Maktaba Iliyojaa Habari
Hivyo ndivyo wasomaji wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! wanavyoyachukua magazeti hayo.
Akiandika kwa niaba yake mwenyewe na jamaa yake, mwanamume mmoja wa Ufilipino aliishukuru Sosaiti yetu kwa kumpa matoleo ya kule nyuma, akisema:
“Kama inavyokuwa katika kila chapa ya magazeti yenu, matoleo hayo yamejaa habari za maana. Si kwamba yanaangaza tu nuru juu ya mambo ya dini, bali pia yanazungumza kirefu juu ya mambo kama sayansi, tiba, historia, serikali, lugha, n.k. Inaelekea kwamba kila toleo linakuwa na makala za kutupendeza sisi kwa njia ya pekee.
“Ingefaa pia nitaje kwamba tuliunganisha matoleo yetu ya wakati uliopita ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! yakawa vitabu. Sasa tuna mabuku manne ya namna hiyo katika maktaba yetu wenyewe. Yanafaa sana kwa uchunguzi, nasi tunayarejea-rejea tupate mauidha na kichocheo chenye msaada.”
Unaweza kupata Mnara wa Mlinzi na Amkeni! katika sanduku la posta. Tupelekee Kshs. 97.00 (Tshs. 480.00) nawe utapokea magazeti yote mawili (nakala tatu kwa mwezi) kwa muda wa mwaka mmoja.
Tafadhali mnipelekee uandikisho wa mwaka mmoja wa magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Mimi nimewapelekea Kshs. 97.00 (Tshs. 480.00) kwa matoleo 36.