Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 7/15 kur. 315-318
  • Ahadi Inaweza Kuwa na Ubora Kadiri Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ahadi Inaweza Kuwa na Ubora Kadiri Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KUVUNJA AGANO KWA SEDEKIA
  • HAKUNA KUOKOKA ADHABU
  • YEYE AMBAYE ATAWATENDA WAVUNJAJI WA KUKUSUDIA WA AHADI
  • Yerusalemu Laharibiwa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Mtumikie “Mfalme wa Mataifa” Ukaokoke
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Yehova Achomoa Upanga Wake Kutoka Ala!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Je, Unatimiza Ahadi Zako?
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2017
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 7/15 kur. 315-318

Ahadi Inaweza Kuwa na Ubora Kadiri Gani?

Makala hii ni ya kutumia kwa mafunzo ya kitabu ya kundi

1, 2. (a) Nia ya wengi leo ni nini juu ya ahadi? (b) Yehova anaonaje kuvunja kwa makusudi ahadi?

HATA siku moja haipiti pasipo mamilioni ya watu kukata tamaa, na hata kukasirishwa na ahadi zilizovunjwa. Maagano, mikataba ya kukodisha na mapatano mengine hayatimizwi. Miadi haitimizwi. Zawadi zilizoahidiwa na huduma vinasahauliwa. Uchumba wa ndoa unavunjwa. Nadhiri za ndoa zinasukumwa kando watu mmoja mmoja wanapotenganishwa kihalali na kupewa talaka kwa sababu zisizo na maana. Mara kwa mara ahadi za wanasiasa zinakuwa maneno matupu. Tena, ahadi nyingi ni za udanganyifu kwa makusudi.

2 Matendo ya watu wengi yanaonyesha kwamba ahadi haina maana kubwa. Hawapendezwi sana juu ya dhara linaloweza kuletwa na ahadi iliyovunjwa. Hata hivyo, watu wa namna hiyo wawe wanataka kujua au wawe hawataki, wana wajibu fulani kwa Yeye ambaye hakushindwa kutimiza ahadi wakati wo wote. Yeye huyo ni Muumba wa mwanadamu, Yehova Mungu. Yeye haoni kufanya ahadi na kuzivunja kama jambo dogo tu, zaidi tendo lenyewe linapokuwa la makusudi na la kudhuru kwa wazi. Halafu, tena, ikiwa jina lake linashirikishwa na ahadi fulani, hataruhusu jina lake livunjiwe heshima kwa kutotimizwa kwa ahadi hiyo. Chukua kisa cha Mfalme wa Kiyahudi Sedekia kama mfano.

KUVUNJA AGANO KWA SEDEKIA

3. Sedekia na Wayahudi wengine wakuu walijiweka wenyewe chini ya wajibu wa kufanya nini kwa Mfalme Nebukadreza?

3 Katika mwaka wa 617 B.C.E. mpwa wa Sedekia, Mfalme Yekonia, pamoja na watu wengine wakuu na washirika wa jamaa ya kifalme, alichukuliwa mateka Babeli. Wakati huo mfalme wa Babeli, Nebukadreza, alimweka Sedekia juu ya kiti cha enzi cha Yerusalemu na akamfanya aahidi, kwa kiapo kwa jina la Yehova, kwamba angekuwa mfalme-raia mwaminifu. Wakuu vile vile waliapa kuwa raia waaminifu. (Eze. 17:13, 14; 21:23) Je! Yehova aliziona ahadi hizi zilizokuwa za lazima kwa kuapa kama zisizo na maana kubwa?

4, 5. (a) Nia ya Wayahudi ilikuwa nini juu ya ahadi zao zilizokuwa za lazima kwa kuapa? (b) Yehova alionaje kuvunja kwa kiapo ambacho Sedekia aliapa kwa jina lake Yeye?

4 Kunao Wayahudi waliofikiri kwamba haikuwa kitu kwa Yehova kama wangevunja ahadi zao za lazima kwa kuapa. Walipendelea kumwasi mfalme wa Babeli na kumtegemea Farao wa Misri kwa tegemezo. Walimtia moyo Sedekia kufanya hivi. Akisema kwa njia ya unabii juu ya uasi uliotendwa Mfalme Nebukadreza, Yehova alitangaza:

5 “[Sedekia] alimwasi kwa kupeleka wajumbe huko Misri, wampe farasi na watu wengi. Je! [Sedekia] atafanikiwa? afanyaye mambo hayo ataokoka? atalivunja agano, kisha akaokoka? Kama mimi niishivyo, asema Bwana [Yehova], hakika mahali pale akaapo mfalme [Nebukadreza] aliyemmilikisha, ambaye [Sedekia] alikidharau kiapo chake, na kulivunja agano lake, ndipo atakapokufa pamoja naye kati ya Babeli. Wala Farao na jeshi lake kubwa, na kusanyiko lake kuu la watu, hawatamfaa kitu vitani, watakapofanya maboma, na kujenga ngome, ili kukatilia mbali watu wengi. Kwa maana [Sedekia] amekidharau kiapo kwa kulivunja agano; na tazama, ametia mkono wake [kwa kiapo cha kutimiza agano], na pamoja na hayo ameyatenda mambo hayo yote; hataokoka.”​—Eze. 17:15-18.

HAKUNA KUOKOKA ADHABU

6. Kutokana na hili ilikuwako sababu yo yote kutazamia kwamba Sedekia asingepata adhabu?

6 Hivyo Yehova alitia mkazo kwamba hangekubaliana na kuvunja kiapo kwa Sedekia na hangemlinda na matokeo machungu ambayo yangefuata. Alisema mbeleni kwamba Mfalme Nebukadreza hangesahau uasi wa Sedekia lakini angeuelekea Yerusalemu kwa vita. Hii ingekuwa kulingana na kusudi la Yehova kumtumia Mfalme Nebukadreza na majeshi yake kama “upanga” wa kuadhibu waasi wenye kuvunja kiapo waliolitumia jina la Yehova bure.

7, 8. (a) Mfalme Nebukadreza alipaswa kuamua nini alipokuwa akielekeza majeshi yake kuingia Palestina? (b) Alifanya nini kuhakikisha huu ungekuwa ndio uamuzi unaofaa?

7 Alipokuwa akija kwenye nchi ya Palestina kutoka kaskazini, Nebukadreza, akiliongoza jeshi lake, alifikia njia panda. Kwa hiyo alitaka uongozi katika kufanya uamuzi kwa habari ya njia anayopaswa kuliongoza jeshi lake. Tawi moja la njia hii panda lilielekeza kwenye mji mkuu wa Waamoni Raba na lile jingine kwenye mji wenye ngome imara zaidi wa Yerusalemu. Ulizo lilikuwa, Je! kwanza anapaswa kuushambulia Raba na kisha, nyuma ya majeshi yake kufurahishwa na kuuteka mji huo, aendelee na mazingiwa yaliyo magumu zaidi ya Yerusalemu? Ili kuhakikisha kwamba uamuzi wake ungefaa, Nebukadreza alitumia njia tatu za uaguzi. Yehova Mungu alimfunulia hili nabii wake Ezekieli:

8 “Tena, mwanadamu, ujiwekee njia mbili, upanga wa mfalme wa Babeli upate kuja; hizo mbili zitatoka katika nchi moja; ukaandike mahali, upaandike penye kichwa cha njia iendayo mjini. Utaagiza njia, upanga upate kufikilia Raba wa wana wa Amoni, na kufikilia Yuda katika Yerusalemu, wenye maboma. Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale [mmoja ukionyesha kwa Raba na ule mwingine kwa Yerusalemu, itolewe katika chombo nyuma ya kutikiswa]. Akaziuliza terafi, akayatazama maini [ya mnyama aliyepatwa na kuchinjwa]. Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome.”​—Eze. 21:19-22.

9. Ni nani kwa kweli aliyekuwa akiongoza mambo kwa werevu ili kwamba Nebukadreza aje kuushambulia Yerusalemu kwanza?

9 Alichotoa Mfalme Nebukadreza kwa mkono wake wa kuume ndilo chaguo lililopendelewa, kuonyesha mwendo wenye bahati zaidi. Yehova Mungu alihakikisha kwamba chaguo hili, kwa kupatana na mapenzi yake, lingemwelekeza mfalme wa Babeli kuushambulia Yerusalemu kwanza. Hii ilimaanisha kuuletea Yerusalemu vifaa vyote vya Kibabeli vya kuzingira kabisa na kutumia vyombo vyote vya kuuzingira mji wenye ngome imara.

10. (a) Itikio la Wayahudi lilikuwa nini kwa matokeo yaliyokuwa yamesemwa mbeleni ya uaguzi wa Nebukadreza, na kwa sababu gani? (b) Wayahudi hao walishindwa kukumbuka nini, na jambo gani lilitukia?

10 Unabii huu ukionyesha mapema matokeo ya uaguzi wa Nebukadreza ulisikika kama “uongo” kwa wakazi wa Yuda na Yerusalemu. Waliona kwamba mfalme wa Babeli hangetamani kupaelekea mahali penye ngome imara sana kama Yerusalemu. Waliona kwamba hangeweza hata kidogo kuuteka mji kama huo wenye kuta imara sana. Vile vile waliona kwamba uwezo wa majeshi ya Misri ungeizuia jitihada yo yote ya kijeshi iliyofanywa kuwashambulia. Walichoshindwa kukumbuka Wayahudi wenye matumaini ya kupita kadiri ni kwamba kuvunja kwao kiapo ilikuwa dhambi juu ya Yehova Mungu. Angehakikisha kwamba mwendo wao wa kuasi ungepasishwa adhabu na haungesahauliwa na Mfalme Nebukadreza. Yerusalemu ungeshindwa na wakazi wake ‘kukamatwa kwa mkono’ na kuongozwa mateka mpaka Babeli. (Eze. 21:23, 24) Hilo vile vile lilimaanisha kwamba Mfalme Sedekia angelazimishwa kufanya ambavyo Yehova alikwisha tangaza kupitia kwa Ezekieli:

11, 12. Maneno ya Ezekieli 21:25-27 yalitimiaje kwa habari ya Mfalme Sedekia?

11 “Wewe, Ewe mtu mwovu, uliyetiwa jeraha kiasi cha kukuua, mkuu wa Israeli, ambaye siku yako imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho; Bwana [Yehova] asema hivi; Kiondoe kilemba, ivue taji; haya hayatakuwa tena kama yalivyo; kikweze kilicho chini, kakishushe kilichoinuka. Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa.”​—Eze. 21:25-27.

12 Kwa mwendo wake wa kuasi Mfalme Sedekia alijitia jeraha la kufisha. Jeraha hilo la kufisha lilimaanisha, si kifo cha amani kama mfalme-raia mwaminifu katika Yerusalemu, bali kifo cha aibu kama mhamishwa aliyefungwa, aliyeshushwa katika kiti cha enzi, bila mtoto, bila macho katika Babeli. Kwa sababu ya uasi wake, Sedekia alijionyesha kuwa ‘mkuu mwovu wa Israeli.’ Siku yake ya kula tunda chungu la uovu wake tayari ilifika. Sasa ulikuwa ni “wakati wa uovu wa mwisho,” si “uovu” wa Mfalme Sedekia, bali vile vile na “uovu” wa ufalme wote wa Yuda na wa Yerusalemu. Wakati wa “mwisho” huu ulianza katika mwaka wa kumi na tatu wa Mfalme wa Kiyahudi Yosia, wakati ambao Yeremia alianza kutoa unabii. (Yer. 1:1, 2; 25:3-11) “Mwisho” huu ulipofika Mfalme Sedekia hakuvua kilemba chake na taji kwa kujitolea. Matokeo haya alilazimishwa kiti chake cha enzi chenye fahari na mji vilipoharibiwa.

13. Katika mwaka wa 607 B.C.E. ni nini ‘kilichokwezwa’ na ni nini ‘kilichoshushwa’?

13 Uharibifu huo ulipotukia mwaka wa 607 B.C.E. ufalme wa mfano wa Mungu duniani, ukiwa na mzao wa Daudi ameketi juu ya ‘kiti cha enzi cha Yehova’ katika Yerusalemu, ulimalizika. Hii ilimaanisha mageuzi kabisa katika mambo ya ulimwengu. Kama mfano mdogo wa ufalme wa Yehova Mungu, Ufalme wa Yuda ulikuwa umekuwa “kilichoinuka.” Lakini ‘ulishushwa’ kwa kuharibiwa. Mataifa au wasio Wayahudi, hata hivyo, ‘walikwezwa,’ kwa kuwa uharibifu wa Ufalme wa Yuda uliuacha utawala wa Mataifa ukiitawala dunia yote.

YEYE AMBAYE ATAWATENDA WAVUNJAJI WA KUKUSUDIA WA AHADI

14. Ni nani “yeye ambaye ni haki yake,” na yu tofauti kabisa na Mfalme Sedekia namna gani?

14 Mataifa yasiyo ya Kiyahudi yalipaswa kuendelea na utawala huo mpaka kuja kwa yeye “ambaye ni haki yake,” mzao wa Mfalme wa Kiyahudi Daudi. Huyo ndiye akawa Bwana Yesu Kristo. Tofauti na Mfalme Sedekia mwovu, Yesu Kristo si mvunjaji wa ahadi. Yeye ni “mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote.” (Ebr. 7:26) Kama mwanadamu duniani sikuzote alisema kweli. ‘Hila yo yote haikuonekana kinywani mwake.’ (1 Pet. 2:22) Hivyo Yesu anawataka kama raia zake watu wanaosukumwa inavyofaa kuuiga mfano wake peke yao. Kwa kupatana na mapenzi ya Baba yake, karibuni atawachukulia tendo wote ambao, kama Sedekia wa kale, ni wenye kuasi na wasiotumainika, wasioliheshimu jina la Yehova.

15. Sababu gani ni hakika kwamba Yesu Kristo atatenda juu ya Kristendomu wakati wa kizazi hiki?

15 Tunajua kwamba Yesu Kristo atachukua tendo hilo katika kizazi hiki. Orodha ya tarehe ya Biblia inaonyesha waziwazi kwamba katika mwaka wa 1914 C.E. alipewa utawala juu ya ulimwengu wa wanadamu. (Dan. 4:16-27; 7:12-14; Ufu. 11:15) Kwa hiyo sasa yuko katika cheo cha kutenda juu ya jamii za watu na mataifa yasiyoiheshimu kweli na haki. Kristendomu leo, kama Yerusalemu asiye mwaminifu, ameshindwa kujiongoza mwenyewe kulingana na amri za Mungu. Kuvunja kwa ahadi nzito ni mojawapo tu ya dhambi alizofanya. Kwa hiyo, kama taratibu inayodai kuwa katika agano na Mungu, Kristendomu ndiye atakayekuwa wa kwanza kuangamizwa.

16. Jambo gani liliwapata Waamoni kwa utimizo wa Ezekieli 21:28-32?

16 Hiyo ni kulingana na mfano wa lililotukia nyakati za kale. “Upanga” wa kuadhibu uliwajia wakazi wa Yuda na Yerusalemu kwanza, watu ambao hawakuwa waaminifu kwa ujamaa wao wa agano na Mungu. Lakini “upanga” haukuachia hapo. Waamoni, kama Wayahudi wasio waaminifu, hawakujitoa kwa kilichokuwa haki na, kwa hiyo, wao vile vile walikuwa wa kuadhibiwa. Kweli, manabii wa Amoni hawakufikiri hivyo. Walikuwa ‘wakiona’ wokovu kwa mji mkuu wao Raba. Vile vile, waaguzi walikuwa wakitabiri kwamba mji ungeachiliwa. Lakini manabii na waaguzi walikosea. Walichokuwa ‘wakiona’ manabii kikawa “ubatili,” na matabiri ya waaguzi yakahakikishwa kuwa “uongo.” Hii ilikuwa ni wakati Nebukadreza alipoiharibu nchi ya Waamoni. Hivyo, kama ilivyosemwa mapema kupitia kwa Ezekieli, waliouawa wa Amoni ‘waliwekwa juu ya shingo’ za Waisraeli waovu waliouawa, kana kwamba walikuwa fungu moja la wafu.​—Eze. 21:28-32.

17. Sababu gani ni jambo la maana kwa watu leo kuchunguza mwendo wao wa maisha?

17 Kwa hiyo leo hakuna taifa ambalo limekuwa danganyifu kwa makusudi katika ahadi zake na mapatano litakalookoka adhabu. Hii inafanya iwe lazima kwa kila mtu kuuchunguza mwendo wake mwenyewe. Anaweza kujiuliza: Je! mimi ni mwigaji wa Yesu Kristo, ambaye ‘kinywani mwake haikuwamo hila yo yote’? Au, mimi naonyesha tabia za mvunjaji mwasi wa kiapo, kama alivyokuwa Mfalme Sedekia? Uzima wa kila mtu leo unategemea kushika mwenendo mwema. Hiyo inatia ndani na kutimiza ahadi nzito za mtu. Kushindwa kufanya hivyo kunaweza kuongoza kwenye kupoteza uzima.

​—Kutoka Kitabu “The Nations Shall Know that I Am Jehovah”​—How?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki