Kumtokeza Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu
“Mungu alimfanya huyu kuwa mkuu kama Wakili Mkuu na Mwokozi kwenye mkono wake wa kuume, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.”—Matendo 5:31, NW.
1. Kwa sababu gani haitatuletea wokovu ikiwa tunamkataa Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu?
YEYE ambaye Mtawala wa Kimungu wa ulimwengu wote anafanya mkuu ili awe Wakili Mkuu wake na Mwokozi sisi hatuwezi kukataa kumwangalia. Kama tungekataa kumwangalia Wakili Mkuu huyo na kujaribu kumwendea Mtawala wa Kimungu katika ibada, isingetuletea wokovu. Ni kwa njia ya Wakili Mkuu wake tu kwamba Mtawala wa Kimungu anatupa sisi njia ya kupatia wokovu kwenye uzima na furaha kamilifu katika taratibu mpya yenye baraka ambayo Mtawala wa Kimungu ameahidi. Ni lazima watu kila mahali wajue uhakika huu wa lazima sana.
2. Ni kwa sababu ya tendo gani la karibuni lililofanywa na ya Yerusalemu baraza hiyo ya hukumu ilihitaji kujua uhakika huo
2 Miaka 1900 iliyopita watu wenye vyeo vikuu kabisa vya kidini katika Yerusalemu walihitaji kujua uhakika huo. Watu hao ndio waliokuwamo katika baraza kuu ya hukumu ya nchi, inayoitwa Sánhedrin. Katika hukumu ambayo walikuwa wametoa majuma fulani yaliyotangulia, walikuwa wamemhukumia kufa mtu mwenye kutokeza ubishi mwingi, Yesu Kristo. Sasa walikuwa wamewaleta mbele yao wafuasi wakubwa kumi na wawili wa mtu huyo mwenye kutokeza ubishi. Katika kuhukumiwa Petro na wafuasi wengine kumi na mmoja waliiambia Baraza kwamba yule mtu ambaye walikuwa wamehukumia kufa alifanywa kuwa “Wakili Mkuu na Mwokozi” wa Mungu. Katika kujibu agizo la Baraza walisema hivi:
3. Katika kujibu agizo la Sánhedrin, wafuasi hao kumi na wawili wa mtu aliyehukumiwa walisema nini juu ya utii na Wakili Mkuu?
3 “Inatupasa kumtii Mungu kama mtawala kuliko wanadamu. Mungu wa babu zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mliua, mkamtundika juu ya mti. Mungu alimfanya huyu kuwa mkuu kama Wakili Mkuu na Mwokozi kwenye mkono wake wa kuume, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, na ndivyo na roho takatifu, ambayo Mungu amewapa wale wanaomtii yeye kama mtawala.”—Matendo 5:29-32, NW.
4. Yeye aliyefanywa mkuu ili awe Wakili Mkuu na Mwokozi alipaswa awape Waisraeli nini, na kulingana na agano gani la Mungu?
4 Acha baraza kuu ya Yerusalemu ipende au isipende, Yesu huyo aliyepigiliwa misumari alifufuka kutoka kwa wafu na kuwa hai, hata kwenye mkono wa kuume wa Mungu, na hivyo ana uwezo wa kutenda kama Wakili Mkuu na Mwokozi kwa Mtawala wa Kimungu, kwa ajili ya taifa la Israeli. “Wakili Mkuu na Mwokozi,” wa kufanya nini? “Awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.” Huu “msamaha wa dhambi” ulipaswa uwe kulingana na “agano jipya” ambalo Mtawala wa Kimungu alikuwa ameahidi kufanya pamoja na watu wake waliochaguliwa.—Yer. 31:31-34; Luka 22:20.
5. (a) Mbele ya kufa kwa Yesu, toba lilikuwa limehubiriwa kwa Israeli na nani? (b) Sasa ni maulizo gani yaliyokuwa yenye kuhusu juu ya toba na msamaha wa dhambi na uhusiano wa washiriki wa Sánhedrin kwa Mungu?
5 Baraza hiyo ya Yerusalemu ilijua kwamba wakati Yesu Kristo alipokuwa hajaonekana duniani, Yohana Mbatizaji alikuwa amehubiri hivi: “Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Halafu, Yohana Mbatizaji alipokwisha kufungwa, Yesu huyu ambaye Yohana alikuwa amebatiza alihubiri ujumbe ule ule, akisema: “Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” (Mt. 3:1, 2, 13-17; 4:12-17) Hii iliendelea hivyo mpaka kufa kwa Yesu chini ya uchochezi wa Baraza ya Yerusalemu. Je! sasa kulikuwako tofauti yo yote katika shauri la kutubu upande wa Israeli? Zilikuwa dhambi gani ambazo zilipaswa zisamehewe? Je! washiriki wa Baraza hawakupewa sababu ya kufikiri kwa maneno ya Simoni Petro aliyekuwa mbele yao? Sasa uhusiano wao na Mungu ulipata matokeo gani? Je! uhusiano huu ulikaa juu ya msingi ule ule kama mwanzoni? Acha tuone.
6. Yehova alionaje wajibu wa kukomboa watu wake Israeli katika Misri, na alifanya hivyo namna gani?
6 Taifa la Israeli lilitokea katika nchi ya Misri, wakati wa miaka 215 ya kukaa kwa muda kwa Yakobo (Israeli) pamoja na watoto wake huko. (Mwa. 49:28-33) Wakati fulani alipokwisha kufa waziri mkuu wa Misri Yusufu, mwana wa Yakobo, Waisraeli waliingizwa katika utumwa, na kulifanywa jaribu la kutaka kuangamiza taifa lote. Ndipo kwa wakati wa Mungu mwenyewe uliotabiriwa aliwatoa wazao hawa wa Yakobo (Israeli) “katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.” Hii ilikuwa wakati Mungu alipokuwa amekwisha kuwaagiza kufanya Chakula cha Jioni kipya, chakula cha jioni cha Kupitwa, Misri katika Nisani 14 wa mwaka wa 1513 B.C.E. Jioni ya siku hiyo mwana-kondoo wa Kupitwa alichinjwa na damu yake ilinyunyizwa juu ya miimo na vizingiti vya nyumba za Waisraeli, halafu aliokwa akiwa mzima na kuliwa ndani ya nyumba zilizofungwa zenye milango iliyotiwa damu. Mungu aliikubali dhabihu ya mwana-kondoo huyo wa Kupitwa na akawaokoa kutoka Misri walipokwisha kula chakula chao cha jioni cha dhabihu. Ilikuwa kana kwamba amewanunua kupitia kwa mwana-kondoo huyo wa Kupitwa aliyetolewa dhabihu. (Kut. 12:1 mpaka 13:18) Ndivyo taifa la Israeli walivyokuwa watu ambao “Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake, wawe watu wake mwenyewe.”—2 Sam. 7:23.
7, 8. (a) Katika Bahari ya Shamu, Mungu aliimarishaje zaidi uenyeji wake wa watu wa Israeli? (b) Yehova aliendelea kuingia katika nini pamoja na Waisraeli katika Mlima Sinai, na alimwambia Musa aseme nini kama shauri?
7 Chini ya uongozi wa nabii Musa, Mungu aliwaongoza Waisraeli waliokombolewa kwa usalama katika maji ya Bahari ya Shamu lakini nyuma yao akazamisha jeshi la Misri lililofuatia. (Kut. 14:1 mpaka 15:21) Kukombolewa huku kwa mwujiza kwa taifa la Israeli kuliweka uenyeji wa Mungu juu yao; kweli walikuwa mali yake. Katika mwezi wa tatu (Sivani) walipokwisha kutoka katika nchi ya Misri, Mungu aliwaleta chini ya Mlima Sinai katika Arabuni. Nabii Musa, kama mpatanishi kati ya Mungu na taifa la Israeli, alipanda juu ya Mlima Sinai (Horebu) apate kushughulika na Mungu kwa ajili ya watu hawa waliokombolewa. Sasa hatua zilichukuliwa ili kuanzisha agano, yaani, mkataba mzito, uliofanywa halali kati ya Mungu na watu hawa wa Israeli waliokombolewa. Angalia ambavyo Mungu alivyomwambia Musa awaambie watu:
8 “Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.”—Kut. 19:3-6.
9. Je! Mungu aliendelea kufanya juu ya msingi wa haki yake, ili awaingize Waisraeli katika agano takatifu pamoja na yeye, au alifanyaje?
9 Katika njia hiyo masharti ya agano yalisemwa waziwazi na kusudi la agano lilielezwa waziwazi, kutokeza “ufalme wa makuhani,” “taifa takatifu,” mali ya Mungu. Isikose kuangaliwa hapa kwamba Mungu hakulazimisha agano hili juu ya taifa la Israeli. Yeye hakusema hivi: ‘Mimi nimewakomboa ninyi kutoka katika utumwa katika Misri na tena nimewaokoa ninyi na maji ya Bahari ya Shamu, na kwa hiyo ninyi mu mali yangu kwa haki na kwa ununuzi. Ninaweza kuwafanyia ninavyotaka, na ninalosema linakuwa sheria na inawapasa ninyi kuitii.’ Pahali pake, lile ambalo Mungu alimwagiza Musa awaambie watu linaonyesha kwamba Mungu alitaka kujua kama watu wake waliokombolewa walitamani, walikuwa na nia, ya kuingia katika agano takatifu pamoja na yeye. Kuliko kulazimisha agano juu yao kwa njia ya kuamuru, ya kuonea, Mungu aliwangojea waonyeshe nia yao katika shauri hili. Bila nia yao, hakuna agano!
NIA ILIYOONYESHWA YA WATU WALIOKOMBOLEWA YANGOJEWA
10. Kwa sababu gani agano hilo lilitaka mpatanishi, na ni sababu gani ya kibinadamu ambayo Mungu alikubali katika shauri hili?
10 Hili lilipaswa liwe agano la washiriki wawili. Kwa kuwa lilipaswa liwe agano kati ya Mungu Mtakatifu Zaidi na viumbe vya kibinadamu visivyokamilika, vyenye dhambi vilivyokuwa vimerithi laana na mauti kutoka kwa Adamu na Hawa, agano hili lilitaka mpatanishi, ambaye Mungu alikubali kama mwenye haki kwa sababu ya imani, yaani, Musa mwana wa Amramu Mlawi. (Gal. 3:19, 20) Mungu, Mshiriki mmoja, alionyesha tamaa yake ya kuingia katika agano hilo, lakini sasa, ilikuwa nia gani ya mshiriki mwingine aliyekaribishwa aingie katika agano? Kufanywa rasmi kwa agano kati ya Mungu na Israeli kulingojea wonyesho wa nia ya mshiriki mdogo aliyekaribishwa. Kwa kadiri kama hii Mungu aliikubali nia ya kibinadamu.
11. Israeli alionyesha nia gani kwa agano lililoshauriwa, na mbele ya kuonyesha huko kwa Yehova, ni jambo gani ambalo Yehova hakueleza kwao?
11 Ni nia gani ambayo watu, waliowakilishwa hapa na wazee wao wa kitaifa, walichukua juu ya agano lililotolewa? Maandishi ya Biblia yanasema hivi: “Musa akaenda akawaita wazee wa watu, akawafunulia maneno hayo yote, [Yehova] aliyokuwa amemwagiza. Watu wote wakaitika pamoja wakasema, Hayo yote aliyoyasema [Yehova] tutayatenda. Naye Musa akamwambia [Yehova] maneno ya hao watu.” (Kut. 19:7, 8) Yehova Mungu alipokuwa hajapokea wonyesho huo wa nia ya watu, yeye hakusema Amri Kumi, sheria za msingi za agano la Torati lililoshauriwa kutoka juu ya Mlima Sinai.—Kut. 19:9 mpaka 20:22.
12. (a) Basi ni jambo gani lililokuwa juu ya watu kufanya juu ya agano? (b) Tendo hilo la Israeli kwa agano tutaliita nini, na ni usemi gani wenye kusimulia unaoonyeshwa katika Warumi 6:13?
12 Ilikuwa juu ya watu waonyeshe uhuru wao, ama kukubali ama kukataa shauri la kimungu. Ilikuwa juu yao kuamua kwa uhuru wa kuchagua ama kuwa ‘tunu kwa Yehova kuliko makabila yote ya watu’ ama kukataa kuwa hivyo kwa sababu ya masharti yaliyotolewa. Basi, watu hawa waliokombolewa walipoitikia kwa umoja shauri hilo la kimungu, “Hayo yote aliyoyasema [Yehova] tutayatenda,” au, kwa njia ile ile, “tutakuwa tukiyatenda,” walikuwa wakifanya nini? Katika maneno mengine tutaliitaje tendo lao? Je! ni kupita kadiri kusema kwamba walikuwa wakijiweka wenyewe chini ya sharti kwa Yehova Mungu kufanya mapenzi yake kama yalivyosemwa na Yeye? Je! inalingana na ambavyo mtume wa Kikristo Paulo alisema kwa kundi la Kikristo katika Rumi: “Jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki?” (Rum. 6:13, UV; AT) The New English Bible inatafsiri hili, ikisema: “Jiwekeni wenyewe kwa matumizi ya Mungu.” Revised Standard Version: “Jipeni wenyewe kwa Mungu.” A New Translation ya Moffatt: “Inawapasa mjiweke wakf wenyewe kwa Mungu.”
13, 14. (a) Kwa sababu gani Yehova alitoa kwao agano kuliko kulilazimisha juu ya Israeli, na, kwa kuitikia kwao, walikuwa wakifanya nini kweli? (b) Ni wakati gani walipotangaza tena kwa nguvu nia yao, na kwa njia hiyo wakawa nini kwa Yehova?
13 Yehova hakutumia ushawishi mwingi kwa Waisraeli, akisema: ‘Mimi nimewakomboa ninyi kutoka Misri na nimewaokoa ninyi katika Bahari ya Shamu. Tena, ninyi ni uzao wa asili wa Ibrahimu rafiki yangu. Kwa hiyo lazima mwingie katika agano hili pamoja na mimi.’ Kweli, ilikuwa kwa sababu hizo kwamba Mungu akatoa kwao uhusiano wa agano pamoja na yeye, naye aliweka tumaini lenye kuvutia mbele yao kwa kuingia katika agano. Lakini ilikuwa juu ya Waisraeli kuchagua kama watakuwa watu wa Yehova kama Mungu wao au sivyo. Kwa hiyo, waliposema: “Yote ambayo Yehova amesema sisi tutakuwa tukiyafanya,” walikuwa wakijiweka wenyewe wakf kwa Yehova wawe watu Wake, wafanye mapenzi Yake ambayo yalipaswa kuandikwa katika agano. Nyumaye, Amri Kumi zilipokwisha kutolewa halafu mpango wa sheria kwa Musa, agano liliimarishwa kwa damu ya wanyama wenye kuchinjwa. Na katika njia hiyo Waisraeli wakawa watu walio wakf wa Mungu katika agano ambalo ni la lazima pamoja na Yehova Mungu. Wakati huo, hata kwa kujua sana, watu walitangaza kwa nguvu tena kuazimia kwao kufanya mapenzi ya Yehova, kwa maana habari katika Kutoka 24:7, 8 inatuambia hivi:
14 “Kisha [Musa] akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena [Yehova] tutayatenda, nasi tutatii. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya [Yehova] pamoja nanyi katika maneno haya yote.”—Tazama tena Waebrania 9:18-20.
15. Agano hilo lilikuwa lenye kuendelea kwa muda gani, na lilikuwa la lazima juu ya nani?
15 Agano hilo, lililofanywa pamoja na washiriki hao wa watu waliokombolewa huko katika Mlima Sinai, halikuwa la lazima kwa wale waliokuwapo peke yao bali lilikuwa la lazima vile vile kwa wazao wao wa kimwili, wa asili. Lilikuwa “agano la milele.” (Law. 24:8) Hii iliwaweka wazao wao wote wa asili katika uhusiano wa agano pamoja na Mungu kwa muda ambao agano liliendelea. Kwa sababu hiyo Waisraeli wale waliozaliwa jangwani agano hilo lilipokwisha kufanywa katika Mlima Sinai walikuwa katika agano hilo pamoja na Mungu katika mwaka wa 40 wa mwisho wa kutanga-tanga kwao kwa lazima katika jangwa. Hivyo waliendelea kuwa watu au taifa lililo wakf.
16. Katika nyanda za Moabu, wengi walichagua wasikae katika uhusiano wa agano pamoja na Yehova namna gani?
16 Walakini, katika mwaka huo wa mwisho (1473 B.C.E.) maelfu ya washiriki wa taifa hilo hawakuchagua kuendelea katika uhusiano wa agano pamoja na Yehova. Walionyesha hili katika nyanda za Moabu. Katika masimulizi ya Musa ya hili tunasoma, katika Hesabu 25:1-5:
“Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. Ikawa Israeli kujiungamanisha [au, Israeli walijishirikisha wenyewe, AT; au, Israeli akajiunga mwenyewe, KS] na Baal-peori; hasira za [Yehova] zikawaka juu ya Israeli.
“Kisha [Yehova] akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie [Yehova] watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za [Yehova] ziwaondokee Israeli. Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha [waliojishirikisha wenyewe, AT; waliojiunga wenyewe, BS] na Baal-peori.”
17. (a) Ni wangapi waliofia huko kwa sababu ya kuvunja agano lao na Yehova? (b) Yehova katika Hosea 9:10, alisema nini juu ya kujiungamanisha wenyewe na Baal-peori?
17 Walikuwa watu 24,000 waliokufa kwa sababu ya kuvunja huku kwa ahadi yao kutenda “yote aliyoyanena [Yehova].” (Hes. 25:9; 1 Kor. 10:8) Zaidi ya miaka 700 iliyofuata Yehova alitaja tukio hili lenye kuchukiza sana, kwa njia ya nabii wake Hosea. Kwanza anasimulia namna taifa la Israeli lilivyokuwa lenye kutamanika kwake kisha anasimulia namna Waisraeli wengi walivyojifanya wenyewe kuwa karaha kwake. Yehova anasema hivi: “Mimi nalimkuta Israeli kama zabibu nyikani; nami naliwaona baba zenu kama matunda ya mtini yaliyoiva kwanza, wakati wake wa kwanza; lakini walikwenda Baal-Peori, wakajiweka wakfu kwa kitu cha aibu, wakawa chukizo kama kitu kile walichokipenda.” (Hos. 9:10) Tafsiri ya Biblia ya Moffatt inasema hivi: “Walijitoa wenyewe kwa Baali Mwovu sana.” (Vile vile ya Leeser) Kwa sababu Waisraeli hao walijitenga wenyewe kutoka kwa Yehova Mungu ili waende kwa mungu mwingine, Revised Standard Version inasema hivi: “Wao . . . walijiweka wenyewe wakfu kwa Baali.” (Vile vile American Standard Version; New American Bible; New English Bible)
18. (a) Tafsiri ya Jewish Publication Society ya Hosea 9:10 inaonyeshaje wazi kutokuaminika kwa tendo lao kwa Yehova? (b) Kutokuaminika kunaonyeshwaje wazi kukamatana na neno lile lile la Kiebrania katika Ezekieli 14:7, 8?
18 Waisraeli hao wasioaminika walikuwa wamejiweka wakf kwa Mungu mmoja aliye hai na wa kweli, lakini sasa wakajitenga wenyewe na Yeye ili wajitoe au wajiweke wenyewe wakf kwa Baali. Ili kuonyesha wazi tendo hilo lisilo la uaminifu, Biblia ya Jewish Publication Society inasema: “Walijitenga wenyewe kwenye kitu chenye aibu.” Kiarifa cha lazima cha Kiebrania hapa ni na·zarʹ, na kinatumiwa kukamatana na ambavyo Mnadhiri wa Kiyahudi alivyofanya alipojitenga mwenyewe kwa pekee kwa Mungu. (Hes. 6:1-8) Katika siku za nabii Ezekieli, punde kidogo mbele ya uharibifu wa kwanza wa Yerusalemu katika mwaka wa 607 B.C.E., walikuwako Waisraeli wengi waliotenda vivyo hivyo kwa kile ambacho Waisraeli wasioaminika walichofanya katika siku za Musa katika nyanda za Moabu. Kwa habari ya hao wasioaminika Yehova alimwambia nabii Ezekieli hivi:
“Kila mtu wa nyumba ya Israeli, au wa wageni wakaao katika Israeli, ajitengaye [na·zarʹ] nami, na kuvitwaa vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake . . . nitamkatilia mbali, asiwe kati ya watu wangu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi [Yehova].”—Eze. 14:7, 8.
19. (a) Je! kujiweka wakf kwa Waisraeli hao wasio waaminifu kwa Baal-peori kulitia wakf mwingine wo wote? (b) Pahali pa kusema juu ya kujitenga wenyewe wawe kwa Baal-peori, Hesabu 25:3 inasemaje waziwazi?
19 Hivyo usemi wenyewe unaonyesha kwamba Waisraeli hao wenye kujitenga kwanza walikuwa katika uhusiano wa agano pamoja na Yehova Mungu, uhusiano ambao katika huo babu zao walikuwa wamewaleta kwa kusema kwa mpatanishi Musa: “Hayo yote aliyoyanena [Yehova] tutayatenda, nasi tutatii.” (Kut. 24:7; 19:8) Lakini sasa, kwa kuacha agano na kwenda kwenye ibada ya sanamu, walikuwa wakivunja wakf wao kwa Yehova na kujiweka wenyewe wakf kwa kitu kinachoabudiwa kama sanamu. Pahali pa kusema juu ya kujitenga kwa Israeli mwenyewe kwenda kwa Baali, Hesabu 25:3 inasema waziwazi hivi: “Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori.” Hili limepaswa liwe onyo kwetu leo, ikiwa wo wote kati yetu wana uhusiano wo wote na Yehova Mungu. (1 Kor. 10:6, 11) Sisi hatutamani kufanya kosa lile lile lenye hatari. Ingemaanisha kutokuaminika au uasi juu ya utawala wa kimungu.
KUONYESHA NJIA YA AGANO JIPYA
20. (a) Kwa sababu gani agano hilo la kwanza halikuwa lisilo na makosa, na hivyo hii iliruhusu nini? (b) Agano jipya lilitabiriwa kupitia kwa nabii gani, na Musa alisema nini juu ya mpatanishi aliye bora?
20 Agano ambalo Yehova alifanya kupitia kwa Musa pamoja na watu walio wakf wa Israeli lilikuwa “agano la milele.” Agano hilo lililofanywa katika Mlima Sinai halikuwa lisilo na makosa, kwa sababu ya kutokukamilika kwa Waisraeli na mpatanishi wao Musa. Kwa hiyo liliacha nafasi kwa agano bora, agano jipya. Kwa hiyo Yehova Mungu alikusudia agano jipya, na pendeleo la kuingia katika agano hili la pili lilipaswa kutolewa kwa taifa la Israeli wa asili. Zaidi ya miaka 600 mbele ya agano hili jipya kufanywa kupitia kwa mpatanishi mpya, Yehova alilitabiri kupitia kwa nabii Yeremia katika karne ya saba mbele ya kuja kwa Mpatanishi huyo aliye bora. (Yer. 31:31-34; Ebr. 8:6-13) Kuja kwa Mpatanishi huyu aliye bora na mkubwa zaidi kulitabiriwa na nabii Musa, naye alisema kwamba mpatanishi huyu anayekuja angeinuliwa kutoka kati ya Waisraeli; yeye angekuwa Mwisraeli wa asili.—Kum. 18:15-19; Matendo 3:22, 23; 7:37, 38.
21. (a) Ni wakati gani, wapi na kwa tangazo gani mpatanishi huyu aliye bora alizaliwa? (b) Kwa sababu gani Yesu aliadhimisha Sikukuu ya Kupitwa ya Kiyahudi, na penye mwadhimisho wake wa mwisho, alijionyesha mwenyewe kuwa nini, na namna gani?
21 Katika mwaka wa 2 B.C.E. Mpatanishi huyo aliye bora alizaliwa, kama mzao wa Mfalme Daudi katika mji wa Daudi, Bethlehemu. Wakati uo huo yeye alikuwa Mwana wa Mungu na wakati wa kuzaliwa kwake malaika wa Mungu aliwatangazia wachungaji waliokuwa mashambani karibu na Bethlehemu: “Mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.” (Luka 2:10, 11) Akizaliwa na mama ya Kiyahudi, huyu aliyepaswa kuwa “Kristo Bwana” alikuwa Myahudi wa asili na chini ya Sheria ya agano ambalo Musa alikuwa amepatanisha kati ya Mungu na Israeli. Katika uhakikisho wa hili tunasoma, katika Wagalatia 4:4 hivi: “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria.” Akiwa chini ya sheria ya agano pamoja na Israeli, Yesu Kristo aliadhimisha chakula cha jioni cha Kupitwa. Penye mwadhimisho wake wa mwisho wa Kupitwa, katika mwaka wa 33 C.E., alijitaja mwenyewe kama akiwa Mpatanishi wa agano jipya lililoahidiwa. Namna gani? Sasa alianzisha kinachoitwa Chakula cha Bwana cha Jioni, na aliwapa mitume wake waaminifu kikombe cha divai akisema hivi: “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.” (Luka 22:20) Yesu alimwaga damu yake mwenyewe ili aimarishe agano hilo.
22. (a) Ni wakati gani Yesu alipochukua wajibu wa kuwa mpatanishi wa agano jipya? (b) Kwa sababu gani Yohana alikataa kwanza kumbatiza Yesu?
22 Walakini, kama nabii Musa, Bwana Yesu alipaswa achukue wajibu wa kuwa yule Mpatanishi wa agano jipya. Ni wakati gani alipochukua wajibu wa kufanya hivi? Wakati wa ubatizo wake katika Mto Yordani. Wakati wa umri wa miaka 30 alikiacha kiwanda chake cha seremala katika Nazareti akamwendea Yohana Mbatizaji ili azamishwe katika maji. Hii ilikuwa namna mpya ya ubatizo kwa Yohana kufanya. Mpaka wakati huo, kama tunavyosoma katika Marko 1:4, “Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.” (Luka 3:3) Lakini Yesu Mwana wa Mungu hakuja kwa Yohana Mbatizaji ili abatizwe kwa mfano wa toba la msamaha wa dhambi. Yesu alikuwa mkamilifu na asiye na dhambi. (Ebr. 7:26) Yeye hakumjia Yohana akiwa na dhamiri mbaya na akataka kuwa na “ombi linalofanywa kwa Mungu kwa dhamiri njema.” (1 Pet. 3:21, NW) Yohana alijua hili, na ndiyo sababu tunasoma kwamba Yohana “alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?” Yesu alijibu namna gani?
23. Yesu alimjibu Yohana nini, na kwa sababu gani alisema juu ya “itupasavyo kuitimiza haki yote” hata ijapokuwa alikuwa ameshika Torati?
23 “Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” (Mt. 3:13-15) Yesu alimaanisha nini kwa kusema hivyo? Kama Myahudi asili, ilimpasa aishike sheria ya agano la Musa kwa ukamilifu. Siku zilizofuata katika Mahubiri yake juu ya Mlima alisema juu ya hili: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.” (Mt. 5:17) Bila shaka, agano la Torati na Israeli yalikuwa mapenzi ya Mungu, lakini Yesu alikuwa amekuwa akitimiza mapenzi ya Mungu katika neno hilo katika maisha yake yote ya kidunia mpaka wakati wa kubatizwa kwake. Hivyo maneno ya Yesu, “haki yote,” yalimaanisha jambo fulani lililokuwa zaidi ya agano la Torati, lakini jambo fulani ambalo lingekuwa katika utimizo wa sehemu za mfano za agano la Torati. Hii ilikuwa ndiyo “haki yote,” maana yalikuwa mapenzi ya Mungu kwake kutimiza haya. Hivyo hili ndilo jambo ambalo alichukua wajibu kulifanya wakati wa kubatizwa kwake.
24. Kulingana na Waebrania 10:5-10, ni unabii gani ambao Yesu alikuwa akitimiza kwa kujitoa mwenyewe kwa ubatizo?
24 Kwa kujitoa mwenyewe kwa ubatizo, kwa kweli Yesu aliyatimiza “manabii,” kama alivyosema. Mtume Paulo anaonyesha ni unabii gani ambao Yesu alitimiza, katika Waebrania 10:5-10, ambapo tunasoma juu ya Yesu wakati wa kuja kwake kwa ubatizo: “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari; sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu. . . . Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.” Kwa njia hiyo Yesu alikuwa akiitimiza Zaburi 40:6-8. “Mapenzi” ya Mungu yalimtaka Yesu ajitoe mwenyewe dhabihu, “mwili” wake.
25. (a) Basi, ubatizo wa maji wa Yesu ulikuwa mfano wa nini? (b) Yesu alikuwa amekwisha kujiweka wakf na kukombolewa namna gani?
25 Kwa kuwa unabii ulitaka hili, basi, Yesu angalikuwa na dhamiri mbaya kama asingalikuja kufanya mapenzi ya pekee ya Mungu na kwa hiyo kujionyesha mwenyewe kwa Yohana ili abatizwe. Ni wazi kwamba kubatizwa kwa Yesu kulikuwa mfano. Ubatizo wake haukuwa “wa toba liletalo ondoleo la dhambi.” Ulikuwa mfano wa kuja kwa Yesu au kujitoa mwenyewe afanye mapenzi ya Mungu, “mapenzi” ya kimungu yaliyotia kutolewa kwa mwili wa Yesu katika dhabihu mara moja tu. Kama Myahudi asili alikuwa amekwisha kuwa chini ya sheria ya Musa na alikuwa mshiriki wa taifa peke yake duniani ambalo wakati huo lilijiweka wakf kwa Mungu, kufanya “yote aliyoyanena [Yehova].” Tena, kama mzaliwa wa kwanza wa Mariamu, ambaye mume wake Yusufu alilea kama mwana wake mwenyewe mzaliwa wa kwanza, Yesu alitakaswa kwa Mungu na akawa wake. (Kut. 13:1, 2) Kwa sababu hii ilimpasa Yesu akombolewe na Yusufu na Mariamu ili kumruhusu afanye kazi ya kimwili. (Hes. 3:13-51; 18:14-16) Hivyo ubatizo wa Yesu ulifananisha, si kujiweka mwenyewe wakf kwa Mungu, bali kujitoa kwake mwenyewe afanye mapenzi ya Mungu hata kutoa dhabihu.
26. (a) Mungu alionyeshaje ukubali wake wa kujitoa kwa Yesu mwenyewe? (b) Ni kwa kadiri gani Yesu alitimiza “mapenzi” hayo ya kimungu katika mwili?
26 Yehova Mungu alifunua kwamba alikubali kujitoa kwa Mwana wake Yesu kwa kumimina roho yake takatifu juu ya Yesu aliyebatizwa na akaacha sauti Yake isikiwe kutoka mbinguni, ikisema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” (Mt. 3:16, 17) Kutoka hapo Yohana Mbatizaji alimtangaza Yesu aliyetiwa mafuta kama “Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” (Yohana 1:28-36; Matendo 10:37, 38) Yesu alitimiza mapenzi ya Mungu mpaka mwisho wa siku zake katika mwili duniani. Wakati wa usiku wake wa mwisho duniani katika mwili wa asili wa kibinadamu alisali kwa Mungu na kusema: “Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.” (Mt. 26:39-44) Alasiri iliyofuata, kama saa tisa hivi, wakati Yesu alipokuwa akining’inia penye mti wa mateso, kama Yohana 19:30 anavyotuambia, Yesu “alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.” Ndivyo, kulingana na mapenzi ya Mungu, mwili wa Yesu ulivyotolewa mara moja tu.
27. (a) Yesu Kristo alikuwa na ufufuo wa namna gani, na kwa sababu gani? (b) Na wakati huo aliwapataje wanadamu wote, kwa tumaini gani kwa wafu?
27 Kupatana na kutoa huku kwa dhabihu ya mwili wake mkamilifu wa kibinadamu, Yesu Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu siku ya tatu, si katika mwili na damu na nyama, bali katika mwili wa kiroho. (1 Pet. 3:18; 1 Kor. 15:42-45) Siku ya 40 tangu kufufuka kwake, Yesu alipaa mbinguni na huko akatoa kwa Mungu bei au wema wa dhabihu yake ya kibinadamu kwa ajili ya wanadamu wote. Yeye alikuwa amesema duniani kwamba alikuwa amekuja “kuhudumu na kutoa nafsi yake ukombozi badala ya wengi.” (Mt. 20:28, NW) Mtume Paulo anasema juu ya Yesu kama akiisha “kupatwa na mauti, ili kwa fadhili zisizostahili za Mungu apate kumwonjea kila mtu mauti.” Tena Paulo anasema juu ya “mwanadamu, Kristo Yesu, ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi unaolingana kwa ajili ya wote.” (Ebr. 2:9; 1 Tim. 2:5, 6, NW) Ndivyo kwa kutoa kwa Mungu bei ya uhai wa dhabihu yake ya kibinadamu Yesu Kristo alivyowakomboa wanadamu wote, akawanunua, hata bila kumwomba kufanya hivyo. Kwa sababu hii, chini ya ufalme wake wa kimbinguni kutakuwako “ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.” (Matendo 24:15) Yesu Kristo akawapata wote.
28. (a) Ndivyo Yesu Kristo aliyefufuka akawa nini kwa habari ya wokovu wa wanadamu? (b) Vile vile yeye anatumikia kama Wakili Mkuu wa jambo gani kubwa zaidi?
28 Katika njia hii, kulingana na “mapenzi” ya kimungu, Yesu Kristo Mwana wa Mungu akawa Wakili Mkuu wa wokovu kwa wanadamu wote. Hivi ndivyo itupasavyo kufahamu kutokana na Waebrania 2:9, 10, NW, inayosomwa hivi: “Tunamwona Yesu, ambaye amefanywa mdogo zaidi kuliko malaika, amevikwa taji yenye utukufu na heshima kwa sababu ya kwisha kupatwa na mauti, ili kwa fadhili zisizostahili za Mungu apate kumwonjea kila mtu mauti. Kwa maana ilifaa kwa mmoja ambaye kwa ajili yake vitu vyote viko na kupitia kwa yeye vitu vyote viko, katika kuwaleta wana wengi kwenye utukufu, kumfanya Wakili Mkuu wa wokovu wao kuwa mkamilifu kupitia kwa mateso.” Na katika Waebrania 5:9, 10: “Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.” Huyu alijionyesha mwenyewe kustahili kutumikia kama Wakili Mkuu wa Utawala wa Kimungu.
[Picha katika ukurasa wa 221]
Ijapokuwa watu wa Israeli walikuwa wa Yehova, yeye hakulazimisha agano lake juu yao bali aliwangojea waonyeshe tamaa yao wenyewe katika jambo hili