Sasa Haogopi
Barua moja iliyopokewa hivi majuzi na afisi ya tawi ya Ujeremani ya Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi inasomwa hivi, kwa sehemu:
“Diana ana umri wa miaka saba na tangu alipozaliwa amesumbuliwa na ugonjwa wa kupooza wenye kukazanisha-kazanisha misuli yake mara kwa mara. Kwa kuwa ni lazima yeye ahudhurie shule ya pekee iliyoko kilometa nyingi kutoka kwenye maskani yao, ni lazima aende kulala jioni-jioni saa moja ili aweze kuamka kesho yake ifikapo saa kumi na mbili ya asubuhi. Sikuzote yeye amekuwa akiogopa kuwa chumbani peke yake. Kwa hiyo sisi tulitia kaseti-rekoda humo na hapo kwanza tukafungulia kaseti za muziki, lakini hiyo haikusaidia. Zaidi ya hilo, mimi nilimtaka asikilize kitu cha kuelimisha ambacho angeweza kuelewa.
“Ndipo utatuzi mzuri ajabu ulipokuja—mirekodio ya kaseti za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nilimnunulia hiyo, na kwa ghafula Diana akawa haogopi tena. Yeye amejifunza kukariri moyoni kumi za hadithi zile—neno kwa neno—na anajua zile nyingine kwa kadiri ya kuweza kugundua kikosa cho chote unachoweza kufanya unapomsomea hadithi hizo, hata ingawa bado yeye mwenyewe hawezi kusoma. Tangu alipojifunza hadithi 69, ‘Msichana Anamsaidia Mwanamume Mwenye Nguvu,’ yeye amekuwa akiongea na walimu wake na watoto shuleni juu ya hadithi anazojua.”
Je! kaseti hizi, pamoja na kile kichapo chenye picha za kupendeza Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, zingefaa kuongezwa kwenye maktaba ya mtoto wako? Ni mtoto gani ambaye hangesisimuka kuwa na kisimulizi kama hicho kilicho tayari ili yeye asomewe mchana au usiku? Kaseti hizi, na pia kitabu kile, zinaweza kuagizwa kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.
Tafadhali nipelekeeni, mkiwa mmelipia malipo ya posta, ile pakiti ya kahawia yenye kanda za kaseti nne za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nawapelekea Kshs. 150.00 (Tshs. 640.00). [ ] Nipelekeeni kile kichapo chenye picha cha kurasa 256, Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, ambacho kwa ajili yacho nawapelekea Kshs. 40.00 (Tshs. 200.00). [ ] Tia alama ya kimoja au vyote viwili, na utupelekee mchango sahihi.