Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 2/1 uku. 72
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Habari Zinazolingana
  • Kila Mtu Ataketi Chini ya Mtini Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Atumia Mtini Kufundisha Kuhusu Imani
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Mwanzo wa Siku ya Mambo Makubwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Mwanzo wa Siku ya Mambo Makubwa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 2/1 uku. 72

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

●Kwa kuwa haukuwa wakati wa mitini, sababu gani Yesu aliulaani mtini ambao haukuwa na tunda, kama inavyoelezwa katika Marko 11:13, 14?​—U.S.A.

Yesu alipouona mtini huo ilikuwa ni Nisani 10 (Machi 28) ya mwaka wa 33 C.E. Kwa habari ya mitini katika nchi hiyo chipukizi za matunda ya majira hayo zinatokeza karibu Februari, juu ya matawi ambayo yanamea majira yaliyopita, lakini majani hayaonekani mpaka sehemu ya mwisho ya Aprili au Mei. Wakati mti huo unapofunikwa na majani inaupasa kuzaa matunda mabivu. Kwa kuwa mti ulioonwa na Yesu ulikuwa na majani mapema isivyo kawaida, angeweza kuutazamia kuwa na malimbuko yasiyo ya wakati wake ambayo yangefaa kwa kuliwa. Kweli ya kwamba mti huo haukuwa na tunda ilionyesha kwamba haungeweza kuzaa. Sura yake ilikuwa ya udanganyifu.

Yesu aliulaani mti huo, akiudhoofisha. Sababu gani? Kwa sababu tu ya sura yake ya udanganyifu? Kwa wazi Yesu alikuwa na kusudi la maana zaidi. Yalikuwa kweli mafundisho ya kujionea kwa macho kwa faida ya wanafunzi wake. Tunajifunza hili kutokana na sehemu ya pili ya habari hii, ambapo Petro alisema: “Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.” Na Yesu akajibu: “Mwaminini Mungu. . . . Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:20-22, 24) Ilikuwa ni imani ya Yesu katika Mungu iliyoifanya laana yake iwe na matokeo.

Zaidi, mti wenyewe ungefananisha taifa la kale la Kiyahudi, ambalo lilikuwa na sura ya kuzaa matunda kwa sababu ya kukamatana kwake kwa agano na Yehova Mungu, na kwa sababu ya kujionyesha kwa viongozi wa kidini wa Kiyahudi kuwa wenye haki. (Mt. 6:5; 23:25-28) Lakini, taifa hili lilikuwa limeshindwa kuzaa matunda mema kwa utukufu wa Mungu. Lilimkataa Yesu Kristo, yule yule aliyetumwa na Mungu na akafunuliwa wazi kuwa Mwana wa Mungu kwa miujiza yake na mafundisho. Lakini sababu gani taifa hili likamkataa Yesu? Kwa sababu ya kukosa imani katika Neno la Mungu. (Luka 13:5-9) Kwa sababu hiyo taifa hili lisilo na imani, lisilotubu, lilipaswa kunyauka na kufa kama vile ule mtini usiozaa.​—Mt. 21:43.

Sisi leo tunaweza kufaidika kutokana na mafundisho ya Yesu kuulaani mtini. Kama tungepoteza imani katika uwezo wa Mungu wa kujibu sala za watumishi wake na kuwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii, kufanya hivyo kungeongoza kwenye kukataliwa kwetu, kulaaniwa kwetu kama mitini isiyozaa. (Yohana 15:2-6; Ebr. 6:7, 8) Neno la Mungu linatuambia: “Pasipo imani haiwezekani kumpendeza [Mungu]; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”​—Ebr. 11:6.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki