Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w73 1/1 kur. 23-24
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Habari Zinazolingana
  • Arusi za Kikristo Zapaswa Kuonyesha Kiasi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Ongeza Shangwe na Heshima ya Siku Yako ya Arusi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Jinsi ya Kupanga Harusi Itakayomletea Yehova Heshima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2025
  • Ni Arusi ya Namna Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
w73 1/1 kur. 23-24

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Je! inafaa kwa Mkristo kuvaa pete ya arusi?​—Greece.

Wakristo wengi wenye mioyo minyofu wameuliza ulizo hili kwa kutaka kuepuka desturi ambazo huenda Mungu hazikubali. Waulizaji wengine wanajua kwamba askofu wa Kikatoliki John H. Newman aliandika: “Matumizi ya mahekalu, na haya yaliyowekwa wakf kwa watakatifu maalum, . . . mavazi ya kikasisi, kipara cha utosini, pete katika ndoa, kugeuka kuelekea Mashariki, sanamu za nyumaye, labda wimbo wa kidini, na Kyrie Eleison (sala ya rehema), yote yana chanzo cha kipagani, na yanatakaswa kwa mwingizo wake katika Kanisa.” (An Essay on the Development of the Christian Doctrine, 1878)a Ingawa mambo ya kweli yanahakikisha kwamba nyingi za desturi za kidini za siku hizi zinazotajwa na Newman bila shaka ziliingizwa kutoka kwenye ibada ya kipagani, je! ndivyo na pete ya arusi?

Kwa kweli kuna maoni yenye kupingana juu ya chanzo cha pete ya arusi. Ebu na tutoe mifano michache: “Kwanza . . . pete ilikuwa pingu, iliyotumiwa kumfunga bibi-arusi mtumwa.” (For Richer, for Poorer) “Pete ni kitu cha siku hizi kinachosimama pahali pa sarafu ya dhahabu au kitu kinginecho cha bei kubwa ambacho mwanamume alitumia kumnunua mke wake kutoka kwa babaye.” (The Jewish Wedding Book) “Pete ya arusi inadhaniwa kuwa ina asili ya Kirumi, na kwamba ilitoka kwenye desturi ya kale ya kutumia pete kwa kufanya mapatano.” (American Cyclopoedia) “Maelezo mbalimbali yametolewa juu ya kukamatana kwa pete na ndoa. Inaelekea kwamba pete za arusi zilivaliwa na Wayahudi mbele ya nyakati za Kikristo.”​—The International Cyclopaedia.

Kwa hiyo inaonekana kwamba asili iliyo sawa kabisa ya pete ya arusi haijulikani vyema. Hata ikiwa ni kweli kwamba wapagani ndio waliotumia pete za arusi kwanza, je! hii ingewakataza Wakristo kuvaa pete? Sivyo kwa lazima. Vitu vingi vya nguo vya siku hizi na namna za maisha vilitoka katika nchi za kipagani. Sehemu za siku hizi zilizogawanywa za saa, dakika na nukta zina msingi wa taratibu ya zamani ya Kibabeli. Hata hivyo, hakuna katazo kwa Mkristo kutotumia sehemu hizi zilizogawanywa za wakati, kwa maana kufanya hivyo kwa mtu hakutii ndani kuendesha kwa mazoea ya dini ya uongo.

Kweli, kupendezwa kwetu ni kukubwa zaidi juu ya matumizi ya pete za arusi, kwa kuwa kunakamatana, si na mambo madogo ya kimwili, lakini na hali ya ndoa, ambayo Mkristo kwa haki anaiona kama takatifu mbele za Mungu. Kwa kweli, jambo la maana si kama pete za arusi zilitumiwa kwanza na wapagani bali ni kama kwanza zilitumiwa kama sehemu ya mazoea ya dini ya uongo na kama zingali ina maana ile ile ya kidini. Kama ilivyoonyeshwa, uhakika wa kihistoria hauruhusu mwisho wa wazi juu ya habari hii. Je! Biblia inasema nini juu ya matumizi ya pete?

Biblia inaonyesha kwamba wengine kati ya watumishi wa Mungu wakati uliopita walivaa pete, hata zile ambazo zilikuwa na maana ya pekee. Kuvaa pete yenye muhuri kulionyesha kwamba mtu alikuwa amepewa uwezo wa kutenda akimwakilisha mtawala mwenye pete yenyewe. (Mwa. 41:42; Hes. 31:50; Esta 8:2, 8; Ayubu 42:11, 12; Luka 15:22) Kwa hiyo, ingawa pete za arusi hazitajwi, waabudu hawa wa kweli kwa wazi hawakutia shaka juu ya kutumia pete kwa mapambo.

Watu wengine wanasema kwamba pete ya arusi inasimama pahali pa upendo wa mtu usiokwisha na kujitoa katika ndoa. Talaka inayoongezeka katika nchi nyingi ambapo watu waliooa wanavaa pete ya arusi inaonyesha kwamba maana hii ni ya kudhaniwa wala si ya kweli. Hata hivyo, kwa watu walio wengi, kutia na Wakristo, katika nchi ambazo pete za arusi ni za kawaida, pete ni onyesho la wazi kwamba anayeivaa ameoa. Katika sehemu nyingine jambo ili hili linaonyeshwa kwa njia tofauti, kama vile mwanamke kuvaa mtindo fulani wa nguo.

Kweli, pete ya arusi kwa vyo vyote si takwa la Kikristo. Mkristo fulani huenda akaamua kutokuvaa pete ya arusi, kwa sababu ya dhamiri, kupenda kwa mtu mwenyewe, gharama, desturi ya anapoishi mtu, au kwa sababu nyingine yo yote. Mkristo mwingine anaweza kuamua kuonyesha kwamba ameoa kwa kutumia pete ya arusi. Hivyo, kwa mchanganuo wa mwisho uamuzi ni wa mtu mwenyewe, wa kufanywa kulingana na maoni ya dhamiri ya mtu.

[Maelezo ya Chini]

a Kitabu hiki kiliandikwa wakati Newman alikuwa yungali Mwanglikana, na kilichapwa mwaka wa 1845. Nyuma ya kugeuka na kuingia katika Ukatoliki, Newman alichapa chapa nyingine iliyosahihishwa katika mwaka wa 1878. Mwaka uliofuata alifanywa Askofu katika kanisa la Katoliki.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki