Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 11/15 kur. 527-528
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Je, Wakumbuka?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Jenga Itibari Katika Yehova kwa Kujifunza Neno Lake kwa Bidii-Endelevu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 11/15 kur. 527-528

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Maoni ya mashahidi wa Yehova ni nini juu ya kazi ya kuamua kesi za kortini?​—U.S.A.

Mashahidi wa Yehova wanakubali kwamba jambo ambalo watu wanafanya juu ya kuamua kesi za kortini ni shauri la kipekee, linaloongozwa na ambavyo dhamiri inasema.

Kwa kadiri inavyowapasa, mashahidi wa Yehova kwa desturi hawajioni kwamba imewapasa waketi kama mahakimu wa watu wengine. Wakati alipotolewa nafasi ya kuamua kesi, Mfano wao Bwana Yesu Kristo aliikataa, akisema: “Ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?” (Luka 12:14) Mtume Paulo alitokeza maulizo yanayofanana na hili katika barua yake kwa Wakorintho: “Yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani [ya kundi la Kikristo]? Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu.”​—1 Kor. 5:12, 13.

Halafu, tena, watu wengi wanaotumikia kama waamuzi wa kesi hawataki waongozwe na sheria za Neno la Mungu katika kufikia uamuzi. Waamuzi wengine wametafuta habari kwa kupiga falaki (kuagua kwa nyota), wamefanya upendeleo na kuamua isivyo haki au wamekazwa na wengine katika kutoa uamuzi. Hivyo kuna hatari ya kuwa mshiriki wa kupotoa haki. Wakati uhai wa mshtakiwa unapotiwa ndani, hii ingeweza kumaanisha kujiletea hatia ya damu. Ndivyo inavyoweza kuonwa sababu gani kutumikia kama mwamuzi wa kesi za kortini kunavyoweza kuongoza kwenye kupingana kukubwa kwa dhamiri.

Matakwa ya halali ya kufanya kazi ya kuamua kesi na mipango ya kuachiliwa inatofautiana mahali na mahali. Katika United States, huenda hali katika tarafa moja ikawa tofauti sana na ile iliyomo katika tarafa nyingine. Mara nyingine kueleza maoni yako kwa karani wa korti au kwa hakimu huenda kukaondolesha jina lako katika orodha ya wale wanaotazamiwa kuwa waamuzi. Kwa kweli, maoni ya Korti katika West Virginia, Minnesota na Washington yametegemeza haki ya mtu kukataa kazi ya kuamua kesi kwa sababu za kidini. Na katika tarafa ya Colorado watu ambao kwa hati za vithibitisho wanaweza kuonyesha kwamba wao ni mashahidi wa Yehova wanaachiliwa wasifanye kazi ya kuamua kesi.

Walakini, maachilio hayaruhusiwi kila mahali. Ikiwa mtu hawezi kuachiliwa wakati anapotakiwa afanye kazi ya kuamua kesi hata akiisha kueleza mambo kwa hakimu, hata hivyo, anaweza kueleza maoni yake ya dhamiri juu ya kesi hiyo wakati anapoulizwa na wanasheria mbele ya kuanza hukumu. Ikiwa maoni yake ya dhamiri hayakubaliwi kama yenye kumwondoa katika kazi ya kuamua, Mkristo anaweza kuona kwamba inampasa akatae kutumikia ili asiihalifu dhamiri yake. Ikiwa hivyo imempasa ajitayarishe kupokea matokeo yo yote ambayo huenda yakatokea kwa sababu ya kuamua kwake.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki