Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w26 Aprili uku. 32
  • Jinsi ya Kuelewa Lugha ya Picha Katika Biblia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jinsi ya Kuelewa Lugha ya Picha Katika Biblia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2026
  • Habari Zinazolingana
  • Kichwa cha Mazungumzo
    Huduma Yetu ya Ufalme—1989
  • Kichwa cha Mazungumzo
    Huduma Yetu ya Ufalme—1989
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2026
w26 Aprili uku. 32

DOKEZO LA KUJIFUNZA

Jinsi ya Kuelewa Lugha ya Picha Katika Biblia

Biblia inatumia mara nyingi lugha ya picha. Hata hivyo, ni vigumu kwa wasomaji wengi wa Biblia kuelewa lugha hiyo ya picha. (Mt. 13:13) Ni nini kinachoweza kukusaidia kuelewa mifano hiyo inayotumiwa katika Biblia? Jaribu mambo yafuatayo:

  • Tambua habari inayozungumziwa na picha inayotumiwa. Lugha za picha zinalinganisha habari fulani na picha. Kwa mfano, Ufunuo 3:3 inalinganisha kuja kwa Yesu (habari) na kuja kwa mwizi (picha).

  • Tambua jinsi habari inayozungumziwa inavyofanana na picha hiyo. Tafuta mambo na sifa zinazofanya habari na picha hiyo zifanane.

  • Fikia mkataa ulio sahihi. Baadhi ya mambo yanayofanana kati ya habari inayozungumziwa na picha, yanaweza kusababisha tufikie mkataa usio sahihi. Katika mfano uliotajwa awali, Yesu haji kuiba chochote. Badala yake, muktadha unaonyesha kwamba kuja kwake kutakuwa kama kuja kwa mwizi katika maana ya kwamba kuja kwake kutakuwa bila kutarajiwa au kutangazwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki