Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 7/15 uku. 335
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Habari Zinazolingana
  • Kushughulika na Maulizo ya Dhamiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1973
  • Je, Ni Lazima Ulipe Kodi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Sehemu ya Mamlaka za Juu Zaidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kutohesabu Maisha Zetu Kuwa Zenye Thamani Mno
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 7/15 uku. 335

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

● Mkristo akikamatwa kisha ahukumiwe na mamlaka za kilimwengu alipe faini kwa sababu ya kufuata mwendo unaopatana na Maandiko, je! lingekuwa tendo la kukubaliana nao kwa kuacha yaliyo haki akiilipa? Akipewa uchaguzi ama wa kulipa faini au kutumikia kifungo jelani, je! hii ingebadili mambo?

Yesu Kristo alitangulia kusema kwamba wafuasi wake ‘wangepelekwa mabarazani’ na “kuchukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yake, kuwa ushuhuda kwao.” (Marko 13:9) Hatua hiyo rasmi juu ya Wakristo huenda ikawa kwa sababu ya kuhubiri kwao habari njema za Ufalme au kwa sababu ya tendo jingine linalohusu dhamiri yao ya Kikristo. (Linganisha Matendo 4:1-3, 18-21; 5:27-40; 1 Petro 4:15, 16.) Huenda baraza ikahukumu kwa kuwapinga nayo hukumu huenda ikahitaji walipe faini. Huenda hii ikawa ndiyo adhabu ya pekee au huenda ikawa kama uchaguzi wa kwenda jela au huenda ikawa sehemu ya adhabu inayotia kufungwa na kulipa faini pia.

Zamani mashahidi wa Yehova kwa ujumla wamekataa kulipa faini utendaji wao wa kuhubiri ulipohusika. Ilionwa kwamba kulipa faini kunaweza kuonwa kama kukubali mtu alifanya kosa halisi. Ilionwa pia kwamba kukataa kulipa na kufungwa badala yake kunaweza kusaidia kuleta matokeo mazuri zaidi katika “kuitetea Injili na kuithibitisha.” (Flp. 1:7) Mara nyingi hii ilileta matokeo mengi mazuri, ikavutia wakuu kwa imara ya uamuzi wetu kumtumikia Mungu, na kwa wazi ilikuwa na baraka ya Yehova. Na nyakati nyingine leo huenda ukaonwa kuwa mwendo wa hekima kufuata kwa sababu ya hali zilizoko. Walakini, ulizo linalotuhusu hapa hasa ni kama kulipa faini kunakubalika kulingana na Maandiko au sivyo.

Faini zinatajwa katika Biblia nazo zilitumiwa katika agano la Torati kama namna ya adhabu. (Kum. 22:19; linganisha Kutoka 21:29-32; Mithali 19:19; 21:11.) Ezra 7:26, NW aonyesha kwamba maafisa wa Uajemi walipanga “faini ya pesa” kama namna ya adhabu pamoja na kifungo, uhamisho na kifo. Nyakati za kisasa, kama kinavyosema World Book Encyclopedia cha mwaka wa 1973, “Mara nyingi faini ni adhabu ya uvunjaji mdogo wa sheria.”

Kwa hiyo faini isichanganywe na jitihada ya mkosaji ‘kununua’ njia yake ya kuepuka kifungo. Si kama hongo ambayo Gavana Feliki alitumaini kupata kwa mtume Paulo na ambayo Paulo hakulipa. (Matendo 24:26, 27) Kwa hiyo, Mkristo anaweza kwa kufaa kuona faini aliyotozwa kama namna ya adhabu na, ingawa huenda akatosheka kwamba hakuwa mwenye hatia ya kosa, kwa kuwa alitenda kupatana na Neno la Mungu, huenda dhamiri yake ikamruhusu kuilipa faini kwa kunyenyekea mamlaka zilizo kuu za ulimwengu. (Rum. 13:1, 2; 1 Pet. 2:13, 14) Ingawa ni kweli kwamba kulipa faini kunaweza kumaanisha tunakubali tu wenye hatia katika akili za watazamaji, ni kweli pia kwamba kufungwa kungemaanisha lile lile katika akili za watazamaji wengi. Hatushughuliki hasa na maoni ya watu wa ulimwengu bali na ya Mungu. Kama tunalipa faini au kutumikia hukumu ya kufungwa, yote ni kwa sababu ya kushikilia kwetu ‘kutii Mungu kama mtawala kuliko wanadamu.​—Soma Matendo 5:29, 32; Waebrania 10:34; Wafilipi 3:8, 9.

Kupewa uchaguzi wa ama kulipa faini ama kufungwa kwa ujumla kunaonyesha kadiri fulani ya rehema ya hukumu au huruma. Watu wanaohukumiwa kuwa hatari kweli kwa mtaa kwa kawaida wanafungwa, lakini faini zinatozwa kama adhabu isiyo kali sana inayoruhusu mtu aishi na jamaa yake na aendelee na kazi bila kukatizwa, bila ya mtu huyo kuondolewa asiishi na jamaa yake na asiishi mtaani kwa kuzuiwa jelani. Hakuna lo lote katika Maandiko linalokataza Mkristo asitumie mpango huu wenye huruma kwa faida yake, wala Maandiko hayatutaki tufuate mwendo utakaolazimisha wakuu waonyeshe upinzani wao kwa ufalme wa Mungu ni mwingi kadiri gani. (Kwa kutofautisha, linganisha shauri la mitume katika Warumi 13:3, 4; Tito 3:1, 2; 1 Petro 2:12-17; 3:13-16.) Uchaguzi ukitolewa wa ama kulipa faini au kufungwa, hapo Mkristo huenda akaona kwamba anaweza kutimiza mengi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya habari njema kwa kulipa faini na kuendelea kuwa na uhuru wa kutenda. Ni shauri la uamuzi wa mtu mwenyewe kulingana na dhamiri ya mtu na uamuzi wa uangalifu, nao uamuzi wa mtu usilaumiwe-laumiwe na wengine kundini akiamua kulipa faini au akiona ni afadhali avumilie kufungwa.

Faini zinaweza kutozwa na wengine wasio maafisa wa kiserikali; kwa mfano, na vyama vya biashara nyakati ambapo dhamiri ya Mkristo haitamruhusu aingie katika utendaji fulani wa chama anaouona kuwa tofauti na kanuni za Maandiko. Hapa, pia, anaweza kuona kwamba kulipa kwake faini ni kuadhibiwa tu isivyo haki kwa sababu ya kuwa Mkristo.​—1 Pet. 2:19, 20; 3:17; linganisha Mithali 17:26.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2026)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2026 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki