizo au kwa miungu ya uongo iliyofananishwa na sanamu hizo. Inaelekea walikuwa na alama miilini mwao kuonyesha waziwazi walijitoa sana kwa mungu gani. (Linganisha Ezekieli 9:4-6; Hosea 9:10.) Kwa desturi, basi, wapagani hawa wajinga wasiotahiriwa walipaswa wasikie habari za “Mungu aliye hai, wa kweli,” ambaye ni Yehova. Ndipo, ili wapate wokovu, iliwapasa wajiweke wenyewe wakf kwa Yeye, wafanye mapenzi yake. Mungu huyu angewapasha habari ni kupitia kwa nani kujiweka wakf huku kwake Yeye kungeweza kufanywa. Wakimtii Yeye, wangeweza kubatizwa.

20, 21. Katika Warumi, sura ya kumi, ni maneno gani ya Musa kwa Waisraeli ambayo Paulo anatumia juu ya kupatikana kwa amri ya Mungu?

20 Utaratibu huu unawekwa waziwazi na mtume Paulo katika Warumi, sura ya kumi. Humo, katika mistari tano kufika kumi, anatumia maneno ambayo Yehova Mungu alimwongoza Musa kusema katika Kumbukumbu la Torati 30:11-14, NW. Hivi ndivyo andiko hili la pili linavyosomwa:

21 “Kwa maana amri hii ambayo ninakuamuru wewe leo si ngumu mno kwako, wala haiko mbali. Haiko katika mbingu, hata itokee katika kusema, ‘Ni nani atakayetupandia katika mbingu na kutuletea sisi, apate kutusikizisha tupate kuifanya?’ Wala haiko upande mwingine wa bahari, hata itokee katika kusema, ‘Ni nani atakayetuvukia upande mwingine wa bahari na kutuletea sisi, apate kutusikizisha tupate kuifanya?’ Kwa maana neno liko karibu sana na wewe, katika kinywa chako mwenyewe na katika moyo wako mwenyewe, upate kulifanya.”

22. (a) Amri ya Mungu ilikujaje kuwa karibu sana na Waisraeli hao katika nyanda za Moabu, hata katika vinywa vyao na mioyo yao? (b) Basi ni jambo gani peke yake lililobaki kwa Waisraeli hao kufanya? (c) Kufanya kwao hivi kulionyeshwa kwa kufanya kwao nini pamoja na Mungu wakati huo?

22 Na tufahamu kwamba Musa aliyeongozwa na roho ya Mungu anaita hili “amri,” jambo fulani ambalo inawapasa walifanye kwa Mungu. Kutoka Mlima Sinai na kuendelea “amri” hii imefunuliwa kwao katika njia yenye kufahamika. Kwa sababu ya kusemwa mara nyingi kwa taratibu hii ya sheria wakati wa miaka arobaini, wanaijua na wanaweza kuisema kwa vinywa vyao, kana kwamba ilikuwa katika ncha ya ulimi wao. Tena ilikuwa imetiwa kwa mkazo katika mioyo yao, ili kuwasaidia wapate maana yake na kuifahamu. Hivyo, jambo lililobaki kwao sasa lilikuwa kwao kuamua kufanya mapenzi haya ya Mungu yaliyosemwa. Kwa wazi hivi ndivyo Yehova alivyowasadia Waisraeli hao kufanya kwa kuwaagiza wafanye agano la nyongeza pamoja na yeye kupitia kwa Musa. Kwa habari ya hili, Kumbukumbu la Torati 29:1 linasema hivi: “Haya ndiyo maneno ya agano [Yehova] alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, [zaidi ya] agano alilofanya nao Horebu.”

23. (a) Nani anayetueleza maana iliyofananishwa na hilo, na wapi? (b) Mungu aliufanya mpango huu kwa haki uwe karibu kwa kadiri gani na Wayahudi, lakini kwa sababu gani walishindwa kuutumia kwa faida nzuri?

23 Yote hayo yalikuwa na maana ya mfano, kufananisha jambo fulani kukamatana na Musa Mkubwa Zaidi, ‘mpatanishi aliye bora,’ Yesu Kristo. Mtume wa Kikristo Paulo anatueleza maana iliyofananishwa, katika barua yake kwa Warumi, sura ya kumi, ili kuonyesha namna tunavyoweza kupata haki na Mungu na dhamiri njema kwake. Hii inataka imani kwa Mungu, kwa vile haki haiwezi kupatikana kwa jitihada za mtu mwenyewe kushika Torati ya Musa. Wakizitumaini kazi zao wenyewe ziwashuhudie kuwa wenye haki mbele za Mungu, Wayahudi waliona hakuna lazima ya kutumia imani katika mpango ambao Mungu alifanya upatikane kwao, akiuweka karibu nao, katikati yao, ambapo wangeweza kuupata. Ili kupata wokovu, inawapasa Wakristo wafanye tofauti kabisa na Wayahudi hao wasioamini.

KUUNGAMA KWA KINYWA

24. (a) Musa alisema nini kwa habari ya Torati na kupata uzima, lakini haki inayotaka imani inasema nini juu ya kupatikana kwa amri ya Mungu? (b) Moyo na kinywa vina sehemu gani juu ya haki na wokovu?

24 Kupatana na takwa hili, ambalo ni kulingana na amri ya Mungu, mtume Paulo anaendelea kusema hivi: “Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo. Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? yaani, ni kumleta Kristo chini, au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu. Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”​—Rum. 10:5-10.

25. (a) Paulo alilifanya “neno” hilo liwe karibu kwa kadiri gani na Mataifa, na Bwana Yesu aliifanyaje kwa pekee habari hiyo iwezekane kwetu kuwa nayo? (b) Kwa vile sasa “neno” hilo lilikuwa karibu sana, lilikuwa ulizo gani kwa habari ya wale wanaotafuta wokovu?

25 “Neno” juu ya Mungu na Kristo wake lililetwa karibu na watu wa Mataifa zaidi kwa njia ya mtume Paulo, aliyekuwa, “kwa hakika, mtume kwa mataifa,” na kwa wamisionari wenzake hata waliweza kulisema mara nyingi kwa vinywa vyao na kulipokea kwa kushukuru katika mioyo yao. Tena, Yesu Kristo alikuwa amefanya habari hii ipatikane kwao kwa kushuka kutoka mbinguni atoe ushuhuda juu ya Mungu na kusudi lake; naye vile vile alikuwa amefufuliwa na Mwenyezi Mungu kutoka kwa wafu ili apate kuwa ushuhuda ulio hai wa kutendeka na kutimizwa kwa kusudi la Mungu. Tena ilishuhudiwa kwa njia hiyo bila kukosea kwamba yeye alikuwa ndiye “Bwana,” Wakili Mkuu wa utawala wa kimungu wa Yehova. Basi lile “neno” lenye kuokoa uhai lilikuwako, mahali ambapo Mataifa hawa waliweza kulipata, karibu nao kama katika vinywa na mioyo yao. Lakini ulizo lilikuwa hivi, Wangelifanyia nini? Ikiwa walitaka wokovu wa milele, kulikuwako jambo moja tu kwao kufanya juu yake. Vile vile, jambo ambalo walipaswa wafanye nalo ili wapate wokovu waliamriwa na Mungu mwenyewe. Kumbuka kwamba Musa aliongozwa na roho ya Mungu aliite “neno” hilo “amri hii ambayo ninakuamuru wewe leo.” (Kum. 30:11-14, NW) Ili tuokoke, lazima tutii.

26, 27. (a) Ni “neno” gani ambalo Mungu anatuamuru sisi tulikubali katika imani? (b) Yesu aliwaambia Wayahudi ni nini kilichokuwa “kazi ya Mungu” ambayo waliuliza, na Paulo alisemaje kwa Wagiriki katika kilima cha Areopago, Athene, kwamba hii ndiyo “kazi” ambayo Mungu anaamuru?

26 Ndiyo, Yehova Mungu, anayeweka masharti yote ya wokovu, anaamuru kwamba tukubali kwa imani lile neno, yaani, kwamba Yesu Kristo ni Bwana na kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Hivi ndivyo Yesu alivyowaambia Wayahudi sawasawa katika ulizo lao: “Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.” (Yohana 6:28, 29) Hii vile vile inawapasa wale wasio Wayahudi au Mataifa wasiotahiriwa. Kwa hiyo hakuna mwendo mwingine unaobaki ila Mataifa waliopashwa habari wajiweke wakf kwa Mungu wafanye mapenzi ya Mungu, waitende kazi ya Mungu. Inawapasa waiache miungu ya uongo ya sanamu ambayo mpaka wakati huo walikuwa wamejiweka wakf kwayo. Hii inapatana na ambayo mtume Paulo aliwaambia Wagiriki wapagani waliokusanyika juu ya kilima cha Areopago, Athene:

27 “Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.”​—Matendo 17:30, 31.

‘KUKIRI HATA KUPATA WOKOVU’

28. (a) Tunaamriwa tufanye nini kwa njia ya moyo? (b) Ni “neno” gani ambalo inatupasa tulikubali kwa imani? (c) Tunasitawishaje imani hiyo katika mioyo yetu, ili tufanye nini?

28 Kupatana na wakf wetu kwa Yehova Mungu kufanya mapenzi yake kwa kushika amri zake, inatupasa kwa kutii tufanye kama ilivyoamriwa: “kuamini moyoni mwako.” Tunajua kwamba moyo ndiko kunakotoka upendo na kwamba una nguvu ya kumsukuma mwenyewe. Kwa huo tunaona shukrani. Basi kwa moyo inatupasa “kuamini” nini? Kuamini lile “neno” ambalo Yehova Mungu amelileta karibu na sisi kwa njia ya Yesu Kristo. Mtume Paulo anasema kwamba “neno” hili, kulingana na usemi wake, “ni lile neno la imani tulihubirilo.” Kukubali kwa “neno” hilo lililohubiriwa na mtume Paulo kunataka kutumia imani, nasi inatupasa tufanye hivi kwa moyo. Inatupasa tuweke mioyo yetu juu ya “neno” hilo lililohubiriwa. Katika mioyo yetu inatupasa tusitawishe upendo wa “neno” hilo. Kwa mioyo yetu inatupasa tuongeze ubora wa unyofu wa moyo wa “neno” hilo. Hali hii ya moyo itamwongoza au kumsukuma mtu aliamini neno hilo na kulikubali na kutenda juu yake.

29. Inatupasa tuamini nini katika mioyo yetu, na hivyo tendo letu kubwa linaelekezwa kwa nani ili kupata wokovu?

29 Ni kwa habari ya nini tunatakiwa “kuamini moyoni [mwetu]”? Kwa habari hii: “ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu.” Ah, hapa tunaona kwamba si “mwamini Bwana Yesu” tu ili kupata kuokoka. (Matendo 16:31) Kwanza ya yote, inatupasa tumwamini Mungu. Bado ingali kweli, kama Paulo anavyotukumbusha, kwamba “kila atakayeliitia Jina la [Yehova] ataokoka.” (Rum. 10:13) Ni Yehova ndiye inatupasa tupende kwa moyo wetu wote, nafsi, akili na nguvu. Yeye ndiye Mwenye Nguvu Zote aliyemfufua Yesu Kristo kutoka kwa wafu kwenda kwenye uzima usioweza kufa. Kwa hiyo kwa Yehova ndiko tendo letu kubwa linakoelekezwa. Ni kwake yeye ndiko inatupasa tujiweke wakf tufanye mapenzi Yake, tuzishike amri Zake.​—Rum. 10:8, 9.

30. (a) Kwa mioyo yetu, inatupasa tuamini nini kwamba Mungu alifanya juu ya Yesu Kristo? (b) Hivyo ni katika maana gani Mungu alifanya lile “neno” lipatikane kwetu?

30 Hivyo mioyo yetu iliyowekwa wakf, yenye kujaa upendo na shukrani, yapaswa ituongoze tuamini kwamba Yehova Mungu alifanya mwujiza mkubwa wa kumfufua Yesu Kristo aliyepigiliwa misumari kutoka kwa wafu. Katika njia hiyo Mungu alifanya iwezekane kwa Yesu Kristo kupaa mbinguni panapo Mungu na kutoa huko bei ya dhabihu yake yenye kupatanisha kwa faida ya wanadamu wote, hivyo kuwanunua wote. Kwa kufa kama dhabihu, Yesu Kristo alishuka kwenda “kuzimuni,” lakini roho au nguvu ya utendaji ya Yehova ilishuka “kuzimuni” huko ili “kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.” Hivyo kwa njia ya Kristo aliye hai, Mungu Mwenye Nguvu Zote Yehova aliweza kufanya lile “neno” lipatikane kwetu, aliweza kutoa yaliyomo au maana kwa “neno” hilo, aliweza kulifanya “neno” hilo liwe na ujumbe ndani yake wenye kutoa uzima kwetu. Basi, mambo yote yameangaliwa, Yehova ndiye mkubwa ambaye kwake imetupasa tuchukue tendo kwa kujiweka wenyewe wakf kwake. Lakini inatupasa tufanye hivi kupitia kwa Wakili Mkuu wake, Yesu Kristo.​—Rum. 10:6, 7; Ebr. 2:9, 10; 5:8, 9.

31. Basi inatupasa tuite juu ya jina la nani ili kupata wokovu, lakini kwa sababu gani vinywa vyetu lazima vile vile vikiri juu ya Yesu Kristo?

31 Kwa hiyo ni lazima tuite juu ya “Jina la [Yehova]” ili kuokoka. (Rum. 10:13; Matendo 2:21; Yoeli 2:32) Hii inataka kinywa, kama kinavyosukumwa na moyo, kifanye jambo fulani. Kwa kinywa tuna wajibu wa kuita juu ya jina la Yehova. Lakini sasa, kwa kuwa Mungu alimleta juu Kristo kutoka kwa wafu, sisi hatuwezi kuita hivi bila Yesu Kristo. Kwa vinywa vyetu inatupasa vile vile tufanye ungamo juu ya Yesu Kristo. Ndiyo sababu mtume Paulo, wakati wa kuzungumza lile “neno” la imani ambalo alikuwa akihubiri, anaendelea kusema hivi: “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana [1] kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na [2] kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”​—Rum. 10:9, 10.

32. (a) Kukiri huku kwa vinywa vyetu kunasemwa kama nini katika tafsiri nyingine za Biblia? (b) Kukiri huku kwa mdomo ili kupata wokovu kunafanywa wakati gani?

32 Ni wakati gani ambao mtu “kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”? Hii ni na yapaswa iwe mbele ya kubatizwa kwa mwamini aliyejiweka wakf “katika jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu.” (Mt. 28:19, 20, NW; Matendo 16:31-33; 17:33; 19:1-7) Kukiri huku ni ungamo, kama Kingdom Interlinear Translation na tafsiri nyingine za Biblia zinavyoonyesha. (RS; Mo; Je; AS) Ungamo au kukiri huku ndiko tunakofanya kwa mdomo kwa au mbele ya mhudumu wa Kikristo anayesimamia ubatizo wa maji. Bila shaka tunaendelea kufanya hivi katika mikutano yetu ya kundi. (Ebr. 10:23) Tena, mbele ya mamlaka za serikali au za hukumu ambao huenda wakataka maelezo juu ya tumaini letu la Kikristo. (1 Pet. 3:15) Tena, katika kazi yetu ya wazi ya kuhubiri nyumba kwa nyumba na katika ziara zetu za kurudia kwenye nyumba za watu ambao tumeona wanapendezwa. Lakini, kwa lazima, ungamo hili linaanza mbele ya ubatizo. Ushuhuda wa mdomo tu kama mtu asiyejiweka wakf mbele ya ubatizo hauokoi.

33. Ungamo maana yake nini, na inatupasa tuungame nini mbele ya wengine ili kupata wokovu?

33 Bila shaka, ungamo linamaanisha kutangaza, kufunua, kukubali au kukiri jambo fulani kwa mwingine au kwa wengine. Hivyo, sasa, ni jambo gani ambalo inatupasa tutangaze, au tukiri, kwa neno la kinywa kwa wengine? Ni “neno” lile, bila shaka. Paulo anasema hivi: “Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, . . . utaokoka.” (Rum. 10:9) Hivyo hatuwezi kumwacha Yesu Kristo katika makusudi na mipango ya Mungu, kwa maana Yesu ndiye “Wakili Mkuu wa wokovu wao.” (Ebr. 2:10, NW) Kwa mdomo inatupasa tutangaze, tuungame, tukubali, tukiri kwamba Yesu si, “Bwana” wa Mfalme Daudi peke yake, bali vile vile “Bwana” wetu sisi. (Zab. 110:1; Matendo 2:34-46) Inatupasa tufanye tangazo hili mbele ya wengine kulingana na lile “neno” lililoongozwa na roho ya Mungu.

34. Kulingana na 1 Wakorintho 12:2, 3, ni chini ya uongozi wa nini tunaungama kwamba Yesu ni Bwana, na ni kwa muda gani tunashika sana ungamo hilo kwa wokovu?

34 Hii ndiyo sababu mtume Paulo alisema: “Kwa hiyo mimi ningetaka ninyi [waabudu wa zamani wa sanamu] mjue kwamba hakuna mtu anaposema kupitia kwa roho ya Mungu anayesema hivi: ‘Yesu ni mlaaniwa!’ na hakuna mtu anayeweza kusema: ‘Yesu ni Bwana!’ isipokuwa kupitia kwa roho takatifu.” (1 Kor. 12:2, 3, NW) Roho ya Mungu ndani yetu inatuongoza tufanye ungamo zuri, kukiri au tangazo zuri kwa wengine, yaani kwamba Yesu ni “Bwana” aliyewekwa na Mungu. Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu apate kuwa Bwana aliye hai. Mungu alimketisha Yesu aliyefufuka kwenye mkono wake mwenyewe wa kuume na akamfanya kuwa “Bwana” juu zaidi kuliko kuumba kwingine kote. Ikiwa tunatamani wokovu wa milele, inatupasa tushike sana tangazo, ungamo, kukiri kule tulikofanya mbele ya ubatizo wetu wa maji, yaani, kwamba Yesu Kristo ndiye Bwana ambaye Yehova Mungu ameweka juu yetu na ambaye tunakubali kwa upendo.

KUJIKANA MWENYEWE

35. Yesu aliwaambia mitume wake jambo gani lapaswa lifanywe na mtu anayetaka kumfuata?

35 Kuungama kwa kinywa chetu kwamba Yesu ni Bwana wetu kunaweka wajibu fulani juu yetu. Yesu aliutaja huu alipokwisha kumkemea Petro kwa kujaribu kumzuia asiendelee na njia yake mpaka kufa penye mti wa mateso katika Yerusalemu. Tunasoma hivi: “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.” (Mt. 16:24) Katika kueleza maana ya “kukana,” The American College Dictionary inasema: “4. Kukataa kujua au kukubali; kukataa uenyeji, kukataa kuwa na uhusiano na kitu fulani.”

36. (a) Petro alimkana Yesu mara tatu wakati gani, na kwa hiyo alikuwa akimkiri nani? (b) Kwa kumkana Yesu, Petro alijidai kuwa wa nani?

36 Usiku wa kusalitiwa kwa Yesu na Yuda Iskariote, mtume Petro alimkana Yesu mara tatu. Wale waliomdhania Petro walimshtaki mara tatu kuwa mshiriki wa Yesu, ndipo, kama Mathayo 26:74 anavyotuambia, Petro “akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu.” Kwa kumkana Yesu hivyo, Petro alijiondoa mwenyewe katika washiriki au wafuasi wa Yesu. Kwa kufanya hivi, Petro hakumwondoa kutoka kwa kila mtu mwingine na kumweka upande wake mwenyewe. Hapana, bali, yeye alijiweka mwenyewe na au upande wa wale ambao hawakumfuata Yesu, lakini walioona yampasa Yesu afikishwe kwenye hukumu ya uhai wake. Au, kutumia neno jingine, “kukataa uenyeji,” kwa kukana kuwa yeye si wa Yesu kama kiongozi na Mwalimu wake Petro alikuwa akidai kuwa yeye ni wa mwingineo kama kiongozi na mwalimu wake. Kwa kukana kuwa yeye si wa Yesu, Petro hakuwa akijiweka mwenyewe katika hali ya kutokuwamo, hali ya kutokupendelea upande huu wala upande huu wa ulizo, hali iliyojitokeza yenyewe tu na isiyompasa ye yote mwingineo. Kwa kukana kuwa yeye si wa Yesu, Petro alipaswa ajidai kuwa wa mtu mwingineo.

37. Basi kujikana mwenyewe ili kuwa mfuasi wa Yesu kuna maana gani, na hili linatanywa kulingana na mapenzi ya nani?

37 Ndivyo ilivyo na yale ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika Mathayo 16:24. Kwa kujikana na kujichukulia mti wa mateso na kuendelea kumfuata Yesu, mtu hajiambii mwenyewe Hapana! kwa habari ya tamaa ya kipekee sasa na tamaa nyingine ya kipekee wakati huo. Kwa kweli, yeye anajiambia Hapana! kwa habari ya sehemu inayobaki ya mwendo wake wa maisha kama asiye mfuasi mwenye choyo wa Yesu Kristo. Kwa kujikana mwenyewe yeye anauacha mwendo huo wa maisha wa kujitafutia yake mwenyewe, wa kupenda mambo ya kimwili na anakuwa mfuasi wa Yesu, akichukua mti wa mateso wa mauti kama Yesu alivyofanya. Yeye anajikana mwenyewe kuwa hajiongozi mwenyewe na kujifanyia uamuzi wake mwenyewe na anamkubali, anamkiri Yesu Kristo kama ndiye Kiongozi na Mwalimu wake. Bila shaka, hatua inachukuliwa kulingana na mapenzi ya Mungu.

38. Kujikana wenyewe ili tumfuate Yesu kunamaanisha nini, na, kama yeye, sisi tunakuwa watumwa wa nani?

38 New World Translation inatafsiri Mathayo 16:24 hivi: “Ikiwa ye yote anataka aje baada yangu, mwacheni ajikane mwenyewe na kuchukua mti wake wa mateso na kunifuata sikuzote.” Basi, hapa kujikana mwenyewe kuna maana gani? Kwa hakika kuna maana ya mtu kutodai tena yeye mwenyewe ni wake mwenyewe. Katika habari hiyo, sisi tunakubali au tunakabidhi uenyeji wa sisi wenyewe kwa mwingineo na kukiri, kukubali, uenyeji wa mtu huyu juu yetu. Hatuwi watu wasio na mwenyewe. Ni nani, basi, anayekuwa mwenye sisi kwa sababu ya kujikana kwetu wenyewe halafu tunakuwa wachukuzi wa mti kumfuata Yesu Kristo sikuzote? Bila shaka, Yesu alijikana mwenyewe; jambo lililomaanisha kwamba yeye aliukubali, aliukiri uenyeji wa Yehova juu yake, na yeye mwenyewe kama mtumwa wa Yehova. Kwa kupatana, basi, wakati sisi, ili tuwe mfuasi ya Yesu, tunapojikana wenyewe, sisi tunakubali, tunakabidhi, uenyeji wa sisi wenyewe kwa Yehova, ambaye tunakuwa mtumwa wake kama Kristo. Sisi hatuwi tena wa sisi wenyewe.

39. (a) Basi, hili linataka tendo gani upande wa wale wanaofanya uchaguzi huo? (b) Hilo linafananishwaje, lakini ni wakati ungamo gani linapokwisha kufanywa peke yake?

39 Basi, jambo hili linataka nini kwa upande wetu sisi tunaofanya uchaguzi huu? Linataka kujiweka kwetu wenyewe wakf kabisa kwa Yehova Mungu tufanye mapenzi yake kuchukua mfano wa Mwana wake Yesu Kristo. Mapenzi yake kwetu ni kuwa wanafunzi waaminifu wa Yesu Kristo. Mapenzi yake kwetu ni kutangaza, kuungama, kumkiri Yesu Kristo kama “Bwana” wetu aliyewekwa na Mungu. Ndivyo Yesu anavyokuwa Bwana wetu mwenye mamlaka ya kutuamuru sisi na kutugawia sisi kazi zetu. Kujiweka huku wakf kwa Yehova Mungu, bila shaka, tunakufanya tukiisha kutubu na kugeukia kwake. Mwendo wetu wa maisha uliogeuzwa tunautimiza kwa kujiweka wenyewe wakf kwa Yehova Mungu kupitia kwa Wakili Mkuu wake Yesu Kristo. Sasa tunaonyesha kujiweka huku wakf kwa kuzamishwa katika maji. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu, mapenzi ambayo tumejiweka wenyewe wakf kwa Yeye tuyafanye. Mbele ya ubatizo wa maji inatupasa tufanye tangazo la wazi au ungamo kwa vinywa vyetu kwa wokovu, kufanya hivi kwa kusema wazi-wazi yale tunayosadiki katika mioyo yetu. Kwa kufanya hivi peke yake ndipo tunaingia katika njia ya wokovu wa milele unaotoka kwa Mungu kupitia kwa Kristo.

[Picha katika ukurasa wa 235]

‘Kukiri hata kupata wokovu’ kunakofanywa na waamini walio wakf kunaanza mbele ya ubatizo wanapojibu kwa mdomo maulizo ya mhudumu anayesimamia ubatizo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki