Jina Ambalo Katika Hilo Mataifa Yote Yanachagua Kutembea
“Mataifa yote, kwa upande wao, watatembea kila moja katika jina la mungu wake; lakini sisi, kwa upande wetu, tutatembea katika jina la Yehova Mungu wetu kwa wakati usiojulikana, hata milele.”—Mik. 4:5, NW.
1. Ingawa wamegawanyika kwa njia ya kidini, watu wa taifa fulani wataabudu mungu gani wa kuungamanisha?
UMOJA wa Mataifa, kama tengenezo la amani ya ulimwengu na usalama, kwa sasa lina mataifa washirika 132. Kuna mataifa mengine nje. Kila mojawapo la mataifa ya kisiasa lina wazo linaloshikamanisha watu wake pamoja chini ya serikali moja. Kwa hiyo linatembea kwa jina la wazo hilo; hivyo ni kusema kwamba, linakwenda kama mfuasi wa wazo hilo. Kwao linakuwa mungu wanayeabudu na kumdhania kuwa juu ya mambo yote yao wenyewe wapendayo. Hivyo watu huenda wakawa wamegawanyika kwa njia ya kidini, na hali wataliabudu wazo hilo la kitaifa kama mungu wa kuungamanisha.
2. Mamilioni ya watu wanaodai kuwa makafiri wanajipingaje wenyewe kwa kweli?
2 Mamilioni ya watu wanadai kuwa makafiri, wasioamini kuwako kwa Mungu, wasioaminishwa kwa mungu ye yote. Lakini wanajipinga wenyewe kwa kuabudu mungu wa kitaifa. Tangu Mapinduzi ya Kiamerika (miaka ya 1775-1783) tumesikia mengi juu ya “mungumke wa Uhuru.” Au, mungu huyu anaweza kuwa kitu kinachoitwa demokrasi, utawala wa watu. Au, unaweza kuwa adui mkali wa demokrasi, yaani, Ukomunisti wa mataifa yote. Watu watashikamana na kanuni hizi za kisiasa kwa nguvu zinazokuwa kujitoa kunakopita kadiri kwa kidini. Mbali na hayo, kila mojawapo la mataifa hayo linalinda kwa choyo linachoona kama “enzi ya kitaifa,” kana kwamba ilikuwa mungu asiyepaswa kuharibiwa au kupotezwa. Katika mataifa mengine watu wengi wanaabudu serikali imara ya kijeshi itakayolipa taifa hali ya nguvu ya kupambana na mataifa mengine. Juu ya “mfalme wa kaskazini,” zamani za kale unabii ulisema: “Katika mahali pake atamheshimu mungu wa ngome.”—Dan. 11:38.
3. Mika 4:5 inakadiri sawa hali ya kutembea kwao namna gani, na namna gani Zaburi 96:5 inakadiri vema ubora wa miungu hiyo inayopendwa na watu wengi?
3 Mwandikaji aliyeongozwa na roho ya Mungu wa nyakati za kale alikadiri vizuri mwendo wa mataifa ya kisasa kwa kusema: “Mataifa yote, kwa upande wao, watatembea kila moja katika jina la mungu wake.” (Mik. 4:5, NW) Kila mmoja wa miungu hii anapendwa sana katika eneo lake mwenyewe. Hiyo ndiyo sababu, ikiwa mtu mmoja anayeijua hali yenyewe vema anakataa kufuatana na makutano, anaonewa chuki sana. Chuki inaonwa kwa kadiri ya kumchukulia tendo kali mkosaji. Lakini ulizo ni, “miungu” hiyo ya sanamu ina ubora gani? Inayaelekeza mataifa kwenye nini? Kwa maulizo haya hali iliyopo ya ulimwengu inapaswa kutoa majibu ya kusadikisha zaidi, zaidi kwa sababu ya mwendo usiogeuka wa mambo na hali za ulimwengu. Tunalazimishwa kukubali kwamba mwandikaji wa kale alikadiri vema juu ya miungu inayopendwa sana aliposema: “Miungu yote ya watu si kitu.”—Zab. 96:5.
4. Chaguo la watu mmoja mmoja leo ni kati ya mtendo gani, na ni nani leo wanaofanya chaguo liletalo salama?
4 Huu ndio wakati wa mataifa kuchunguza ubora wa miungu yao. “Miungu” iliyowatia katika matata haya yaliyopo haiwezi kuwaondoa mle na haiwezi kutegemewa kuwaondoa. “Mataifa” wasipoamka, basi, walau, watu mmoja mmoja wanapaswa kufanya hivyo, mbele ya mzunguko wa matukio ya kasi kasi ya ulimwengu kuwasukuma, kuwazamisha katika uharibifu. Kuvutwa kwetu kutoka kwenye mvuto huu wenye msiba kuja kwenye salama kunaweza kutokana na kumchagua Mungu anayefaa na kutembea katika jina la Mungu huyo. Ama tuchague kwenda upande mwingine, tukitembea katika jina la Mungu bora kuliko miungu yote ipendwayo sana ya jamaa za mataifa. Chaguo la mwendo huu wa pili, mwendo ulio haki, lingali linawezekana kwa wapenda uzima na furaha. Miaka ya karibuni mamia ya maelfu duniani kote wameamshwa kuona maana ya matukio ya ulimwengu na wamefanya chaguo lenye furaha. Bado si kuchelewa mno kwa wengine kufanya vivyo hivyo.
5. Je! unyofu peke yake ulisaidia katika kuchukua kwao mwendo huu wa kihodari, na sababu gani ndio mwendo unaofaa?
5 Ni mwendo wenye uhodari huo? Ndiyo, kweli kweli! Ili kuchukua mwendo wenye uhodari kama huo bila shaka unyofu unatakiwa. Unyofu wao kwa kuchukua mwendo huu hautiliwi shaka hata kidogo, lakini je! unyofu wenyewe kama unavyoonekana kwa kuchukua kwao mwendo huu unaufanya uwe mwendo unaofaa? Hapana! Hivyo, mwendo wenye uhodari ni kutiwa si katika unyofu peke yake, bali katika habari ya kutegemewa, ujuzi wa kweli. Na huu kwa uongozi wa kutumainika, ni bora kuliko uongozi wa miungu ambayo “si kitu.” Usawa wa mwendo huu unahakikishwa na ukweli wa kwamba ulisemwa mapema katika unabii ambao umekuwa si uongo bali ukweli. Sehemu zote za unabii huu ni kweli, kwa sababu unatoka kwa Mungu asiyeweza kushitakiwa kusema uongo na ye yote, kwa kuwa yeye hasemi uongo. Nyuma ya karibu zaidi ya miaka 4,000 ya matendo yake kwa wanadamu bado ingeweza kuandikwa juu yake Yeye: “Mungu hawezi kusema uongo.” (Ebr. 6:18; Tito 1:2) Huyu ndiye Mungu ambaye kwa jina lake watu zaidi na zaidi wanachagua kutembea leo.
6. Unabii huu unatoka katika nchi ya namna gani, na ulitolewa lini na nabii?
6 Kwa hiyo unabii ulioonyesha kweli tukio hili la siku zetu haukutoka mahali pa hadithi tu. Mahali hapa ni pa kihistoria—nchi inayojulikana ulimwenguni kote leo, ikisemwa sana katika habari—Israeli. Msemaji aliyeongozwa na Mungu wa unabii huo alikuwa mtu aliyeitwa Mika, aliyejijulisha kama akiishi katika mji wa Morashti katika eneo la kabila la Yuda na karibu maili 22 magharibi ya kusini ya Yerusalemu. Aliishi wakati wa utawala wa wafalme watatu wa kihistoria, yaani, “Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda.” (Mik. 1:1) Hiyo inamweka Mika katika karne ya nane mbele ya Wakati wetu wa Kawaida, na kwa hiyo lazima kutoa kwake kwa unabii kuwe kulimalizika mbele ya mwaka wa 716 B.C.E.
7. Ni nini juu ya Mika linalotia nguvu matumaini yetu katika unabii wake, na ni nabii gani wa nyumaye anayeelekeza kwa hili?
7 Lakini, linalopaswa kuyatia nguvu matumaini yetu kwamba Mika alikuwa nabii wa kweli wa Mungu wa kweli, anayeishi, si kuwa kwake mtu wa kihistoria tu, bali vile vile uhodari wake kutoa ujumbe wake ijapokuwa alihatirisha maisha yake kwa kufanya hivyo. Siku zake wafalme walikuwa na uwezo kweli kweli, uwezo juu ya uhai au kifo cha raia zao. (Mit. 16:14) Ubora huu wa nabii Mika unakaziwa fikira zetu wakati wa nyumaye ambapo nabii Yeremia katika Yerusalemu alitishwa kuuawa na viongozi wa Kiyahudi waliochukizwa na hotuba iliyoelekea kwao kupindua na kutokuza taifa. Ebu na tusome habari ya Yeremia mwenyewe juu ya hili:
8. Yeremia 26:16-19 panaonyeshaje mtajo huu wa unabii wa kihodari wa Mika?
8 “Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la [Yehova], Mungu wetu. Ndipo watu kadha wa kadha miongoni mwa wazee wa nchi wakaondoka, wakanena na mkutano wa watu, wakisema, Mikaya, Mmorashti, alitabiri katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda; akasema na watu wote wa Yuda, ya kwamba, [Yehova] wa majeshi asema hivi, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni. Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! hakumcha [Yehova], na kumwomba [Yehova] awafadhili; naye [Yehova] akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Na sisi tungetenda mabaya makuu juu ya [nafsi] zetu.”—Yer. 26:16-19.
9. (a) Mika alitimizaje matakwa matatu ya msingi ya nabii wa kweli? (b) Jina Mika lina maana gani, na Isaya 26:4 panasema ni njia gani inayofaa kutenda juu ya ulizo hilo lenye kutoa mwito?
9 Bila shaka, Mika alikuwa nabii wa kweli wa Mungu aliye mmoja wa kweli, akitimiza matakwa matatu ya msingi. Hivyo ni kusema: (1) Alisema kwa jina la Mungu wa kweli. (2) Unabii wake ulitimia. (3) Unabii wake ulielekea na kusaidia kuwageuza watu waaminifu kwa Mungu aliye mmoja wa kweli. (Kum. 13:1-5; 18:20-22) Bila shaka iwayo yote, Mika alitembea kwa jina la Mungu wake. Jina lake lile lile ni mwito kwetu sote tumlinganishe Mungu wake na miungu mingine yote ambayo “si kitu” wanayoabudu jamaa za mataifa, kwa kuwa jina lake la Kiebrania, Mika, linamaanisha “Ni Nani Anayelingana na Yah?” Njia inayofaa kwetu sisi kuitikia ulizo hilo lenye kutoa mwito ilishauriwa na nabii wa wakati ule ule wa Mika, yaani, Isaya, alipoandika: “Mtumainini [Yehova] sikuzote, maana [Yehova] YEHOVA ni mwamba wa milele.”—Isa. 26:4; 12:2.
MAHALI PA KUGEUKIA KATIKA HISTORIA
10. (a) Kwa kweli, jibu letu linapaswa kuwa nini kwa ulizo linalotolewa katika jina la Mika? (b) Ni ulizo gani linalotokea juu ya kujibu kwetu namna hiyo, na Mika alielekeza kwenye mahali gani pa kugeukia katika historia kwa uongozi wetu katika jambo hili?
10 Ikiwa tunataka kujibu ulizo lenye mwito lililo katika jina la Mika, mambo ya hakika yangetulazimisha kujibu: “Hakuna anayelingana na Yah Yehova!” Ikiwa hivyo, ulizo linalotujia ni, Tunafanya nini juu ya jambo hili? Kufanya kwetu lililo haki juu yake kungetia alama mahali pa kugeukia katika maisha yetu, hata katika maisha za watu wengi wanaodai kuwa Wakristo. Geuzi hili lingelingana na aliyosema nabii Mika mapema. Katika unabii wake alielekeza kwenye mahali pa kugeukia katika historia ya kibinadamu. Sivyo, hapa hatumaanishi unabii wa Mika kwamba Masihi au Kristo aliyeahidiwa angezaliwa kama mwanamume katika mji mdogo wa Bethlehemu katika nchi ya Yuda. (Mik. 5:2) Wakati wa utimizo wa unabii huo unatumiwa kama mwanzo wa anachoita Kristendomu “wakati wa Kikristo,” hata ingawa yeye hana hakika kabisa juu ya siku yenyewe ya kuzaliwa kwa Kristo. (Mt. 2:1-6; Luka 2:4-17) Haijatimia kabisa miaka 2,000 tangu wakati huo. Lakini mahali pa kugeukia katika historia ya kibinadamu ambapo tunazungumza ni pale palipofikiwa katika kizazi chetu wenyewe. Nabii Mika alielekeza hapo!
11. Ni kwa kuelekeza kwenye nini Mika akatanguliza unabii huu mtukufu, na sababu gani tunapaswa kutazamia kuuona utimizo wake katika kizazi chetu wenyewe?
11 Mika alitoa unabii juu ya matukio haya. Je! tunayaona yakitukia? Inatupasa kuyaona, kwa kuwa tu katika kipindi hicho cha historia. Mika alipoeleza katika unabii tunayoona yakitukia leo, aliyatanguliza kwa kusema mapema mahali ambapo pakawa pa kugeukia katika historia ya taifa lake mwenyewe. Unabii huu ulitimia karne iliyofuata nyuma ya Mika, na kwa hiyo hakuishi kuona unabii wake ukitimia. Kwa njia hiyo aliokoka mabaya ya kitaifa. Lakini mabaya haya juu ya taifa lake mwenyewe yamekuwa na kifani katika kizazi chetu cha kisasa, kwa sababu hiyo hili likistahili fikira zetu. Kwa hiyo ebu na tusome aliyoandika Mika na kuona namna yanavyotanguliza unabii mzuri mno unaotimia karne ii hii ya 20:
12. Katika Mika 3:9–4:1, ni hali gani mbaya ya kidini aliyoieleza nabii, na ni mageuzi gani aliyoonyesha mbele juu ya ‘mlima wa nyumba ya Yehova’?
12 “Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili. Wanaijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wale hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea [Yehova], na kusema, Je! hayupo [Yehova] katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia. Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni. Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya [Yehova] utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.”—Mik. 3:9 mpaka 4:1.
13. Kugeuka huko kwa matukio kulitukia lini katika nyakati za kale?
13 Je! mtajo huo kutoka katika Mika unasikika kama kugeuka upesi katika matukio ya taifa? Hapawezi kuwa na shaka kwamba sehemu kubwa ya mwisho ya unabii huu ni lazima itimie, kwa kuwa maneno ya unabii unaoitanguliza yalitimia kweli. Historia iliyoandikwa inaonyesha hili. Mwaka wa 607 B.C.E., karibu na mwanzo wa ambao kwetu ungekuwa mwezi wa Oktoba, mji wa huko Mashariki ya Kati unaoitwa kwa usemi wa mashairi “Sayuni” kweli uliachwa kama shamba tu lililolimwa. Ndiyo, mji mkuu wa kitaifa Yerusalemu uliachwa ukiwa kama boma la magofu.
14. (a) Wakati huo ‘mlima wa nyumba ya Yehova’ ulianza kuonekana kama nini? (b) Ni kwa sababu ya mazoea gani ya kidini na ya hukumu Yehova alikuwa amekusudia hili litukie?
14 Namna gani juu ya mlima wenye urefu wa futi 2,500 palipokuwa na nyumba ya ibada ya Yehova iliyokuwa imejengwa na Mfalme Sulemani ikiwa na uzuri wa kustaajabisha? Mlima huo mtakatifu ulianza kuonekana kama “mahali palipoinuka msituni.” Uliachwa kama kilele cha kilima kilichojazana miti. Je! hiyo ilikuwa aibu kwa Yehova Mungu? Inaelekea kuwa hivyo. Na hali alikusudia iwe hivyo, kwa kuwa alimwongoza nabii Mika kwa roho yake kuwa wa kwanza kutoa unabii wa mabaya kama hayo ya kidini. Alipaswa kabisa kufanya hivyo, zaidi kwa kuwa Yerusalemu ulikuwa ukijazwa na uovu wa matendo ya umwagaji wa damu. Je! kuna jambo jingine lililopaswa kutazamiwa kwa mji hali wakuu wake wakiacha wapofushwe wasitumie haki kwa kukubali rushwa, makuhani wa hekaluni wakiendeleza mafundisho ya kidini kwa bei isiyogeuka na manabii wa madanganyo wakiendesha uaguzi wa kishetani wapate fedha kutoka kwa watu wajinga? Na hali wanafiki hao wa kidini walijisikia kana kwamba walikuwa wakitembea kwa jina la Yehova, kwamba Yehova angeendelea kuwa katikati yao katika hekalu lake, kuwalinda na mabaya! Si ajabu kwamba unabii wa Mika, ijapokuwa wa kushtusha namna hiyo, ulitimia.
15. (a) Yehova alitumia njia gani kuyaleta mabaya ya kitaifa yaliyokwisha semwa mapema, na lini? (b) Ni nini kilitukia kwa vitu vya kiserikali na kidini Yerusalemu, na ni nini kilitukia kwa ubora wa Yehova kama mungu?
15 Dini sio ulinzi kwa wanafiki. Wanafiki hao wa kidini walikata tumaini la waliyotazamia kwa kosa kutoka kwa Yehova, ijapokuwa kile ambacho Mika alitumiwa kuonyesha mbele. Ni kwa njia gani, basi, Yehova aliwaletea mabaya ya kitaifa mwaka wa 607 B.C.E.? Ni kwa kuwatumia Wababeli chini ya Mfalme Nebukadreza. Nyuma ya karibu miezi kumi na minane ya kuuzingira Yerusalemu, jeshi la Kibabeli liliingia kwa nguvu katika mji, likauteka pamoja na hekalu lake, likawachukua waokokaji wenye msiba mateka, na kuuteketeza mji mtakatifu. Kiti cha enzi chenye fahari, ‘kiti cha enzi cha Yehova,’ kama kilivyoitwa, ambacho juu yake ukoo wa wafalme wa jamaa yenye fahari ya Daudi walikalia kilitoweka, vile vile na “sanduku la ushuhuda” la Yehova lililokuwa katika chumba cha ndani sana, “Patakatifu Sana,” pa hekalu. Hivyo ufalme wa Daudi, ukiwa wa miaka 463 katika Yerusalemu, uliangushwa. Vile vile, ibada yote ya Yehova katika hekalu lake ilikatizwa. Kukadiriwa kwa Yehova kama mungu kulishuka mara moja kati ya mataifa ya kipagani. Ibada yake Yeye ilishuka mara moja kwa kukadiri kwa mataifa ya ulimwengu. Jina lake takatifu lilionekana lililonajisiwa.
16. Mataifa ya kipagani yenye kutazama yalielekea kuamini nini juu ya kuinuka tena kwa ibada ya Yehova katika Yerusalemu, na sababu gani?
16 Je! ibada ya Yehova ingeinuka tena? Bila shaka hilo ndilo lililokuwa ulizo katika akili za wapagani wengi wenye kupendezwa. Kama wangalijua na kuamini unabii wa Mika na Isaya na Yeremia na manabii wengine wa Yehova wangalijua jibu kuwa Ndiyo! Lakini wapagani wasioamini na wale walioidharau ibada ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo walidhani sivyo. Mwaka nyuma ya mwaka ukapita, mpaka mwaka wa 70, na ibada ya Yehova haikurudishwa katika mji mtakatifu. Yerusalemu uliendelea kuwa boma la magofu; Sayuni uliendelea kuwa kama shamba tu lililokwaruzwa-kwaruzwa kana kwamba kwa kulimwa. Mlima wa hekaluni ukawa kama kilima kilichoachwa katika mwitu. Pahali pa muziki na nyimbo za vyombo za hekaluni, sauti kali, zisizopendeza za ndege na wanyama wa porini zilitokea kule. Wapagani wenye kutazama wa karibu walionekana kuwa na sababu ya kuamini kwamba, watu wa Yehova wakiwa uhamishoni Babeli kwa wingi, ibada yake ingekwisha.
17. Ni mfuatano gani wa matukio uliotokea juu ya Babeli, na tawi jingine la jamaa ya kibinadamu lilichukuaje mamlaka ya ulimwengu?
17 Lakini, ye yote asidhani kwamba ibada ya Mungu wa kweli inaweza kufutiliwa mbali! Wale walioridhika kutokana na kuharibika vibaya kwa ibada ya Yehova hawakujua kwamba matukio yangefuatana karibuni. Mwisho wa miaka 68 ya kuachwa kwa Yerusalemu ukiwa bila mwanadamu au mnyama wa kufugwa, Mamlaka ya Tatu ya Ulimwengu yenye nguvu ya historia ya Biblia ilianguka. Kama ilivyosemwa mapema na manabii wa Mungu asiyesema uongo wakati wo wote, Yehova, milki ya Babeli ilianguka. Babeli kwa kutumia majeshi yake ya kutisha alikuwa ameliharibu hekalu la Yehova Yerusalemu kwa ruhusa yake, lakini hakuachwa bila kuadhibiwa kwa tendo hilo la kiburi la kumtusi Mungu aliye mmoja anayeishi na wa kweli. Mamlaka ya Ulimwengu kwa watawala wa ukoo wa Shemu ilikoma. Kwa mfuatano wa matukio, mamlaka ya ulimwengu kwa watawala wa ukoo wa Yafeti ilianza, kuendelea hata siku zetu wenyewe. Mshindi wa Kiajemi, Koreshi Mkuu, akawa mfalme wa Babeli na wa Mamlaka ya Nne ya Ulimwengu ya historia ya Biblia. Dini ya Kibabeli ikaanguka. Mungu wake mkuu, Merodaki au Marduk, alianguka katika aibu.
18. (a) Ni unabii gani wa Yeremia juu ya mungu wa Babeli na nchi yake ulikaribia kuanza kutimia? (b) Ukiwa wa Babeli umelinganaje na ule iliouletea Yerusalemu?
18 Ukawa wakati wa maneno ya nabii Yeremia kutimizwa: “Tangazeni katika mataifa, mkahubiri na kutweka bendera; hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli [Bwana] amefedheheka; Merodaki amefadhaika; . . . Maana toka kaskazini taifa [limekuja] juu yake, [linaloifanya] nchi yake kuwa ukiwa; wala hapana mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.” (Yer. 50:2, 3) Unabii huu una maana kwetu leo. Ni wapi, twaweza kuuliza, ilipo Babeli katika Mto Frati ulio katika inayoitwa leo Iraq? Ni magofu tu, ikiwa na msiba kama ule iliyouletea Yerusalemu wa kale, ila tu ukiwa wake umeendelea kwa karne nyingi zaidi ya miaka 1,000, kwa maana ukiwa wa Yerusalemu ulikuwa wa miaka 70 tu.
YEHOVA ANACHUKUA UWEZO WA KUTAWALA KAMA MUNGU
19. Nyuma ya Uajemi kuishinda Babeli, ni mungu gani aliyepata heshima, na mungu huyu alimtumia nani kwa kulirudisha hekalu lake?
19 Wakati wa kuanguka kwa Babeli mwaka wa 539 B.C.E., ni mungu gani aliyekwea kuwa na heshima ya mataifa yote? Ni mungu wa kitaifa wa Waajemi washindi au ni mungu wa wahamishwa katika Babeli, Yehova? Unabii wa Mika, pamoja na unabii wa wanaume wengine walioongozwa na roho takatifu ya Mungu, ulionyesha kwamba Yehova angechukua uwezo wa kutawala. Alifanya hivyo, kuhakikisha kwamba unabii wake haushindwi. Alisema Mika chini ya uongozi wa roho ya Mungu: “Itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya [Yehova] utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.” (Mik. 4:1) Ili kuleta utimizo mkubwa au wa mfano wa unabii huo wenye kutoa mwito, Yehova Mungu alimtumia Mfalme Koreshi Mkuu kama chombo, mwabudu mungu mkuu wa Uajemi mshindi. Yehova, kwa ukuu wake Yeye, alimfanya mwabudu mungu wa uongo amfanyie kazi Yeye ya kulirudisha hekalu la Yerusalemu.
20. Ni kwa utimizo wa unabii gani juu ya mshindi wa Kiajemi hili likatukia, na lini na namna gani?
20 Namna gani hivyo? Basi, Yehova alisema juu yake kama “nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.” (Isa. 44:27, 28) Mfalme Koreshi alitimiliza kabisa jambo ambalo Yehova alifurahia, ingawa hili lilitofautiana na ambalo mungu wa kitaifa wa Uajemi angalifurahia kufanya. Mwaka wa 537 B.C.E., mwaka wa 70 wa ukiwa wa Yerusalemu na hekalu lake, Yehova aliichochea roho ya Koreshi kutangaza kwamba hekalu linapaswa kujengwa upya Yerusalemu. Kwa sababu hiyo Koreshi alitangaza kwamba wahamishwa katika Babeli ambao wangejitolea kwa kazi hii ya hekalu wanapaswa kufunguliwa Babeli na kuurudia “mlima wa nyumba ya [Yehova].” (2 Nya. (Sik.) 36:20-23; Ezra 1:1-4) Mwishoni mwa mwaka huo wa 70 wa ukiwa wa Yerusalemu mabaki ya waaminifu wa kujitolea kwa kazi ya hekalu waliirudia nchi ya Yuda, wakiumaliza ukiwa wake. Katika masika ya mwaka uliofuata (536 B.C.E.) msingi wa hekalu la pili la Yerusalemu uliwekwa.—Ezra 3:8-12.
21. Ijapokuwa nini hekalu la Yehova la pili likamalizwa, na wakati gani?
21 Hili halikuwapendeza wapinzani wa kipagani wa ibada ya Yehova. Lakini upinzani wao haungeweza kumshinda Mungu Mwenyezi. Kwa hiyo, nyuma ya miaka ya upinzani mkali wa wapagani hawa wenye kiburi, hekalu la pili la Yehova katika Yerusalemu lilimalizwa na mabaki wake waaminifu wakati wa majira ya baridi, siku ya tatu ya mwezi wa Adari mwaka wa 515 B.C.E.—Ezra 6:15.
22. Ni kwa njia gani ‘mlima wa nyumba ya Yehova’ ‘uliwekwa imara juu ya milima,’ kwa habari ya mabaki waliorudishwa na kwa habari ya mataifa ya kipagani na makundi ya watu?
22 Ili watumiwe kwa kufanya hili, mabaki waliorudishwa iliwalazimu kuiinua ibada ya Yehova juu ya mambo mengine yote katika maisha zao, na kuacha ibada ya miungu ya uongo ambayo babu zao walichagua kwa kukosa uaminifu. Ibada ya Yehova, kama inavyofananishwa na “mlima wa nyumba ya [Yehova],” iliinuka juu ya cheo bora ambacho mataifa ya kipagani yalikipa miungu yao ya kishetani, hii ikiabudiwa nyakati nyingi katika sehemu za asili za juu kama vileleni vya vilima na milima. Kwa maana ya mfano, mlima wa nyumba ya Yehova ya ibada ‘uliwekwa imara juu ya milima’ na ‘ukainuliwa juu ya vilima.’ Heshima kwa ibada ya Yehova ilichukua cheo cha juu, si kati ya watu wake wateule peke yao lakini vile vile kati ya watu mmoja mmoja wa mataifa ya kipagani na makundi ya watu. Bila shaka wengi wa watu hao walikuja mpaka Yerusalemu kumwabudu Mungu wa kweli, kama vile walivyofanya waongofu wa kidini siku za mitume wa Kikristo na kama vile alivyofanya towashi yule mkuu wa Ethiopia, ambaye mwinjilisti Filipo aliagizwa kugeuza kwenye Ukristo.—Matendo 2:5-10; 8:26-39; Yohana 12:20, 21.
23. (a) Watu hao mmoja mmoja kutoka kwa mataifa na makundi ya watu walianza kutembea kwa jina la nani? (b) Huo ulikuwa utimizo wa namna gani wa unabii, na, tangu kuja kwa Masihi, ni ulizo gani linalotokea juu ya kutembea kwa jina hilo?
23 Pahali pa kutembea kwa jina la miungu yao ya kwanza, watu hao wa mataifa yote mbalimbali na makundi ya watu walitembea kwa jina la Mungu ambaye ibada yake ilikwezwa juu zaidi, Yehova. Kwa kweli huo ulikuwa utimizo wa unabii wa Mika. Lakini utimizo mdogo tu, wa sehemu au wa mfano. Utimizo wote haukutukia nyuma huko mbele ya Yehova Mungu kumtuma Masihi wake duniani. Utimizo wa mwisho, wa kufikia upeo ulipangiwa karne yetu ya 20. Je! unatukiaje? Je! ni kwa sababu tunaishi katika karne ambapo Kristendomu amekua kwa kadiri kubwa zaidi, au kufikia washiriki wanaokadiriwa kuwa mia tisa milioni na zaidi kati ya mataifa duniani kote? Na je! hili halikuleta geuzi? Tangu kuja kwa Masihi au Kristo, je! silo jambo linalofaa kutembea kwa jina la Masihi, Yesu, pahali pa jina la Yehova? Je! makanisa ya Kristendomu ndiyo utimizo wa unabii wa Mika? Inatakiwa hili lichunguzwe—hapa!