Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w83 9/15 uku. 23
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
w83 9/15 uku. 23

Maswali kutoka kwa Wasomaji

◼ Yesu alimwambia hivi mtu mmoja aliyekuwa amemponya: Usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.” je! alimaanisha kwamba tunakuwa wagonjwa kwa sababu tumetenda dhambi?

Hapana, si lazima iwe kwamba kila ugonjwa unatokana na dhambi fulani. Yohana sura ya tano inaeleza kwamba Yesu aliponya mtu aliyekuwa amekuwa mgonjwa miaka mingi. Baadaye Yesu alimwona mtu huyo katika eneo la hekalu na akamwambia hivi: “Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.”—Yohana 5:14.

Sisi sote tumerithi dhambi na hali ya kutokamilika kwa Adamu. (Warumi 5:12) Ushuhuda mmoja wa kuonyesha hivyo ni kwamba tunakuwa na “kawaida” ya kupatwa na ugonjwa nyakati fulani. Ni wazi kwamba mtu aliyeponywa na Yesu alikuwa mgonjwa kwa sababu ya hali ya kutokamilika aliyorithi. Kwa rehema ya Mungu mtu huyo aliponywa na kuonyeshwa njia ya wokovu kupitia Kristo. Baada ya hapo alipaswa kumfuata Mwokozi. Ikiwa, badala ya kufanya hivyo, mtu huyo aligeukia dhambi ya makusudi, jambo baya zaidi lingempata; angekuwa na hatia ya kutenda dhambi juu ya roho, na jambo hilo lingemstahilisha uharibifu wa milele.​—Mathayo 12:31, 32.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki