Mungu Alifufua Taifa
Makala hii ni ya kutumia kwa mafunzo ya kitabu ya kundi
KATIKA mwaka wa 607 B.C.E. Yerusalemu uliharibiwa na hesabu kubwa ya Wayahudi waliookoka wakakokotwa kuingia uhamishoni wa Kibabeli. Taifa la Kiyahudi lilikaribia kufa kabisa. Wingi wa wahamishwa hawakuwa na tumaini la kuishi tena kama taifa lililoungana katika nchi yao waliyopewa na Mungu. Nchi ya Babeli ilielekea kuwa mahali pa kuzikia taifa lao. Je! Yehova Mungu angelifufua taifa lililokufa?
2. Kwa sababu gani ufufuo wa taifa usingekuwa jambo gumu mno kwa Yehova Mungu?
2 Ufufuo huo haungekuwa mgumu mno Mungu Mwenye Nguvu Zote asiweze kuufanya. Hapo awali alikuwa amewapa uwezo manabii waaminifu Eliya na Elisha wa kuwafufua wafu kwenye uzima. (1 Fal. 17:17-24; 2 Fal. 4:32-37; 8:4, 5; Ebr. 11:35) Kwa hiyo si ajabu kwamba Yehova Mungu, katika njozi, alimfunulia nabii Ezekieli kwamba angelifufua taifa lililokufa.
3-5. Yehova alimwonyeshaje Ezekieli kwamba lilikuwa kusudi lake kulifufua taifa lililokufa la Israeli?
3 Nyuma ya kuja chini ya utendaji wa roho ya Mungu, Ezekieli alijikuta mwenyewe katikati ya bonde lililojaa mifupa mikavu ya kibinadamu. Halafu Ezekieli akasikia sauti, “Mwanadamu, je! mifupa hii yaweza kuishi?” “Ee Bwana [Yehova],” akajibu Ezekieli, “wajua wewe.” Haukupita muda mwingi mbele ya Ezekieli naye kulijua jibu la ulizo hilo. Aliamriwa kusema na mifupa hiyo kwa maneno haya: “Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la [Yehova]. Bwana [Yehova] aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi [Yehova].”—Eze. 37:1-6.
4 Mwujiza! “Palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.” Mifupa ile mikavu ilivikwa tena mishipa, nyama na ngozi. Hili ni jambo lisiloweza kufanywa na wanasayansi hata katika karne ya 20. Ijapokuwa wanajua namna ya kuunganisha mifupa ya kibinadamu, wao hawawezi kuweka mishipa wala nyama juu ya mifupa hiyo iliyounganishwa tena na viungo vya lazima ndani yake. Lakini Yehova Mungu, katika njozi, alijifananisha mwenyewe kama akilifanya jambo hili lisilowezekana kwa njia ya mwanadamu.—Eze. 37:7, 8.
5 Kisha likaja jambo lenye kustaajabisha kupita yote. Kama alivyoongozwa kwa kimungu, Ezekieli aliuamuru upepo uvume juu ya miili hiyo ya kibinadamu iliyounganishwa tena. Kwa hiyo “pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.”—Eze. 37:9, 10.
6. Nini kinachoonyeshwa na uhakika wa kwamba waliofufuliwa wanaitwa “jeshi kubwa mno”?
6 Lo! hili lilikuwa jambo la kuogofisha kama nini kwa Ezekieli! Kama “jeshi kubwa mno,” hao waliofufuliwa hawakuwa watu dhaifu. Walikuwa watu wenye uwezo waliostahili utumishi wa kijeshi. Hivyo Ezekieli alipendelewa kuuona ufufuo wa taifa la Kiyahudi kwa njia ya njozi. Hii inahakikishwa na masimulizi aliyopewa mara tu nyuma ya hapo. Twasoma:
7, 8. (a) Wayahudi waliomo utumwani waliionaje hali yao? (b) Utendaji wa roho ya Mungu juu ya wahamishwa wa Kiyahudi ulitimiza nini? (c) Nani wangetiwa ndani katika “nyumba yote ya Israeli” ambayo ilipaswa irudishwe?
7 “Mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa. Basi tabiri, uwaambie, Bwana [Yehova] asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi [Yehova], nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, [Yehova], nimesema hayo, na kuyatimiza, asema [Yehova].”—Eze. 37:11-14.
8 Wayahudi wahamishwa, walioelekea kutokuwa na tumaini wakati huo, walipaswa wafufuliwe wakiwa na tumaini jipya lenye msingi wa neno kamilifu la Yehova. Kama mnenaji wa Yehova, Ezekieli, kwa kutabiri kwake, alipaswa ashiriki katika kuwafurahisha Waisraeli hao wenye huzuni kwa tumaini la kurudishwa kwenye nchi yao waipendao, mamia ya maili kutoka huko. Lakini Yehova Ndiye ambaye, kwa kuitia roho takatifu yake katika Waisraeli wenye kutubu, kwa kweli angewasimamia na kuwafanya wazima wakiwa na shauku na nia ya kurudishwa kwenye nchi yao wenyewe. Yeye Ndiye ambaye angewafungulia njia kwa mwujiza wayaache “makaburi” yao katika nchi ya Babeli na kuirudia “nchi ya Israeli.” “Nyumba yote ya Israeli” ilipaswa ishiriki katika hili, kutia na washiriki wa kabila kumi zilizokuwa zimehamishwa mapema zaidi na Waashuri.
9. Nini kilichotukia katika mwaka wa 537 B.C.E. kwa utimizo wa njozi ya Ezekieli ya bonde lililojaa mifupa mikavu?
9 Njozi ya unabii ilitimizwa. Katika mwaka wa 537 B.C.E., Mfalme Koreshi mshindi wa Babeli alilitoa tangazo lake akiwafungua Waisraeli wauache uhamisho wao katika Babeli na kuurudia Yerusalemu wakalijenge upya hekalu la Mungu wao. Koreshi alimpa Yehova daraka la hili. Tangazo, kama lilivyowekwa katika 2 Mambo ya Nyakati (Siku) 36:23, linasema hivi:
10-12. Koreshi alimhesabia nani kufunguliwa kwa Wayahudi, na kusudi la kufunguliwa huku lilikuwa nini?
10 “Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; [Yehova], Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, [Yehova], Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.”
11 Kusudi la ‘kukwea’ huko kwenda Yerusalemu linaonyeshwa katika maelezo zaidi yaliyotolewa katika kitabu cha Ezra:
12 “Na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya [Yehova], Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu. Na mtu awaye yote aliyesalia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu.”—Ezra 1:3, 4.
13. Nini lilikuwa itikio la Wayahudi kwa tangazo la Koreshi?
13 Koreshi Mkuu alipomshirikisha Yehova na tukio hili lisilotazamiwa kwa njia hiyo, Waisraeli walijua kwamba Yehova Ndiye aliyekuwa na daraka la kuyafungua makaburi yao katika Babeli na kuwatoa nje wakiwa hai kwa ajili ya utendaji zaidi katika utumishi wake na ibada katika nchi yao iliyoachwa ukiwa. Wakisaidiwa na Waisraeli wenye huruma ambao wasingeweza kuiacha Babeli kwa kufaa wakati huo, Waisraeli 42,360 waliiitikia roho ya Yehova iliyomiminwa nao wakaifurahia nafasi ya kuvijaza vilima, milima na mabonde ya nchi ya Israeli na watu, kuujenga Yerusalemu na hekalu lake upya na kuirudisha ibada ya Yehova humo. Zaidi ya watumwa 7,500 na waimbaji wastadi wasio wa Kiisraeli walilikubali pendeleo la kuambatana nao kwenye utumishi wenye umoja wa Yehova. (Ezra 2:64-67) Hili lilikuwa kama “jeshi kubwa mno” kweli kweli.—Eze. 37:10.
UFUFUO WA KISASA
14. Njozi ya bonde lililojaa mifupa mikavu na vile vile utimizo wayo ilikuwa unabii wa nini?
14 Utimizo wa kihistoria wa njozi ya Ezekieli ya bonde lililojaa mifupa mikavu ulikuwa wa unabii kama njozi yenyewe. Utimizo huu wa siku zijazo unaonyeshwa katika kitabu cha Ufunuo, kilichoandikwa zaidi ya karne saba nyuma ya njozi ya Ezekieli. Humo kufufuliwa kwa Israeli wa kiroho kunaonyeshwa kama ifuatavyo:
15, 16. Ufunuo 11:7-12 unafananishaje kufufuliwa kwa Israeli wa kiroho?
15 “Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa. Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
16 “Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama. Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.”—Ufu. 11:7-12.
17. Ufunuo 11:7-12 na njozi ya bonde lililojaa mifupa mikavu ulitimizwaje kwa Israeli wa kiroho?
17 Katika utimizo wa kisasa wa njozi hii ya unabii mabaki ya Waisraeli wa kiroho wa Kikristo waliuawa, kwa habari ya kazi yao ya kutabiri na kutoa ushuhuda waziwazi na kwa uhuru. Hii ilitukia wakati wa upeo wa mateso ya mataifa yote juu yao katika mwaka wa mwisho wa Vita ya Kwanza ya Ulimwengu. Waliingia katika hali ya kiroho kama ile ya mifupa mikavu iliyoonwa na Ezekieli katika bonde, katika Babeli. (Mwa. 11:2-9) Kuendelea kwao kuwamo katika hali hii kulionyeshwa kama kwa siku tatu u nusu, muda unaotosha kwa maiti kukauka. Lakini, katika masika ya mwaka uliofuata, 1919 C.E., “roho ya uhai itokayo kwa Mungu” iliwaingia nayo ikawafufua kwenye utendaji wenye nguvu wa waziwazi tena katika kuihubiri “habari njema ya ufalme” kwa mataifa yote. (Mt. 24:14) ‘Kupanda mbinguni katika wingu’ kulionyesha kwamba walitengwa kwa kidini na “mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya Sodoma, na Misri” (Yerusalemu aliyefananishwa au Kristendomu, mshiriki mkubwa wa kidini wa Babeli Mkuu, milki ya ulimwengu ya dini ya uongo). Wakaja kujua kwa wazi sana kwamba Yehova alikuwa ameyafungua “makaburi” yao katika Babeli Mkuu na akawatoa humo wakiwa hai kwa kiroho, akiwarudisha kwenye makao yao ya kiroho yanayofaa.
18. Ufufuo wa Israeli wa asili na wa kiroho vile vile unalihakikishaje tumaini la ufufuo?
18 Alilofanya Yehova Mungu katika kuwafufua Israeli wa asili na wa kiroho vile vile linaonyesha kwa nguvu kwamba ahadi zake ni za kutegemeka. Vile vile inafaa iangaliwe kwamba Waebrania wa kale, akiwamo babu ya Waisraeli, Ibrahimu, waliamini katika ufufuo wa wafu. Kwa habari ya imani ya Ibrahimu katika uwezo wa Yehova wa kufufua vilivyokufa, twasoma hivi: “[Ibrahimu] aliye baba yetu sisi sote; (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.” (Rum. 4:16, 17) Ijapokuwa haipaswi ionwe kama inaufananisha ufufuo wa wafu wa kibinadamu, njozi ya Ezekieli ya bonde lililojaa mifupa mikavu inapatana na imani katika ufufuo. Kwa hiyo utimizo wa njozi unatoa uhakika zaidi wa tumaini la ufufuo.
—Kutoka Kitabu “The Nations Shall Know that I Am Jehovah”—How?
1. Nyuma ya uharibifu wa Yerusalemu katika mwaka wa 607 hali ya Wayahudi kama taifa ilikuwa nini?